Na Dunstan Shekidele Morogoro.
KUNA Maswali mengi kwa baadhi ya wadua wa Soka duniani wakihoji kwa nini timu tajiri dunia Manchester United ya Uingereza kujenga uwanja wake wa Old Ttefford kwa tofari za kuchoma zinazotajwa kuwa na viwango vya chini tofauti za tofari za Saruji [Block Tofari].
Maswali hayo yanajibiwa na uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu juu ya tofari hizo za kuchoma .
Mwandishi huyo alizunguka kwenye viwanda vya kutengeneza tofari hizo maeneo mbali mbali ya Mkoani Morogoro na kubaini yafuatayo.
Mosi. Tofari hizo hufyatuliwa kwa tope kisha kuanikwa jua kwa takribani wiki moja.
Baada ya kukauka wahusika huzipanga kwenye Tanuri na kuzichoma Moto wakichomeka lundo la kuni kwenye njia maalumu zilizotengenezwa kwenye tanuli lenye uwezo wa kubeba zaidi za Tofari elfu 30.
Zikishaiva hugeuka rangi kutoka nyeusi kuwa nyekundu hapo tayari kwa kuingia sokoni ambapo wanunua hutinga kwenye kiwanda husika na kununua tofari hizo.
Akijibu maswali mmoja wawafanyakazi wa kiwanda cha Kingolwira aliyejitambulisha kwa jina Moja ya Selemani alisema.
“Hii ni ajira kama ajira nyingine na vijana wengi ambao hatukufanikiwa kuendelea na Elimu tumekimbilia kwenye kazi hii ambayo tunaendesha familia zetu kwa kipato hichi.
Nikirejea kwenye maswali yako Tanuri moja hubeba Tofari zaidi ya elfu 30.
Tofari moja tunauza shilingi mia na kumi lakini wewe shekidele kwa sababu ni Mwandishi wetu Marufu hapa Morogoro tutakuondole hiyo 10 lipia mia unahitaji ngari?
Mwandishi. Zinaingia tofari ngapi kwenye Lori?
Sele. Zinaingia tofari elfu 2.
Mwandishi. Ok na kutoka hapa Mpaka Mjini nauli ya Lori kiasi gari?
Sele.Elfu 50 ila kwa sababu wewe shekidele utalipilia elfu 40.
Chaajabu baada ya Mwandishi kulipia tofari hizo pamoja na nauli ya gari, wafanyakazi wote waliokuwa wakipakia tofari hizo walishuka kwenye gari na kubaki dereva tu, niliomuliza Sele nani ashusha tofari tutakapofika site? Alijibu.
“Shekidele hizi tofari ni chuma hili tipa litazibinua kama mchanga na hakuna hata tofari itakayovunjika, hizi tofari unajengea hata ghorofa kaandike kwenye magazeti watu wasizidharau hizi tofari ni chuma cha Mjerumani”alisema Sele na kuangua kicheko.
Kweli baada ya kufika Site Lori hilo lilibinua Tofari hizo na hakuna zilizovunjika kama zinavyoonekana pichani.
Kazi ya kujenga uzio ulinza kwa kutumia tofari hizo na nyumba kuonekana kama uwanja wa Old Trafford unaomilikiwa na timu tajiri dunia ya Manichester United’Wazee wa Tofari za Kuchoma’.
Kwa uchunguzi huo sasa watu atapata majibu ni kwa nini Man U waliamua kujenga uwanja wao kwa tofari za kuchoma.
Ifahamike pia majengo mengi ya Misheni hasa yale ya kanisa Katolini yamejengwa kwa tofari za kuchoma na kuonekana wake unavutia kama huu wa uwanja wa Old Trafford.
Baada ya kuona Lori libaninua Tofari hizo kanisa la T.A.G limeingilia kati kisa nini endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment