Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, February 29, 2024

RAIS DAMU CHAFU AVAMIWA NA SHABIKI, BAUNSA AMUOKOA.

     Shabiki wa Black akimfukuza Rais Ayub kwenye gari lao huku Baunsa Big Suma akiingilia kati.

 

Shabiki wa Black People akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu.na nguo lake  jeusi la la mshono wa ‘Kanyeramumo’

Shabiki wa Black mwenye nguo za njano ambaye hapo juu amevaa nguo nyeusi akiwa na nahodha wa timu hiyo lbra Mkaa wakisimamia ugawajiw a chakula
Rais wa Damu Chafu, Ayub Aziz akichupata akificha Pilau huku akimkodolea Macho Mwandishi wa Mtandao akisema’Shekidele karibu tule’
  Rais Ayub akiteta jambo na Nahodha wa timu ya Washachi Fc Said Kapetera
 


        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Rais wa timu ya Damu Chafu yenye Maskani yake Pande za Mafisa Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa, Ayub Aziz amevamiwa na shabiki  wa timu ya Black People alitakiwa kuondoka na mizigo yake nyuma ya gori.

Tukio hilo lililonaswa live na Mwandishi wa Mtandao huu limetokea hivi karibu kwenye mchezo wa Fainali ya Michuano ya Ndondo Cup, uliopigwa Uwanja wa Saba saba kati ya Black People’Taifa la Watu Weusi’ na Damu Chafu Vijana wa Kelvin  Pius John[21] ‘Mbape wa Mji Kasoro Bahari’ anayecheza soko la kulipwa Ulaya timu ya K.R.C GENK inayoshiriki Ligi kuu nchini Ubelgij.

lshu ilikuwa hivi licha ya timu zote mbili kusheheni wachezaji wengi wa ligi kuu, bado mipango ya nje ya uwanja ya kusaka ushindi’Ushirikina’ilipewa nafasi na timu zote mbili.

Awari kabla ya kuanza kwa mchezo huyo wa fainali uliotamatika kwa Black ibuka na ushindi wa Pelnaty 7-6 baada ya dakika 90  kutoka sare  Mwandishi wa Mtandao huu aliwashudia mashabiki wa Black People na wenzao wa Damu Chafu wakihangaika kufukia Vitu Uwanjani.

‘Kichekezo’ ile mageti ya uwanja wa saba saba yanafunguliwa  majira ya saa 8 mchana  Mzee mmoja hakufahamika mara moja ni wa timu gani aliweka mayai viza 2 getini.

ile anaweka tu mayai hayo Kunguru wawili ya Zanzibar wameyapitia na kuondoka nayo,babu katoa macho kama fundi saa kangusha nati,kabaki mdomo wazi akiamini mipango yake ya ushindi imeshavurugwa na Kunguru hao ‘Zoa zoa’

  Gemu ilipoanza sasa mipango hiyo ya kamati za  ufundi  ziliendelea,Mwandishi wa Mtandao huu aliyeketi nyuma ya gori la Black People akipiga Picha matukio mbali mbali, alimuona Rais wa Damu Chafu Ayub Aziz akitinga eneo hilo huku akiwa na kitu mkononi.

 Kunaona hivyo Shabini mmoja wa Black People alimfuta na kumkunja akimuamulu kuondoka nyuma ya gori lao, Rais Ayub aligoma hali iliyopelekea kuibuka kwa majibishano ya maneno makali huku wakisukumana sambamba na kukunjani wakitaka kuzichapa kavu kavu.

Hali hiyo ilimsukuma Baunsa Maarufu Mkoani Morogoro lsmain Juma Almaarufu ‘Big Suma’aliyetinga eneo la tukio na muamulu Rais huyo kuondoka nyuma ya gori na mazaga zaga yake.

“ Kukaa nyuma ya gori la wapinzani wako  ni uchokozi kwa nini usiende kukaa nyuma ya gori la timu yako tunahitaji amani kwenye mchezo huu hivyo naomba uondoka hapa gorini” Alsema baunsa huyo na rais Ayub kutii na kuondoka.

 Mchezo wa Kiungwana ‘Fair Play’Mara baada ya Black People kunyakua ubingwa huo wa Ndondo Cup na kukabidhi Kombe na Pesa Cash Milioni 2.

Uongozi wa timu hiyo uliamua kutumia sehemu ya pesa hizo kuandaa lbada ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka waliofarikim dunia. Rais huyo wa Damu Chafu alialikwa kwenye lbada hiyo.

 RAIS AYUB NA SHABIKI WAKUTANA TENE KWENYE SUFURIA LA PILAU.

Kwenye lbada hiyo Mwandishi wa Mtandao huu aliwashuhudia tena Rais Ayub na Shakini wa Black People wakikutana kwenye sufuri la Pilau. Mwandishi aliacha shughuri zote na kusogea eneo hilo kusaka udaku nini kitatokea tena kati ya wawili hao waliokunyanja Uwajani?

                 KILICHOTOKEA HIKI HIKI.

Shabiki huyo wa  Black People[pichani mwenye Nguo ya Njano mbele ya  sufuria la Pilau ambaye uwanjani  alivaa nguo nyeusi tu akiwakirisha kwa vitendo’Taifa la Watu Weusi’, alipewa jukumu la Uandazi na ugawaji wa Chakula.

Mara paa Rais wa damu Chafu katinga jikoni akihitaji sahani ya Pilau, Shabiki huyo kamtazama kisha kamkumbatia na kumjazia Pilau na Mavyama kibao.

Usimuone hivyo lfamiake Rais huyo wa Damu Chafu  Ayub Aziz ndio mwenye sauti ya Mwisho kwenye timu hiyo na mchezo Kelvin John akiwa huko Ulaya hata awe bize vipi akiiona simu ya  Rais Ayub lazima aipokee.

 lkumbukwe Kelvin John ni Mzaliwa wa Mkoa wa Morogoro na nyumba yao iko jirani kabisa na Maskani ya timu hiyo ya Damu Chafu hivyo anaisaidi timu yake hiyo ya kitaa  kwa kiwango kikubwa. 

Wednesday, February 28, 2024

VIONGOZI MMDFA WAKOSOA IBADA YA KUWAREHEMU WACHEZAJI WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI.

 

Tuliketi kikao cha dharura kama tunavyoonekana Pichani Mwenyekiti Hamis Suff [kuli]mwenye kanzu, Katibu Maharagande anayezungumza kwa ishala ya kunyoosha mkono,Seif Kijiji mwenye kanzu nyeupe na mwisho kushoto ni Mwenyekiti wa Mtaa lssa Chaballa, Mwandishi wa Mtandao huu hayupo pichani,yuko nyuma ya kamera.
Viongozi hao  Mwenyekiti suffi kulia na Maharagande wakiokea dua wakati majina hayo yakisomwa
Shehe mkuu wa Wilaya ya Morogoro akisoma majira ya marehemu hao wakati ibada hiyo iliyofanyika ljumaa iliyopita uwanja wa Shujaa Mji Mpya ikiendelea.

Na Dustan Shekidele Morogoro.
VIONGOZI wa zamani wa chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MMDFA’ Mwenyekiti Hamis Suffi na Katibu wake Kafale Maharagande kwa pamoja wametoa maoni yao yalioambatana na ukosoaji wa lbada ya kuwaombea wanasoka walifariki dunia. 
 
Viongozi hao ambao walialikwa Kwenye lbada hiyo iliyoandaliwa na timu ya Black People na kuongozwa na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Thiney Jaffar, hawakupewa nafasi ya kuzungumza kwenye lbada hiyo jambo lililoonekana kuwakwaza.
Kimsingi walijiataa kuzungumza neon kufuatia mwaliko huo 
 
walioupokea, chaajabu hadi shehe Mkuu wa Wilaya anafunga ibada hiyo viongozi hao wakupewa fursa ya kuzungumza, hivyo kwa kinyongo Mwenyekiti Siffu alijitutumua na kumfuata Mwandishi wa Mtandao huu na kutema nyongo akisema” Shekidele wewe ni Mwandishi wa habari pekee ulioalikwa kwenye lbada hii, kimsingi mimi na mwenzangu Kafale tunawapongeza sana Viongozi wa Black People kwa kuwarehemu wachezaji wa zamani na wadau wa soka.
Lakini masigitiko yetu sisi viongozi wa Soka hatukupewa nafasi ya kuzungumza kwenye lbada hii licha ya kupewa mwaliko rasmi wa kuja hapa.
 
Mfano majina yaliyosoma wadau wengi wa soka hawakutajwa sisi tunawajua Mfano Mzee Ahmed Mumba mkufunzi Maarufu wa Makocha nchini, Mzee Aman Komanya mwenyekiti Mstaafu wa chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro, hao wamefariki hivi karibuni lakini majina yao hatukuyasikia kwenye ile orodha kama tungepewa nafasi ya kuzungumza tungewataja wengi kwenye habari yako utakayoiandika liweke sawa na jambo hili”alisema Mwenyekiti huyo kwa unyonge.
 
Mwandishi wa Mtandao huu alimjibu hivi
”Uko sahihi sana Mwenyekiti lakini kumbuka kwenye shunguli yoyote lazima mapungufu yawepo sasa niombe hilo libebeni kama ni pungufu”. 
 
Ngoja nikamuite Mratibu mkuu wa shughuri hii Seif Kijiji ili muweze kumueleza dukuduku hilo mtokea hapa mkiwana amani ya Moyo” 
 
Mwenyekiti huyo alikubari wazo hilo kwa sharti la kutozungumza yeye akimpa madaraka ya kuzungumza msaidi wake Maharagande. Mwandishi wa Mtandao alimfuta Rais wa Black People Seif Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa ‘ A’ lssa Kitukwa Maarufu lssa Chaballa. 
 
Baada ya kuelezwa Seif Kijiji na lssa Chaballa kwa pamoja walikubali kosa na kuwaomba Msamaha Viongozi hao wambao walipokea msamahama huyo na kuondoka makwao wakiwa na furaha ya amani ya moyo.
 
Alioulizwa juu la jambo hilo shehe mkuu wa wialya alisema" Kwanza ni cheki Shekidele mbona hilo ni jambo dogo kama hao viongozi wangesema tungewapa nafsi wazungumze hakuna shida yoyote"alisema shehe huyo na kuangua kicheko.
 
 

Monday, February 26, 2024

TASWIRA MABINGWA WA NDONDO CUP KUWAREHEMU MAREHEMU

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

HII imekaa poa, juzi Mtandao huu uliripoti habari ya timu ya Black People’Taifa la Watu Weusi’ yenye maskani yake Jijiga jirani na stend ya daladala ya Kaloleni Kata ya Mji Mpya, kufanya ibada maalumu ya kuwarehemu  wachezaji na wadau wa soko waliotangulia mbele za haki.

Baada ya kunyakua ubingwa wa Michuano ya Ndondo Cup iliyoandaliwa na Mdau mmoja wa Soka na kukabidhiwa kombe na pesa taslimu Milioni mbili.

Uongozi wa Black People umeamua kutumia pesa hizo kuandaa lbada hiyo ya kuwaombe marehemu iliyoongozwa na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Thiney Jaffar. Mara baada ya dua Shehe Jaffar alisoma majina ya marehemu hao wake kwa waume wakiwemo pia wachezaji na wadao wa soka wa Mkoa wa Morogoro.

    

Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Sherhe Thiney Jaffar akisoma majina hayo ya marehemu
Cheki picha za majija ya marehemu hao unaweza kuliona jina la mpendwa ndugu yako ambaye alitajwa kwenye ibada hiyo iliyofanyika juzi ljumaa uwanja wa Shujaa Mji Mpya.






Viongopzi wa timu Nane zilizsoshiriki mashindano hayo ya Ndondo Cup Rais wa Damu Chafu Auyu Azz mwenye penzi aliyesimama na mbele yake mwenye kanzu aliyerketi ni Rais wa Wakushi Fc Manzese United Faraji

Ndugu zangu nawasihi na kuihusia pia nafasi yangu kuache maasi na turejee kwa Mwenyezi Mungu.

Angalia orodha hii ya ndugu zetu zote hao wamefariki dunia, juzi tulifanya ibada maalumu ya kuwarehemu.

Mtandao huu unamuomba mwenyezi Mungu awapunguzie adhabu ya Kabri wapendwa wetu hawa na kuwaweka wanapostahiri Kwa kadri walivyoishi hapa duniani.




Nahodha wa timu ya Washashi ya Mji Mpya Said Kapetera naye akificha chakula hiyo ya Mtume. lfahemeke kwenye michuano hiyo ya ndondo Cup Black People alimchapa Washisha bao 1-0

.



 

Sunday, February 25, 2024

TAJIRI ABOOD ASHUHUDIA MASTAA WA LIGI KUU WAKIONYESHANA UNDAVA FAINALI YA NDONDO CUP.

 Papatu  Papatu ya Winga wa Black People Salum Kihimbwa ‘Chuji’[kulia] na beki wa Damu Chafu Jobiso John.




Licha ya Jobiso Kumvuta jezi na kumkata mtama, bado faulo hizo mbili ambazo refa alizimezea filimbi hazikumzuia Kihimbwa kuendelea na safari zake.

Beki kisiki wa Damu Chafu Sady Mapuya akimthibiti mshambuliaji wa Black People Richard Maarufu ‘Richi’



Nahodha wa Balack People lbra Mkaa akiwatambulisha wachezaji wenzake kwa mhe Abood
Wachezaji nyota wa Black Pleople anaokipiga ligi ligi kuu lsmail Mhessakulia anakipiga Mashujaa ya Kigoma na Salum Mkihimbwa'Chuji' anayekipiga lhefu wakiteta jambo labla mchezo huo kuanza. lkumbukwe wawili hao kabla ya kutimkia timu hizo wote walikuwa Mtibwa Sugar
Mh Abood akijianda kumkabidhi kombe la ubingwa Nahodha wa Black People lbrahim Mkaa
              Shabiki lia lia wa Black People Mtu mweusi

waliimba hivi 'Tunapotaka sisi ni hapo tunapotaka sisi ni hapo tu'

 


         Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MBUNGE wa Jimbo la Moropgoro Mjini Mh Aziz Abood wiki iliyopita alishuhudia wachezaji nyota wanaokipiga timu za Ligi Kuu Tanzania Bara na Zanzibar  wakionyeshana umahiri wao kwenye fainali ya Michuano ya Ndondo Cup.

Mastaa hao wa ligi kuu walisheheni kwenye mchezo huo wa fainali uliozikutanisha timu za Black People ‘Taifa la Watu weusi kutoka Jijiga Kata ya Mji Mpya na timu ya Damu Chafu’Vijana wa Kelvin John’ Kutoka Pande za Mafisa Kata ya Mwembesongo.

Timu hizo zinazoogozwa na Marais  Ayubu Aziz  wa Damu Chafu na Seif Kijiji wa Black People zilisheheni wachezaji hao wa ligi kuu kutoka timu za  Mashujaa ya Kigoma ‘Wazee wa Mapigo na Mwendo’ Ihefu ya Mbarali Mbeya, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Tanzania Prinsons,Mbeya City na Mlandege ya Zanzibar. Baadhi ya wachezaji hao ni Salum Kihimbwa ‘Chuji’ anayekipiga lhefu Fc Wababe wa Yanga. lsmail Aidan Mhessa[Maafande wa Mashujaa] Mohamed Kapeta Mbeya City, Sady Mapuya Mlandege ya Zenji na Kipa wa Hassan Dior wa Prinsons.

Wengine ni Omar Manga’Adebayo’ Mkopi na Richi wote kutoka Mtibwa Sugar ya Manungu  Kata ya Mtibwa Tafara ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa. 

Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa February 16 uwanja wa Saba saba,Black People waliinyuka Damu Chafu Pelnaty 7-6 baada ya dakika 90 za awari miamba hiyo kutoka sare. Gemu hiyo ilivyotamatika mgeni Rasmi Mh Abood alimkabidhi nahodha wa Black People lbra Mkaa kombe na pesa taslimu Milion 2.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hizo mashabiki wa Black People wake kwa waume watoto kwa wakubwa waliingia katikati ya uwanja  na kuanza kucheza Muziki wa mavumbini Maarufu Kigodoro.

Kama hiyo haitoshi huku akiwa na kombe lao mashabiki hao waliliamsha shangwe kwa maandamano mpaka Mji Mpya eneo la Kaloleni’Maarufu Jijiga’ huko balaa lilikuwa kubwa.

Baada ya kupokea pesa hizo Juzi ljumaa Black People wakitumia sehemu ya pesa hizo kufanya ibada ya kuwarehemu Marehemu iliyoongozwa na shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

Matukio ya lbada hiyo sambamba na Majina ya marehemu yote waliotajwa yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtanmdao huu muda wote uweze kuyaona majina ya ndugu zetu waliyetajwa na kufanyiwa maombi Maalumu kwenye lbada hiyo.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...