Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, May 9, 2024

YARIYOJIRI KUMBI WA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. KOCHA WA DUNIA ‘MWIJUMA’ALIZA WATU UKUMBINI NA WIMBO WAKE WA MGUMBA.

Muumini Mwijua Kocha wa dunia  aqkiimba wimbo wa Mgumba

Prezeda Joshua Malekela akigonga gitaa la soro kunogesha wimbo huo wa mgumba


 


               Na Mlala Nje Dustana Shekidele,Morogoro.
 
MWANAMUZIKI Mkongwe nchini wa Muziki wa Dansi, Muumini Mwijuma’Kocha wa Dunia’Mwishoni mwa wiki ameliza baadhi ya mashabiki waliofurika ukumbi lpo lpo wa mkoani hapa,alipoimba wimbo wake wa Mgumba. 
 
Kwa takribani miezi 4 hivi Mlala Nje alisitisha kipengele cha kuzunguka kumbi za starehe usiku Mnene, kusaka matukio akipisha miezi mitakatifu ya Kwarezima na Ramadhani.
 
Hekima na hofu ya Mungu kwa pamoja vilimuongoza Mlala Nje kusitisha kurusha picha za kumbi za starehe miezi hiyo ambayo Wakristo na Waislamu kwa pamoja walikuwa kwenye lbada za toba ya funga. 
 
Wiki End iliyopita Kipengele hicho kimereje hewa kwa Mlala Nje kuzunguka Kumbi za Starehe.
 
6 usiku Mlala Nje anatinga Ukumbi wa lpo lpo Mazimbu na kushuhudia Muumini Mwijuma akifanya ‘Korabo’akishirikiana kuimba na Band ya Maisha Mapya ‘Full Vipaji’ ya Mkoani Morogoro.
 
Mara kwa mara Mlala Nje alimshuhudia Kocha huyo wa dunia mwenye maskani yake Mikoa ya Dar es salaam na Pwani akifunga safari kutoka huko kuja Mji Kasoro bahari kufanya Korabo na Band hiyo ya Maisha Mapya’Kipenzi cha Wana Moropgoro’.
 
Kwenye Koroba hiyo Mwijuma’Mzaramu wa Bagamoyo’ aliimba wimbo wake wa Mgumba ‘usiochuja kama tui la nazi’ kwa hisia kari akishirikiana na Mwanadada wa band ya Maisha Mapya,lngizo jipya aliyejiunga na Band hiyo hivi karibuni akitokea Band ya Waluguru Og, 
 
Habari za Mwanadada huyo kujiunga na Band hiyo zitaruka hewani wiki ijayo kwenye kipengele hiki cha Mlala Nje baada ya kukamilisha habari hiyo.
 
Muumini na Mrembo huyo waliimba kwa hisia kari Wimbo wa Mgumba huku wakikumbatiana kwa kushikana mikono kama walivyonaswa na na kamera za Mlala Nje.
 
Wakati wanamuziki hao wakiendele kuimba wimbo huo huku kwa mashabiki vilio vilitawara, Mlala Nje alimshuhudia dada mmoja aliyeketi mbele ya meza yake akijifuta machozi mara kwa mara akitumia mtandio wake ambao mpaka wimbo huo unakamilika 
 
Mlala Nje alishuhudia Mtandio wa dada huyo ukirowa machozi chapa chapa kama amenyeshewa na Mvua uliyokwenda sambamba na kingunga cha Hidaya. 
 
Kwa maneno mengi ya hudhuni ya wimbo huo wa Mgumbe yaliyochangizwa na hisia kali za waimbaji hao hali hiyo ilizidisha machungu kwa dada huyo na kujikuta akishindwa kuzimalizia bia alizokuwa akinywa.
 
Kuna hivyo wenzie aliyeketi nao waliweka kando mastori yao na kubeba jukumu la kumbembereza mwenzao huyo aliyeangua kilio hadharani kama mtu aliyefiwa.
 
Baadae Mlala Nje aliwashuhudia hao wanaombembeleza nao wakishindwa kuyazuia machozi yao kutiririka kwenye mboni za macho yao hivyo meza hiyo iliyokuwa eneo lenye mwanga hafifu ilijaa vidimbwi vya machozi ya warembo hao.
 
Baada ya Muumini kushuka Jukwaani dada huyo alitoka nje ya Ukumbi na kudandia boda boda kuondoka zake. 
 
Baada ya dada huyo kuondoka Mlala nje alizungumza na wenzake ambao walisema,Mwenzao huyo katika maisha yake hajajaliwa kupata mtoto licha ya kufanya juhuzi kubwa bila mafanikio.
 
“{Wimbo huu wa Mgumba ni kama umetonesha kidonda kwenye moyo wake na kujikuta akimwaga machozi kama ulivyomshuhudia bia zake hizi hapa kashindwa kuzimalizia katuaga kasema anakwenda kulala’’Walisema mashosti zake hao ambao baadae waliendelea kula bata wakipombeka na kusahau yaliyopita.
 
Hadi Mlala nje anaondoka ukumbini hapo majira ya saa 8 usiku Warembo hao walikuwa wakiendeleakukata maji kama Mamba ziwani, nahisi walivunja kikoba siku hiyo wakaamua kujitoa ‘Out’ na kujipongeza. 
 
Pichani Kocha wa dunia [kulia] akiimba wimbo huo wa Mgumba kwa hisia kari akiwa sambamba na mwanadada Usajiri jipya wa ‘Chama la Wana’ Band ya Maisha Mpya.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...