Paroko wa Parokia ya Mt. Monica Padre Octavian Msimbe[kati] akiwa na Micheli Raia ya Uingereza[kushoto] mchumba wa hayati Ngweha.
[Kulia] ni Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Hamza Mgaza’ Maarufu M- 2- THE- P ambaye ni rafiki mkubwa wa hayati Mangweha, watatu hao walipozi mbele ya kamera za Mtandao huu kwenye lbada ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Mangweha Mei 28-2014
Mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye kaburi la Mangweha nje ya kanisa Katoliki Parokia ya Mt Monica Kihonda.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Kumbukizi ya Miaka 11 ya kifo cha Mkali wa muziki wa Bongofleva nchini, Mwana Morogoro Hayati Albert Keneth Mangweha’Ngwea’ aliyefariku dunia Mei 28=2013 nchini Afrika Kusini, na kuzikwa nyumbani kwao Morogoro kwenye makaburi yaliyopo nje ya kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro Parokia ya Mt Monica Kihonda.
Watanzania wengi haswaa Wana Morogoro watakukumbuka daima kamanda Ngwea umeipeperusha nyema bendera ya Mkoa wa Morogoro kwenye tasnia hiyo ya Muziki wa kizazi Kipya miondoko ya ‘Hip Hop’.
Moja ya wimbo wako uliotia fora nchini ni ule wa ‘Geto langu’
Panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mei 28 2024 Mwandishi wa Mtandao huu atatinga nyumbani kwa Mama Mangweha ambaye ni mmoja wa viongozi wa Parokia ya Mt. Monica, kushiriki lbada ya kumbuki ya miaka 11 ya kifo cha Mangweha.
Baada ya lbada hiyo nitazungumza mawili matatu na Mama Mangweha kuelekea miaka 11 ya kifo cha mpendwa mtoto wake huyo aliyekuwa kipenzi cha Watanzania wengi.
Hivyo nakusihi endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
.
.
No comments:
Post a Comment