Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, April 30, 2024

MAONI YANGU MWENENDO MTIBWA SUGAR.



 

 

Baada ya jana Mtibwa Sugar kuokea kichao cha bao 2 kwa 1 dhidi ya JKT Tanzania mchezo ambao Mtibwa walikuwa na uwezo wa kuondoka hata na alama moja lakini kwa mshangao dakika ya 9o nikiwa kwenye Luninga naifuatilia timu yetu ya Morogoro.

Wana Morogoro  tumeumia  sana tukishuhudia Mtibwa ikufungwa  bao la 2 dakika ya 9o huku chanzo cha bao hilo ikiwa ni makosa ya mlinda mlango aliyetoa boko kwa kichuya na kuacha gori wazi.

 Kichuya baada ya kuona lango liko wazi kafumua shuti lililounganishwa wavuni na Six Sabilo.

Binafsi kuguza Mgonjwa siwezi, kwenye ukweli nasema ukweli  unaona kabisa Mgonjwa kazidiwa hata macho habwenzi, uji unamshinda kunywa,  kuhema kwake kama maji yanayotokota jikoni.

Wewe unayemuuguza nafsi yako inakushuhudia kabisa kwamba Mgonjwa wako  anakaribia kukata roho, unamtia moyo kwa kumwambia maneno ya Tumaini kwamba.

Mgonjwa wangu kuugua sio kufa, kweli hayo ni maneno ya faraja kwa mgonjwa   lakini hayatamsaidi kwenye safari yake ya kuelekea kwa Mungu.

kwangu mimi nikiona hivyo na mwambia ukweli, kwamba kila nafsi itaonja umauti na hakuna atakayeishi Milele  chini ya jua.

Hata mimi ninayekuugua muda wangu utafika nitaiacha hii duniani na kurejea kwa muumba wangu.

Hivyo ushauri wangu kwako mgonjwa wangu kwa hali ilivyo, tumia muda huu kutubu dhambi zako kwa mwenyezi Mungu, ili wakati wowote akikuita  maombi hayo yenye  toba. Yakusaidie mbele ya safari

            TIMU YA MTIBWA SUGAR.

Kwa mtibwa Sugar yenye Maskani yake katikati ya Mashamba ya Miwa eneo la Manungu Kata ya Mtibwa, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Kwa sasa taa ya Oil inawaka kwenye Dash Bord la gari lao, muda wowote gari lina Nock na kuzimika.

Kama ni boda boda Mtibwa wamevuta juu Chock  wanatembelea mafuta  ya Lizevu kwenye Kabreter ambayo hayajai hata kwenye kile kikombe cha kahawa muda wowote boda linazima kwa kukosa wese .

Mtibwa kwa msimu huu  imebadili makocha zaidi ya watatu,  walinda mlango zaidi ya 3,Kama hiyo haitoshi Mtibwa  msimu huu katika kuhangaika kujinusuru na janga la kushuka daraja kwenye usajiri wa dirisha dogo wamesajiri  wachezaji  zaidi ya 8,

Juhudi zote hizo hazikuza matunda bado timu inafungwa huku wakiukaribia mlango wa kushuka daraja wakikusanya alama  17 akiburuza mkia kwenye ligi hiyo yenye timu 16 huku wakibakiwa na michezo 7.

Kati ya michezo hiyo 7 kuna Simba watakao chezo nao keshokutwa Mei 3, bado na Yanga. Bado na Azam, bado na Tabora United.na Mashujaa ya Kigoma.

Mimi na hisi Mtibwa wanahangaika kunjoosha kivuli cha Mti ili hali Mti ndio wenye shida, tiba  ni kuukata huo mti.

  Mara baada ya mchezo wa jana kutamatika, Afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobiasi Kifaru Ligalambwike akizungumza na Waandishi wa habari sehemu kubwa ya maelezo yake limtaja kiongozi wa zamani wa Mtibwa  Jamal Baizer akidai toka kiongozi huyo aondoke timu hiyo haina mwenendo mzuri.

Monday, April 29, 2024

PLAY OF.KURUGENZI SIMIYU, YAINGIA MITINI MORO KIDS NJIA NYEUPE KUPANDA DARAJA LA PILI.

             Kikosi kabambe cha Moro Kids

           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Kurugenzi ya Mkoani Simiyu iliyofanya vibara Ligi daraja la Pili na kuangukia kwenye michezo ya Mtoani Maarufu ‘Play Off’juzi imeshindwa kutokea  Uwanja wa Jamhuri Morogoro kukipiga na wenyeji wao Moro Kids.

 Wana wa Pakaya Moro Kids iliyoshika nafasi ya tatu  Ligi ya Mabigwa wa Mikoa iliyotamatika hivi karibu Mkoani Dodoma na kupata tiketi ya kucheza Play Off na timu za daraja la Pili.

Katika mchezo huo wa Play Off dhidi ya Kurugenzi,Moro Kids akifanya vizuri katika michezo yote miwli ya nyumbani na Ugenini itapanda Ligi daraja la pili huku Kurugenzi ikishuka daraja la tatu ngazi ya Mkoa.

  Nayo Kurugenzi akifanya vizuri kwa maana ya kumfunga Moro Kids Uwanja wa Jamhuri  Morogoro,  kisha kumfunga tena au kutoka sare kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Simiyu anasalia Ligi daraja la Pili na Moro Kids inarejea alikotoka Ligi daraja la tatu Mkoa.

Katika mchezo huo waamuzi wa mchezo  walisubiri  kwa muda wa dakika 15 baada ya timu ya Kurugenzi kutoonekana   walimaliza mchezo na Moro Kids wakatoka uwanjani na Vicheko vya furaha ya kuferi kwa mahasimu wao.

Baadhi ya mashabiki wa Soka Mkoani Morogoro waliokuweo uwanjani hapo,walijawa nafuraha wakiamini timu yao ya Moro Kids  imepanda Ligi daraja la Pili.

 Kufuatia hali hiyo Jana majira ya saa 12 jioni Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro Jimmy Lengwe kwa lengo la kupata ufafanuzi wa tukio hilo.

 “Ni kweli Shekidele [jana] Moro Kids walifika uwanjani lakini wapinzani wao Kurugenzi ya Simiyu hawakutokea.

Mimi kama msimamizi wa kituo,na wenzangu kwa maana ya Mechi kamishina  na waamuzi  wote hatuna taarifa zozote juu ya timu hiyo kutofika uwanjani”.alisema Katibu huyo.

Alipoulizwa nini kinafuata baada ya tukio hilo?  alijibu.

“ Sisi sote kwa maana mimi msimami wa kituo kamisaa wa mchezo na waamuzi kwa pamoja tumetuma ripoti zetu bodi ya ligi hivyo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho lakini na kudokeza huenda majibu ya swali lako hilo yakajibikwa kesho kutwa jumanne kwani kamati ya Masaa 72 itaketi na kutoa majibu”alimalizia kusema Lengwe.

               SHERIA ZA TFF NA FFA.

Kwa mujibu wa sheria za shirikisho la Mpira wa Miguu duniani’FFA’ na shirikisho la Mpira Tanzania’TFF’ timu yoyote isipofika uwania bila taarifa itapokwa Pointi na kushushwa madaraja huku mpinzani wake akipewa ushindi wa Pointi 3 na mabao 3.

Hivyo kwa sheria hizo za FFA na TFF kuna uwezekano Mkubwa Wana Morogoro Moro Kids’Full Vipaji’ kupewa ushindi na kupanda Ligi daraja la Pili.


 

Saturday, April 27, 2024

MBUNGE AMTAJA HAYATI MICHAEL JACKSONI KWA WAANDISHI WA HABARI


 

MBUNGE wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Kudumu ya Bunge ]TAMISEMI] Mhe Denis Londo.

 Akizungumza kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa Wanachama wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro, uliofanyika Leo Ukumbi wa  JKT Bwalo la Umwema, amemtaja Mwanamuziki nguli duniani Hayati Michael Jackson.

Kwa nini amemtaja mwanamuziki huyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote

Thursday, April 25, 2024

SALA YA LEO.


 


“Mungu akuongoze katika Maamuzi yako na akuongoze katika njia ya haki.

Utembee katika nuru na upate kibari cha Mungu katika kila eneo la Maisha yako.”

 Kama unaamini sala hii thibitisha kwa kusema  Amen.

Monday, April 22, 2024

KUMBUKIZI YA MIAKA 11 YA KIFO CHA MKALI WA HIP HOP ‘NGWEHA’

           Hayati Mangweha enzi za uhai wake.
Denisia Mangweha ambaye ni Mama Mzazi wa hayati Albert Mangweha akihojiwa na Mtandao huu nyumbani kwake Kihonda Mazimbu Road Morogoro huku akiikumbatia picha ya Mpendwa Mtoto wake, huku akiwa na majonzi makubwa.
Paroko wa Parokia ya Mt. Monica Padre Octavian Msimbe[kati] akiwa na Micheli Raia ya Uingereza[kushoto] mchumba wa hayati Ngweha.

[Kulia] ni Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Hamza Mgaza’ Maarufu M- 2- THE- P ambaye ni rafiki mkubwa wa hayati Mangweha, watatu hao walipozi mbele ya kamera za Mtandao huu kwenye lbada ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Mangweha Mei 28-2014



 Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye kaburi la Mangweha nje ya kanisa  Katoliki Parokia ya Mt Monica Kihonda.


           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 Kumbukizi ya Miaka 11 ya kifo cha Mkali wa muziki wa Bongofleva nchini,  Mwana Morogoro Hayati Albert        Keneth Mangweha’Ngwea’ aliyefariku dunia  Mei 28=2013  nchini Afrika Kusini, na kuzikwa nyumbani kwao Morogoro  kwenye makaburi yaliyopo nje ya kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Parokia ya Mt Monica Kihonda.

Watanzania wengi haswaa Wana Morogoro watakukumbuka daima kamanda Ngwea umeipeperusha nyema bendera ya Mkoa wa Morogoro kwenye tasnia hiyo ya Muziki wa kizazi Kipya miondoko ya ‘Hip Hop’.  

Moja ya wimbo wako uliotia fora nchini ni ule wa ‘Geto langu’         

Panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mei 28 2024 Mwandishi wa Mtandao huu atatinga nyumbani kwa Mama Mangweha ambaye ni mmoja wa viongozi wa Parokia ya Mt. Monica, kushiriki lbada ya kumbuki ya miaka 11 ya kifo cha Mangweha.

Baada ya lbada hiyo nitazungumza  mawili matatu na Mama Mangweha kuelekea miaka 11 ya kifo cha mpendwa mtoto wake huyo aliyekuwa kipenzi cha Watanzania wengi.

Hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.  

                        

  .

 .

 

 

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...