Na Dustan Shekidele,Morogoro.
KWA sasa kuna baadhi ya vituo vya Radio nchini vipo kwenye kampeni kabambe ya mwanamke, kila kituo kina Srogan yake, wengine wanaita Marikia wa Nguvu na wengine Mwanamke wa shoka.
Kwangu mimi Dr.Rehema Kilangwa nitamwita mwanamke mfungua njia ya ellimu kwa mabinti wa Kitanzania.
lfahamike Binti Kilangwa huyo amesoma na kufanikiwa kumaliza madarasa yote nikimaanisha kwamba ana Master’s au PhD.
Kama sijakosea katika elimu PhD ndio mwisho wa masoma ya darasani ingawa wahenga wanasema Elimu haina Mwisho.
Kirefu cha PhD ni ‘Doctor Of Philosophy’ndio maana kwa mtu yoyote mwenye PhD anaitwa Doctor, ifahamike Kwamba huyo sio Doctor wa hospital ni Doctor wa Elimu.
Dr Rehema Kilangwa mwenye umri mdogo ametunukiwa PhD yake katika Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro’Muslim University Of Morogoro ‘MUM’.
Kama hiyo haitoshi Dr Rehema baada ya kutunukiwa PhD hiyo,kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu hicho kilichopo maeneo ya Msamvu kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
lkumbukwe pia Chuo Kikuu cha Kiislamu kina toa Masomo kwa waandishi wa habari ambapo pia Chuo hicho kinamiliki kituo cha Radio ‘MUM FM.’
Hivyo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro, Chuo kikuu hicho kilimteua Dr Rehema kukiwakilisha kwenye mkutano huo.
Dr Rehama alitumia muda mwingine kuwahamasisha Waandishi hao kujiendeleza kielimu huku akijitolea mfano yeye alivyopambana kupata PhD hiyo huku akiwa angali binti mdogo.
Hata hivyo kwenye kundi hilo la Waandishi wa habari kuna baadhi wanamiliki PhD hiyo akiwemo Mtangazaji Amina Said.
No comments:
Post a Comment