Daktari
Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KAMA Kawaida Mtandao Pendwa wa Shekidele kila uchao unabuni story mpya na Moto Moto hasa zile a Kijamii zinazoibuka kwenye mitaa tunayoishi.
Kipengere hiki kitaruka kila siku za Jumatatu ambapo wiki nzima Mwandishi wa Mtandao huu atazunguka kitaa kusaka habari kubwa za kitaa hivyo nakusihi uwe jirani na Mtandao huu muda wote.
Wiki iliyopita Mwandishi wa Mtaa huu aliingia mtaani na kushuhudia baadhi ya Wazai wakiwakatisha zima vichanga vyao nje ya Muda kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kuendele kura usichana , majukumu ya kazi na Vifo. Kufuatia hali hiyo Mtandao huu ulizungumza na Mzazi Farha Abraham ambaye pia ni Mfundaji’Somo’ na Mtangazaji Maarufu wa Planet Redio ya Mkoani Morogoro akikitenda haki kipindi pendwa cha Mcharuko wa Pwani
“Nikosa kumkatisha mtoto ziwa unajua maziwa ya Mama yanavirutubisho kama ikitokea uko bize kikazi basi unapokwenda kazini kamua maziwa yako yahifadhi kwenye chombo kisafi baadae unayemuachia huyo mtoto atamnywesha”alisema Somo huyo kwa njia ya simu.
Ili kupata Ufafanuzi zaidi wa jambo hilo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Daktari Maarufu Mkoani Morogoro anayehudumu Hospital ya Ahmadiyyah inayomilikiwa na Watanzania wenye asili ya Asia’Wahindi’ Dkt Saddick Juma na Mahojiano yetu yalikuwa hivi.
Mwandishi. Habari za kazi Doktari, juzi nilifika hapa ofisini kwako nimekuta uko bize nikaomba ahadi ya kukutana nje ya ofisi nashukuru umekubari ombi langu umeniomba nije hapa Mji Mpya kwenye biashara yako binafsi.
Daktari. Ok asante sana kwa kunielewa na karibu sana.
Mwandishi, Asante, moja kwa moja niingie kwenye hoja yangu, hivi mtoto akizaliwa anahitaji kunyonya ziwa la Mama kwa muda gani.
Daktari. Sheria ni Miaka 2 kama Mama ameathirika na hili gonjwa letu yeye anamnyonyesha kwa mwaka 1.
Mwandishi. Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia baadhi ya wazazi kwasababu mbali mbali zikiwemo za kiuchumi wanawakatisha ziwa watoto zao ndani ya miezi 6 au mwaka, kisha anampa mbadara wa maziwa ya Mnyama Ng’ombe madhara yake ni yapi?
Daktari. Kufanya hivyo ni kosa kubwa unajua mwenyezi Mungu anaukuu wake Maziwa ya Mama ameyaweka Kinga ya magonjwa ikiwemo Almoni.
Hivyo kitendo cha kumkatisha ni kumuondolea kinga.
Mwandishi. Swali la Mwisho baada ya mzazi kujifungua anapaswa kuingia tena kwenye tendo la ndoa baada ya muda gari, ili asije kumbemenda Mtoto?
Daktari. Wiki 6 kwa maana ya siku 42 baada ya hapo anakuwa huru kufanya tendo hilo.
Mwandishi. Hee kama ni hivyo ndani ya hizo wiki 6 huyo mzazi si anaweza kubeba ujauzito mwingine na kitaaramu mzazi huyo anatakiw akujifungua mtoto mwingine baada ya muda gani?
Daktari. Swali Zuri ndio maana siku zote tunawasihi wajawazi kuhudhuria Clinic ambako huko watapewa semina ya kinga za kupata ujazito mwingine wakati unalea. Kisheria mtoto anapoacha kunyonya baada ya miaka 2 unaruhusiwa kubeba ujauzito mwingine, kwa sababu utakuwa umeshamaliza malezi.
No comments:
Post a Comment