Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, March 2, 2025

MCHEZAJI YANGA AONGOZA MAMIA YA WANANCHI MORO KUMUAGA MSWAKI.

Mwili wa Mpendwa wetu Victor Mswaki ikiwasii nyumbani kwa Bigwa
Groly akiangua kilio baada ya kushuhudia jeneza lililobeba mwili wa kaka yake likiwasi nyumbani kwa Bigwa, anaye msaidia ni Reuben Ngome
Mshambuiaji hatari wa Yanga Princess Fau Magori kulia akiwa na refa wa ligi Kuu Raphae Ikambi



Mshambuiiaji wa Yanga preincess Fau Magori akimuaga Mswaki
Kiongozi wa saba saba United Shuu mwenye nguo nyekundu akimuaga Mswaki
                   Mama Sengo naye akimuaga Mswaki
Mtoto wa marehemu akisindikizwa na bibi yake mzaa Mama kumuaaga mpendwa baba yake
lna uma sana mtoto wa marehemi awaki na picha ya hayati baba yake


Baadhi ya wachezaji waicheza na hayati mswaki wakiwa Bigwa  Msaiani

        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MCHEZAJI nyota wa Yanga Princess Fausta Alfrerd Maarufu [Fau Magoli] amewaongoza wananchi wa Mkoa wa Morogoro kumuaga Mchezaji Maarufu Mkani hapa Victor Mswaki Reuben Ngome

Mswaki ambaye enzi za uhai wake aliwahi kuzitumikia timu za daraja la kwanza za Mkoani Morogoro Burkina Faso na Mawenzi Market   Sambamba na timu mbali mbali za Ndondo Cup amefariki dunia Februar 26 Mwaka huu.

Baada ya kufariki wadau wa Soka mkoa wa Morogoro walijazana chumba za kuhifadhia maiti[Mochwari]kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanasoka huyo,zoezi hilo lilipokamilika mwili ulielekea nyumbani kwao Bigwa Mtaa wa kisiwa huko ilifanyika ibada iliyoongozwa na mchungaji Elibariki Makundi wa kanisa la Calvary Assembuliess Of God.

Baada ya ibada hiyo kutamatika siku hiyo hiyo ya ljumaa mwili  ulisafirishwa kwenda Tanga Wilaya ya Lushoto Kijiji cha Sonni Kisiwani ambapo jana Jumamosi alipunzishwa kwenye nyumba yake ya Milele.

    RAFIKI WA MSWAKI AFUNGUKA MAZITO.

Tukiwa Mochwari Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuzungumza na Rariki mkubwa wa Mswaki ambaye alikuwa na haya ya kusema.

“ Shekidele inauma sana aishee,Jumapili mimi na Mswaki tuliangalia gemu ya Yanga na Mashujaa pale Mawenzi nyumbani kwa Refa Raphael Ikambi  Maarufu ‘Rapha Webb’.

Baada ya gemu tukaniambia anakwenda  nyumbani wake Kihonda Azimo, gemu ya Simba  na Azam sijamuona  nikampigia simu akaniambia tumbo linamsumbua huyo Bingwa kwa Mama yake  nikamuambia kesho nakuja kukuona, chaajabu Jana saa 5 asubuhi najianda kwenda kumuona  napokea taarifa kwamba  amefariki” aisema Patrick Edward Maarufu Paty Edo ambaye yeye na  Mswaki waiitumikia timu ya Burkinafaso.

Kwa upande wake Msemaji wa famiia Reuben Ngome ambaye ni Mjomba wa Marehemu alipotakiwa kutoa historia fupi ya marehemu alisema

” Victor ni Mtoto wa marehemu Dada yangu  alipomaliza shule nyumbani Sonni mimi na shemeji yangu John Bosco tulimwita na kumfundisha kazi pale ofisini  kunatengeneza Radio, TV Simu na Camera.

Kila siku jioni aliomba ruhusa ya kwenda  mazoezi baadae tunamsikia kwenye maredio akizichezea timu kubwa za daraja la kwanza.

 Marehemu ameacha na mtoto mmoja wa kiume anaitwa Kendi amezaa na dada mmoja Refa wa mpira wa Miguuu.

kuhusu kifo chake Juzi alilalamika  Tumbo linamuuma kama unavyojua Shekidele ofisi yetu  ipo  jirani na hospital ya Saba saba akaenda hapo akapatiwa dawa.

 Jioni tulivyofunga ofisi mimi nikaenda Kwangu Lugala yeye nikamwambia kwa sababu anaumwa asiende kulala peke yake nyumbani kwake Azimo,  akalale Bigwa kwa Shangazi wake”alisema Reuben na kungeza

Siku iiyofuata majira ya saa 4 asubuhi Mpwa wangu amefariki dunia inauma sana, kuhusu ratiba ya mazishi watu wa Mjini wataaga hapa Mochwari baadae mwili utaelekea Bigwa kwa dada yangu Agnes Ngome ‘Mrs Bosco’ pale itafanyika lbada itakapoisha tutasafiri kwenye kijijini kwetu Sonni Kisiwani kuzika”alimalizia kusema

 Naye Mwenyekiti wa Serikai ya Mtaa wa Bigwa Kisiwani Nicholaus  Mpili kwenye salamu zake za rambi rambi alisema kama mtaa wamepoteza kipaji kikubwa cha soka.

” Kila Mwaka kwenye Kata yetu ya Kilakaia yenye Mitaa 15 tunacheza Ligi ya Ndond Cup inashirikisha timu kutoka mitaa hiyo,Mwaka Jana Mtaa wetu  tulikuwa mabigwa tukanyakua zawadi ya Milion Moja Mswaki alifunga magori mengi yaiyotupa ubingwa”aisema Mwenyekiti huyo,

 

No comments:

Post a Comment

UJUMBE WA NANE LA MUNGU USALAMA WA WATU WAMUNGU.

Mwandishi wa Mtandao huu akiwa kwenye msitu Mnene Matombo Wilaya ya Morogoro Vijiji ........Mwandishi huyo akiwa Juu ya Milima ya Mgeta wila...