Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, October 28, 2024

DAKTARI AFUNGUKA MADHARA YA KUCHANGANYA ENERGY NA POMBE KALI.




Na Dustan Shekidele,Morogoro.

JUMATATU iliyopita Mtandao Pendwa wa Shekidele, ulizindua kipengele kipya cha habari kali ya [Jumatatu ya kitaa].

Jumatatu iliyopita tulizindua kipengele hiKi kwa habari ya madhara ya kumkatisha mtoto zima la Mama kabla miaka 2 inayohitajika kisheria.

Kwenye habari hiyo Daktari Sadick Juma na Mzazi Farham Abraham ambaye pia ni mfundaji ‘Somo’ na Mtangazaji Maarufu wa Planet Radio,wawili hao walidadavua kwa weledi madhara ya mzazi kumkatisha mtoto zima.

Baada ya habari hiyo iliyosomwa na watu wengi kuruka hewani siku hiyo ya Jumatatu moja kwa Moja Mwandishi wa habari hizi aliingia Mtaani kusaka habari nyingike kali na kufanikiwa kupata stori ya vijana wengi kuchanganya Pombe Kali na Juice ya kuongeza nguvu mwilini ‘Energy’.

Uchunguzi huo uliofanywa na Mtandao huu umebaini wanaofanya hivyo wengi wao ni Vijana wadogo ambao ni madereva wa boda boda.

Ushushu huo pia umebaini baadhi ya wana wake wakiwalalamikia wapenzi wao kukosa nguvu za kiume.

Bint mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa kulinda heshima yake na ya mpenzi wake alikubali kuzungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake popote.

”Ni kweli vijana wengi siku hizi ni magoigoi hawana nguvu za kiume za kutosha, nilimuacha mpenzi wangu wa awali kwa sababu hizo nimekuja kwa huyu mwingine penzi lilipokuwa jipya alijitahidi kidogo lakini kadri siku zilivyoendea uwezo wake umezidi kupunguka”alisema dada huyo na kuendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

“Hatujaona kwa sasa ni wachumba ambao hatusihi pamoja yeye ndio kwanza anaanza maisha na umri wake bado mdogo baada ya kumaliza shule alipata Boda boda ya Mkataba ndio anaendelea nayo.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Daktari Clementi Lugaya anayefanya kazi hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Alipotakiwa kuelezea madhara ya kuchanganya Pombe kali na Energy alisema.

“Shekidele kwanza lazima ujua unywaji pombe kali mara kwa mara kuna madhara kiafya, sasa ukichanganya na hiyo Energy ndio mbaya zaidi unatengeneza kiwanda kingine cha pombe tumboni.
Siku hizi vijana wengi wanatatizo la nguvu za kiume kwa sababu ya unywaji wa pombe kali kupindukia, utashuhudia kijana wamiaka 25 mpaka 40 analalamika kukosa nguvu za kiume” alisema Dkt Lubaya na kuendelea kufunguka mazito.

“Kwa sasa baadhi ya vijana wenye changamoto hiyo wanachanganya kinywaji hicho cha Energy na Panaldo kutafuta nguvu hizo za kiume”

Mwandishi. Ni kweli kwa kufanya hivyo wanapata nguvu hizo?
Dkt Lubaya. Yes ukichanganya hivyo unazipata nguvu hizo vizuri kabisa ila ni kwa muda sasa kama una mke nyumbani huwezi kumchangania Energy na Panalod kila siku.

Mwandishi. Je na hilo la kuchanganya Energy na Panado ambalo kimsingi ndio nalisikia kwako linamadhara au halina?

Dkt Lubaya. Linamadhara pia na madhara yake watayaona baadae.
Mwandishi. Kama daktari sasa unawapa ushauri gani wanaume wenye changamoto hizo za nguvu za kiume?.

Dkt. Lubaya. Ushauri wangu waache au wapunguze kunywa pombe kali.

Pili wazingatia kufanya mazoezi mara kwa mara
Tatu waachane kula machipsi wale vyakula vya kujenga mwili kama vile Ugari wa Dona, Mboga za majani,Matunda, wanywe maji mengi .

Na Mwsho wapunguze msongo wa mawazo unapokuwa faragha, wakizingatia hayo viungo vyote vya mwili vitakuwa na nguvu za kutosha.

Mwandishi. Swali za mwisho uko hospital kuu ya Mkoa wa Morogoro. ile sindano ya kinga ya Tetenasi kuchoma gharama zake ni kiasi gani?

Dkt Lubaya. Hiyo sindano ya Tetenasi ni bure kwa mtu yoyote.
Mwandishi. Asanye kwa ushirikiano wako.
Dkt Asanye na wewe kwa kujari karibu tena.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...