,Mwandishi wa Mtandao huu akiwa juu ya kilele cha Milima ya Uluguru
Leo muda huu wa saa 8 mchana hali iko hivi
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MAAFANDE wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, wamepanda juu ya kilele cha Milima ya Uluguru kuzima Moto mkubwa uliokuwa ukisambaa kwa kasi kwenye Milima hiyo inayotajwa kuzalisha vyanzo vya maji safi yanayosambaa mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.
Muda huu wa mchana Mwandishi wa Mtandao huu anashuhudia moto huo ukipungua kasi baada ya Jeshi la Zima Moto kuendelea na kazi ya kuudhibiti, kama inavyoonekana pichani sehemu ndogo ya Mlima ikivuka Moshi.
Mwandishi wa Mtandao huu ambaye ndiye wa kwanza kuripoti tukio hilo jana usiku kwenye mtandao huu kisha kusambaza picha hizo za moto kwenye Magroup mbali mbali likiwemo Group la Whatsap la Jeshi la Zima Moto Mkoa wa Morogoro.
Baada ya kuona picha hiyo inayooshesha Mlima huo ukiteketea kwa Moto, mmoja wa makamanda wa Jeshi hilo aliyefahamika kwa jina la Esther alimshukuru Mwandishi wa Mtandao huu kwa taarifa hiyo aliyoituma kwenye Group hilo akiwa Mwandishi wa kwanza kuripoti tukio hilo.
Hata hivyo kupitia Group hilo Afande Esther alisema baada ya Moto huo kuibuka juzi Vijana wake walipanda juu ya Mlima kuudhibiti Moto huo.
Ili ufike kwa haraka juu ya kilele cha Mlima huo itakuradhimu kutumia usafiri wa pikipiki kama ambavyo Mwandishi wa Mtandao huu siku za nyuma alipanda juu ya kilele cha Mlima huo akitumia boda boda yake.
Taarifa zinadai Milima ya Uluguru inazalisha Vyanzo vya maji vinavyosambaa katika Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es salaam.
Hali hiyo ya uchoma Moto Mlima huo ni uharibifu wa mazingira unaweza kuviua vyanzo hivyo vya Maji na kupelekelea upungufu wa Maji kwenye Mikoa hiyo.
No comments:
Post a Comment