Mafuta ya Mtume Mwamposa yakiwa kwenye kichupa hicho kidogo chenye mfuniko mweupe.
Mama huyu anayedaiwa kuwanga akiendelea kugaragara chini baada ya kuondolewa katikati ya barabara
HABARI KALI YA KITAA.
MWANAMKE ANASWA USIKU MNENE MAKABURI YA WAHINDI AKIDAIWA KUWANGA.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Kama kawaida kipengele pendwa cha habari kali ya kitaa kinaendele leo ljumaa.kabla ya kuendele nitoe mrejesho wa habari iliyopita.
Niliahidi kuendelea kumtafuta yule bibi aliyedaiwa kumfanyia vitu vya ajabu marehemu mumewake,juhuzi hizo zimegonga mwamba kila nikimpigia simu kupitia no yake ya tigo mwisho 10 haipatikani.
Majirani wanadai ameludi kijijini kwao Mgeta na wengine wanadai amekwenda Dar kwa watoto zake.
Majirani hao wamesema huenda huko kamua kukata mawasiliano kwa kubadili namba ya simu.
TUENDELEA NA STORI MPYA
MWANAMKE Mmoja ambaye hajafahamika mara moja anayekadiliwa kuwa na Umri kati ya Miaka 35 mpaka 40, anadaiwa kukutwa usiku Mnene eneo la Makaburi ya Watanzania wenye asiri ya lndia ‘Wahindi’yaliyopo ‘ushuani’ eneo wanaloishi Mabosi na matajiri Forest Mkoani hapa akiwa uchi wa mnyama akidaiwa kufanya vitendo vya kishirikina’kuwanga.
Akizungumza na Mtandao huu Shuhuda wa tukio hilo Nickson Mkilanya’Nick Fado’ alisema.
”Juzi majira ya saa 6 usiku nikiwa ndani ya gari langu nilipofika eneo la Makaburi ya Wahindi nilikuta foreni kubwa ya magari na Pikipiki niliposogea jirani nimeshuhudia huyu Mama akiwa uchi wa Mnyama akisota kwenye lami jirani na geti la makaburi ya wahindi ”alisema Mkilanya na kuongeza
“Inaonekana amenasa kwenye makaburi hayo ya ndugu zetu Wahindi, kwa sababu alikuwa katikatia ya barabara madereva wameogopa kumgonga wameishi kummulika na taa baada ya foreni kuwa kuwa kubwa mtu mmoja kajitolea kumpa nguo na kumuondoa eneo la barabara kuruhusu gari zipite.
Alivyovaa nguo nikampiga hizi picha za Video na Mnato ambazo nimekurushia kwenye Whatsapp yako, nasikia alfajiri alitoweka kimiujiza”alimalizia kusema Mkilanya ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro.
Baada ya kupewa ‘Tip’ hiyo Mwandishi wa habari hizi aliingia mzigo akatinga eneo la tukio na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa na haya ya kusema.
“ Taarifa hizo hatuna si unajua huku Forest ni uzunguni nyumba nyingi zina mageti muda wote mchana na usiku watu wako ndani ya mageti yao yanayotokea huko nje hatuyajui”walisema wananchi hao.
Mtandao huu alimtafuta Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo wa Old Dar es salaam Mzee Asanali.
”Binafsi sina taarifa za tukio hilo ninachoweza kusema ni kwamba taarifa hizi nitazipeleka BMK pia nitamfahamisha polisi Kata aimalishe ulizi kwenye makaburi yale ambayo tumeyazungushia uzio yakjo ndani ya geti”alimalizia kusema Mwenyekiti huyo ambaye ni pia ni Muhindi.
Chaajabu baada ya habari hii kukamilika kwa maana ya kuzungunza na mashuhuda pamoja na Uongozi wa Serikali ya Mtaa Mwandishi alipofungua picha za Mama huyo Whatsapp hakuziona.
Hivyo jana mchana imemradhimu kumpigia Mkilanya na kumjuza taarifa hizo, ‘Big Bos’ huyo wa Waandishi wa habari mkoa aliangua kicheko kisha akatuma tena picha hizo za Mnato na Video, muda huu kabla ya kuzifungua Mwanahabari huyo aliamua kujipaka mafuta ya Mtume Mwamposa mwili mzima na kuzifungua picha hizo safari hii zilifunguka fasta.
Clips Video inayomuonyesha Mama huyo akisota barabara nimeshindwa kuirusha kwa kuzingatia maadili kwa sababu alikuwa akifanya hivyo akiwa uchi wa mnyama.
lfahamike Mtaa wa Old Dar unaanzia eneo la daraja la Shan sinema Kitope Road kando kando ya barabara ya zamani ya Dar es salaam,ndani ya Mtaa huo kuna kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro, Uwanja wa Jamhuri, Hospital ya Rufaa ya Mkoa, Chuo cha VETA, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Ofisi za Posta mkoa, Hazina Mkoa C.A.G Mkoa, NSSF Mkoa. Madini Mkoa, Maktaba ya Mkoa Msikiti Mkuu wa Wahindi ‘Jamatini’na Shule ya Sekondari ya Morogoro.
No comments:
Post a Comment