Baada ya jana Mtibwa Sugar kuokea kichao cha bao 2 kwa 1 dhidi ya JKT Tanzania mchezo ambao Mtibwa walikuwa na uwezo wa kuondoka hata na alama moja lakini kwa mshangao dakika ya 9o nikiwa kwenye Luninga naifuatilia timu yetu ya Morogoro.
Wana Morogoro tumeumia sana tukishuhudia Mtibwa ikufungwa bao la 2 dakika ya 9o huku chanzo cha bao hilo ikiwa ni makosa ya mlinda mlango aliyetoa boko kwa kichuya na kuacha gori wazi.
Kichuya baada ya kuona lango liko wazi kafumua shuti lililounganishwa wavuni na Six Sabilo.
Binafsi kuguza Mgonjwa siwezi, kwenye ukweli nasema ukweli unaona kabisa Mgonjwa kazidiwa hata macho habwenzi, uji unamshinda kunywa, kuhema kwake kama maji yanayotokota jikoni.
Wewe unayemuuguza nafsi yako inakushuhudia kabisa kwamba Mgonjwa wako anakaribia kukata roho, unamtia moyo kwa kumwambia maneno ya Tumaini kwamba.
Mgonjwa wangu kuugua sio kufa, kweli hayo ni maneno ya faraja kwa mgonjwa lakini hayatamsaidi kwenye safari yake ya kuelekea kwa Mungu.
kwangu mimi nikiona hivyo na mwambia ukweli, kwamba kila nafsi itaonja umauti na hakuna atakayeishi Milele chini ya jua.
Hata mimi ninayekuugua muda wangu utafika nitaiacha hii duniani na kurejea kwa muumba wangu.
Hivyo ushauri wangu kwako mgonjwa wangu kwa hali ilivyo, tumia muda huu kutubu dhambi zako kwa mwenyezi Mungu, ili wakati wowote akikuita maombi hayo yenye toba. Yakusaidie mbele ya safari
TIMU YA MTIBWA SUGAR.
Kwa mtibwa Sugar yenye Maskani yake katikati ya Mashamba ya Miwa eneo la Manungu Kata ya Mtibwa, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
Kwa sasa taa ya Oil inawaka kwenye Dash Bord la gari lao, muda wowote gari lina Nock na kuzimika.
Kama ni boda boda Mtibwa wamevuta juu Chock wanatembelea mafuta ya Lizevu kwenye Kabreter ambayo hayajai hata kwenye kile kikombe cha kahawa muda wowote boda linazima kwa kukosa wese .
Mtibwa kwa msimu huu imebadili makocha zaidi ya watatu, walinda mlango zaidi ya 3,Kama hiyo haitoshi Mtibwa msimu huu katika kuhangaika kujinusuru na janga la kushuka daraja kwenye usajiri wa dirisha dogo wamesajiri wachezaji zaidi ya 8,
Juhudi zote hizo hazikuza matunda bado timu inafungwa huku wakiukaribia mlango wa kushuka daraja wakikusanya alama 17 akiburuza mkia kwenye ligi hiyo yenye timu 16 huku wakibakiwa na michezo 7.
Kati ya michezo hiyo 7 kuna Simba watakao chezo nao keshokutwa Mei 3, bado na Yanga. Bado na Azam, bado na Tabora United.na Mashujaa ya Kigoma.
Mimi na hisi Mtibwa wanahangaika kunjoosha kivuli cha Mti ili hali Mti ndio wenye shida, tiba ni kuukata huo mti.
Mara baada ya mchezo wa jana kutamatika, Afisa habari wa Mtibwa Sugar Thobiasi Kifaru Ligalambwike akizungumza na Waandishi wa habari sehemu kubwa ya maelezo yake limtaja kiongozi wa zamani wa Mtibwa Jamal Baizer akidai toka kiongozi huyo aondoke timu hiyo haina mwenendo mzuri.
No comments:
Post a Comment