Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, September 27, 2024

SABABU ZA UWANJA WA MANCHESTER UNITED KUJENGWA KWA TOFARI ZA KUCHOMA.












 


      Na Dunstan Shekidele Morogoro.

KUNA Maswali mengi kwa baadhi ya wadua wa Soka duniani wakihoji kwa nini timu tajiri dunia  Manchester United ya Uingereza kujenga uwanja wake wa Old Ttefford kwa tofari za kuchoma zinazotajwa kuwa na viwango vya chini tofauti za tofari za  Saruji  [Block Tofari].

 Maswali hayo yanajibiwa na uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya tofari hizo za kuchoma .

Mwandishi huyo alizunguka kwenye viwanda  vya kutengeneza tofari hizo  maeneo mbali mbali ya Mkoani Morogoro na kubaini yafuatayo.

Mosi. Tofari hizo hufyatuliwa kwa tope kisha kuanikwa jua kwa takribani wiki moja.

Baada ya kukauka wahusika huzipanga kwenye Tanuri na kuzichoma  Moto wakichomeka lundo la kuni kwenye njia maalumu zilizotengenezwa kwenye tanuli lenye uwezo wa  kubeba zaidi za Tofari elfu 30.

Zikishaiva hugeuka rangi kutoka nyeusi kuwa nyekundu hapo tayari kwa kuingia sokoni ambapo wanunua hutinga kwenye kiwanda husika na kununua tofari hizo.

Akijibu maswali  mmoja wawafanyakazi wa kiwanda cha Kingolwira  aliyejitambulisha kwa jina Moja ya Selemani alisema.

“Hii ni ajira kama ajira nyingine na vijana wengi ambao hatukufanikiwa kuendelea na Elimu tumekimbilia kwenye kazi hii ambayo tunaendesha familia zetu kwa kipato hichi.

Nikirejea kwenye maswali yako Tanuri moja hubeba Tofari zaidi ya elfu 30.

Tofari moja tunauza shilingi mia na kumi lakini wewe shekidele kwa sababu ni Mwandishi wetu Marufu hapa Morogoro tutakuondole hiyo 10 lipia mia  unahitaji ngari?

Mwandishi. Zinaingia tofari ngapi kwenye Lori?

Sele. Zinaingia tofari elfu 2.

Mwandishi. Ok na kutoka hapa Mpaka Mjini nauli ya Lori kiasi gari?

Sele.Elfu 50 ila kwa sababu wewe shekidele utalipilia elfu 40.

Chaajabu baada ya Mwandishi kulipia tofari hizo pamoja na nauli ya gari, wafanyakazi wote waliokuwa wakipakia tofari hizo walishuka kwenye gari na kubaki dereva tu, niliomuliza Sele nani ashusha tofari tutakapofika site? Alijibu.

“Shekidele hizi tofari ni chuma hili tipa litazibinua kama mchanga na hakuna hata tofari itakayovunjika, hizi tofari unajengea hata ghorofa kaandike kwenye magazeti watu wasizidharau hizi tofari ni chuma cha Mjerumani”alisema Sele na kuangua kicheko.

Kweli baada ya kufika Site Lori hilo lilibinua Tofari hizo na hakuna zilizovunjika kama zinavyoonekana pichani.

Kazi ya kujenga uzio ulinza kwa kutumia tofari hizo na nyumba kuonekana kama uwanja wa Old Trafford  unaomilikiwa na timu tajiri dunia ya Manichester United’Wazee wa Tofari za Kuchoma’.

Kwa uchunguzi huo sasa watu atapata majibu ni kwa nini Man U waliamua kujenga uwanja wao kwa tofari za kuchoma.

Ifahamike pia majengo mengi ya Misheni hasa yale ya kanisa Katolini yamejengwa kwa tofari za kuchoma na kuonekana wake unavutia kama huu wa uwanja wa Old Trafford.

Baada ya kuona Lori libaninua Tofari hizo kanisa la T.A.G limeingilia kati kisa nini endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

Tuesday, September 24, 2024

WAJINA


 

KUNA siku nilikutana na wajina wangu gari aina ya Datsun na kulikagua kiaina.
Kwa sasa magari ya kampuni hiyo ni adimu sana kuonekana kitaa unaweza kumaliza Mwaka usilione gari hilo.

Wednesday, September 18, 2024

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA












Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.
 
Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.
 
Miongoni mwa jumbe hizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU.
Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.

 

Monday, September 16, 2024

HATIMAYE MOTO UMEZIMWA MILIMA YA ULUGURU


 

Muda huu saa 5 usiku niko eneo la Bigwa chini ya Milima ya Uluguru hatimaye Moto umezimwa kwenye Milima hiyo kama picha iliyopigwa sasa hivi inavyoonyeshe hakuna hata chembe ya moto Wala Moshi.

 

Pongezi za thati kwa Maafande wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro kwa kazi kubwa walioifanya.

 

Zinazong'ara hapo chini ni taa za majengo yaliyopo chini ya Milima.hiyo.

 

Picha na Dunstan Shekidele Morogoro.

ZIMA MOTO WAKWEA MILIMA YA ULUGURU KUDHIBITI MOTO.

                              Hii ni jana majira ya saa 2 usiku

,Mwandishi wa Mtandao huu akiwa juu ya kilele cha Milima ya Uluguru
 

Leo muda huu wa saa 8 mchana hali iko hivi

    Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MAAFANDE wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, wamepanda juu ya kilele cha Milima ya Uluguru kuzima Moto mkubwa uliokuwa ukisambaa kwa kasi kwenye Milima hiyo inayotajwa kuzalisha vyanzo vya maji safi yanayosambaa mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.

Muda huu wa mchana Mwandishi wa Mtandao huu anashuhudia moto huo ukipungua kasi baada ya Jeshi la Zima Moto kuendelea na kazi ya kuudhibiti, kama inavyoonekana pichani sehemu ndogo ya Mlima ikivuka Moshi.

Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ndiye wa kwanza kuripoti tukio hilo  jana usiku kwenye mtandao huu kisha kusambaza picha hizo za moto kwenye Magroup mbali mbali likiwemo Group la Whatsap la Jeshi la Zima Moto Mkoa wa Morogoro.

Baada ya kuona picha hiyo inayooshesha Mlima huo ukiteketea kwa Moto, mmoja wa makamanda wa Jeshi hilo aliyefahamika kwa jina la Esther alimshukuru Mwandishi wa Mtandao huu kwa taarifa hiyo aliyoituma kwenye Group hilo akiwa Mwandishi wa kwanza kuripoti tukio hilo.

Hata hivyo kupitia Group hilo  Afande Esther alisema baada ya Moto huo kuibuka juzi  Vijana wake walipanda juu ya Mlima kuudhibiti Moto huo.

Ili ufike kwa haraka juu ya kilele cha Mlima huo itakuradhimu kutumia usafiri wa pikipiki kama ambavyo Mwandishi wa Mtandao huu siku za nyuma alipanda juu ya kilele cha Mlima huo akitumia boda boda yake.

Taarifa zinadai Milima ya Uluguru inazalisha Vyanzo vya maji vinavyosambaa katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.

Hali hiyo ya uchoma  Moto Mlima huo ni uharibifu wa mazingira unaweza kuviua vyanzo hivyo vya Maji na kupelekelea upungufu wa Maji kwenye Mikoa hiyo.

Sunday, September 15, 2024

BREKING NEWS, MILIMA WA ULUGURU UNATEKETEA KWA MOTO USIKU HUU


 Milima ya Uluguru inateketea kwa Moto usiku huu

MACHO YA BWANA YAKO KILA MAHALI.


 


                            MITHALI 15.2-7.

“Jawabu la upole hugeuza hasira, bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.

Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa Vizuri, bali vinywa vya wapumbavu humwaga Upumbavu.

Macho ya Bwana yako kila mahali.yakimchunguza mbaya na mwema.

Ulimi safi ni Mti wa Uzima, bali ukorofi wa Ulimi uvunja Moyo.

Mpumbavu hudharau kurudiwa  na babaye, bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara.

Katika nyumba ya mwenye haki mnahakiba nyingi,bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu” Huu ndio ujumbe wetu wa Jumapili ya leo septemba 15. Bwana naatufanyie wepesi kuyafuata mafundisho yake yenye Mwanga katika Maisha yetu.

Panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu tukutane Jumapili ijayo kwa ujumbe mwingine wa neno la MUNGU.

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...