Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, April 29, 2024

PLAY OF.KURUGENZI SIMIYU, YAINGIA MITINI MORO KIDS NJIA NYEUPE KUPANDA DARAJA LA PILI.

             Kikosi kabambe cha Moro Kids

           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Kurugenzi ya Mkoani Simiyu iliyofanya vibara Ligi daraja la Pili na kuangukia kwenye michezo ya Mtoani Maarufu ‘Play Off’juzi imeshindwa kutokea  Uwanja wa Jamhuri Morogoro kukipiga na wenyeji wao Moro Kids.

 Wana wa Pakaya Moro Kids iliyoshika nafasi ya tatu  Ligi ya Mabigwa wa Mikoa iliyotamatika hivi karibu Mkoani Dodoma na kupata tiketi ya kucheza Play Off na timu za daraja la Pili.

Katika mchezo huo wa Play Off dhidi ya Kurugenzi,Moro Kids akifanya vizuri katika michezo yote miwli ya nyumbani na Ugenini itapanda Ligi daraja la pili huku Kurugenzi ikishuka daraja la tatu ngazi ya Mkoa.

  Nayo Kurugenzi akifanya vizuri kwa maana ya kumfunga Moro Kids Uwanja wa Jamhuri  Morogoro,  kisha kumfunga tena au kutoka sare kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Simiyu anasalia Ligi daraja la Pili na Moro Kids inarejea alikotoka Ligi daraja la tatu Mkoa.

Katika mchezo huo waamuzi wa mchezo  walisubiri  kwa muda wa dakika 15 baada ya timu ya Kurugenzi kutoonekana   walimaliza mchezo na Moro Kids wakatoka uwanjani na Vicheko vya furaha ya kuferi kwa mahasimu wao.

Baadhi ya mashabiki wa Soka Mkoani Morogoro waliokuweo uwanjani hapo,walijawa nafuraha wakiamini timu yao ya Moro Kids  imepanda Ligi daraja la Pili.

 Kufuatia hali hiyo Jana majira ya saa 12 jioni Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia simu Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro Jimmy Lengwe kwa lengo la kupata ufafanuzi wa tukio hilo.

 “Ni kweli Shekidele [jana] Moro Kids walifika uwanjani lakini wapinzani wao Kurugenzi ya Simiyu hawakutokea.

Mimi kama msimamizi wa kituo,na wenzangu kwa maana ya Mechi kamishina  na waamuzi  wote hatuna taarifa zozote juu ya timu hiyo kutofika uwanjani”.alisema Katibu huyo.

Alipoulizwa nini kinafuata baada ya tukio hilo?  alijibu.

“ Sisi sote kwa maana mimi msimami wa kituo kamisaa wa mchezo na waamuzi kwa pamoja tumetuma ripoti zetu bodi ya ligi hivyo wao ndio wenye maamuzi ya mwisho lakini na kudokeza huenda majibu ya swali lako hilo yakajibikwa kesho kutwa jumanne kwani kamati ya Masaa 72 itaketi na kutoa majibu”alimalizia kusema Lengwe.

               SHERIA ZA TFF NA FFA.

Kwa mujibu wa sheria za shirikisho la Mpira wa Miguu duniani’FFA’ na shirikisho la Mpira Tanzania’TFF’ timu yoyote isipofika uwania bila taarifa itapokwa Pointi na kushushwa madaraja huku mpinzani wake akipewa ushindi wa Pointi 3 na mabao 3.

Hivyo kwa sheria hizo za FFA na TFF kuna uwezekano Mkubwa Wana Morogoro Moro Kids’Full Vipaji’ kupewa ushindi na kupanda Ligi daraja la Pili.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...