Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, May 8, 2024

ROBO FAINALI MICHUANO YA RAMADHAN CUP ‘DERBY’ YA KIHONDA MAGHOROFANI, MWAKINGWE AMUADHIBU MAUYA.

Diwani wa kata ya Kihonda Maghorofani Mhe Eng Hamisa Ndwata akizungumza na wachezaji wa timu za Kihonda Maghorofani na JL- Academy .
Mhe Diwani akiwa na kikosi cha JL Academy pambeni yake ni mratibu mkuu wa michuano hiyo Kafale Maharagande
....Eng Ndwata akiwa na kikosi cha Kihonda Maghorofani








 Ulimboka Mwakingwe. Kushoro mwenye kapeso akiwa jukwaani akifuatia lia mchezo huo akiwa sambamba na Meneja wa timu ya Moro Kids Mussa Miraji,


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya J.L- Academy inayomilikiwa na mchezaji nyota wa zamani wa SImba Ulimboka Mwakingwe’Uli’ imewadhibu mahasimu wao wakubwa timu ya Kihonda Mahofofani ambayo ni timu ya kitaa anayoitumikia mchezaji  wa Yanga Zawadi’Gift’ Mauya.

Katika gemu hiyo ya robo fainali ya michuano ya Ramadhani Cup iliyoandaliwa na chama cha soka Wilaya ya Morogoro, imepigwa jana uwanja wa Saba saba na JL -Academy kuwanyuka Maghorofani  bao 2-0.

Gemu hiyo ya ‘Derby’ya ilijaa upinzani mkali kwa muda wote wa dakika 90 kufuatia timu zote mbili kutoka mtaa mmoja ndani ya kata ya Kihonda Maghorofani inayoongozwa na Mhe Diwani  Eng Hamis Ndwata, aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo uliowakutanisha timu mbili kutoka kwenye kata yake.

Mara baada ya kukagua timu hizo Mhandisi Ndwata alitoa nasaha fupi” katika hatua za awari za michuano hii kila siku nilikuwa na kuja hapa uwanjani na kuketi kwenye benchi la Kihonda Maghorofani na JL Academy kwa lengo la kuwasapoti na shukuru hamasa hiyo imesaidia kufika hatua hii ya robo fainali ambapo leo tunakutana wenyewe kwa wenyewe.

Leo sitakuwa pande wowote zote ni timu zangu sita kaa kwenye benchi la timu yoyote nikaketi pale meza kuu nikiunga mkono timu zote ingawa nafahmu lazima mmoja afungwe”alisema Mhe Diwani Ndwata. Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia Ulimboka akiwa jukwaani akiwafuatilia vijana wake, lkumbukwe ‘Uli’ amefungiwa na TFF kujihusisha michezo kufuatia kutiwa hatiani kwa kosa la kuwarubuni baadhi ya wachezaji Fountain Gete ya Dodoma kwenye mchezo wa Ligi daraja la kwanza dhidi ya Tabora United.

Ulimboka na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Tabora na mmiliki wa timu ya Tabora United Yusuf Kitumbo kwa pamoja wamefungiwa kwa kile kilichodaiwa sauti zao kudukuliwa kwenye simu wakiwarubuni kwa fedha wachezaji wa Fountain Gat wacheze chini ya kiwango dhidi ya Kitayose sasa Tabora United.

Wakati hayo yanatoke ulimboka[pichani kushoto mwenye kofia alikuwa kocha msaidizi wa timu ya Kagera Sugar, baada ya kumuona Mpiga Picha wa Mtandao huu anamtwanga mapiga akiwa jukwaani na Meneja wa Moro Kids Mussa Miraj[kulia].

 Ulimboka kapasa sauti akisema” Shekidele siunajua nimefungiwa usije kuandika kwamba niko kwenye benchi na Viajana wangu katika kuheshimu adhabu hiyo ndio maana umeniona jimejitena niko huku mbali jukwaani nikifuatioa mchezo kama mashibi mwingine”alijihamia Uli.

 lfahamike kata ya Kihonda Maghorofani ndio kata pekee Mkoani Morogoro ambayo mastaa wengi Tanzania wanamijengo ama kuishi kwenye kata hiyo.

Baadhi ya mastaa hao  ni pamoja na Juma Kaseja. Mecky Mexime, Ulimboka Mwakingwe. Mzamiru Yassin, Zawadi Mauya. na Jumanne ‘Shengo’ Tondoro huyu alikuwa mchezaji wa Moro United kabla ya kutimkia Simba.

 Mastaa wengine  ni wanasiasa  katibu mwenezi wa CCM Taifa Mhe Amos Makalla, hayati Mchungaji Mama Getruda Lwekatale na Mwanamuziki wa muziki wa kizazi Kipya Stamina.pamoja na mmiliki wa shule za Fouantain Gat  Bw Jafet Makao ambapo mara kwa mara timu za Fountain Get huweka kambi eneo hilo la Kihonda Maghorofani.

                     

 


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...