Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, May 10, 2024

PICHA KALI YA WIKI.




 

                      

                             CAPTION.

Wiki iliyopita Waziri wa Utamadun, Sanaa na  Michezo, Mhe Dkt Damas Ndumbaro,alifanya ziara ya kikao mkoani Morogoro.

Kwenye ziara hiyo Mhe Waziri alitoa maagizo kwa halmashauri zote nchini kutenda na kulinda viwanja vya michezo  mashuleni na Mitaani.

Juzi Mpiga Picha wa Mtandao huu alikatiza shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege na kushuhudia kiwanja cha michezo cha shule hiyo kikegeuzwa Packing ya Malori.

Kufuatia kiwanja chao kuvamia na Malori hayo, watoto hao wameijiongeza na kuweka magori ya miti jirani na madarasa yao na kucheza Mpira wakisaka vipaji vyao.

Walipohojiwa   watoto hao walisema “Father kama unavyoona kule kwenye kiwanja chetu magari yamepack tumeamua kucheza hapa pembeni,hii ni Darby  ya darasa la Tatu na darasa la Nne”walisema madent hao.

 Ifahamike Jirani na shule hiyo eneo la Faya kuna Soko la Mbao hivyo maLori mengi yanajazana eneo hilo kusubiri wateja wa kusafirisha mizigo hiyo ya mbao.

 Picha na Dustan Shekidele,Morogoro.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...