Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, February 29, 2024

RAIS DAMU CHAFU AVAMIWA NA SHABIKI, BAUNSA AMUOKOA.

     Shabiki wa Black akimfukuza Rais Ayub kwenye gari lao huku Baunsa Big Suma akiingilia kati.

 

Shabiki wa Black People akipozi mbele ya kamera za Mtandao huu.na nguo lake  jeusi la la mshono wa ‘Kanyeramumo’

Shabiki wa Black mwenye nguo za njano ambaye hapo juu amevaa nguo nyeusi akiwa na nahodha wa timu hiyo lbra Mkaa wakisimamia ugawajiw a chakula
Rais wa Damu Chafu, Ayub Aziz akichupata akificha Pilau huku akimkodolea Macho Mwandishi wa Mtandao akisema’Shekidele karibu tule’
  Rais Ayub akiteta jambo na Nahodha wa timu ya Washachi Fc Said Kapetera
 


        Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Rais wa timu ya Damu Chafu yenye Maskani yake Pande za Mafisa Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa, Ayub Aziz amevamiwa na shabiki  wa timu ya Black People alitakiwa kuondoka na mizigo yake nyuma ya gori.

Tukio hilo lililonaswa live na Mwandishi wa Mtandao huu limetokea hivi karibu kwenye mchezo wa Fainali ya Michuano ya Ndondo Cup, uliopigwa Uwanja wa Saba saba kati ya Black People’Taifa la Watu Weusi’ na Damu Chafu Vijana wa Kelvin  Pius John[21] ‘Mbape wa Mji Kasoro Bahari’ anayecheza soko la kulipwa Ulaya timu ya K.R.C GENK inayoshiriki Ligi kuu nchini Ubelgij.

lshu ilikuwa hivi licha ya timu zote mbili kusheheni wachezaji wengi wa ligi kuu, bado mipango ya nje ya uwanja ya kusaka ushindi’Ushirikina’ilipewa nafasi na timu zote mbili.

Awari kabla ya kuanza kwa mchezo huyo wa fainali uliotamatika kwa Black ibuka na ushindi wa Pelnaty 7-6 baada ya dakika 90  kutoka sare  Mwandishi wa Mtandao huu aliwashudia mashabiki wa Black People na wenzao wa Damu Chafu wakihangaika kufukia Vitu Uwanjani.

‘Kichekezo’ ile mageti ya uwanja wa saba saba yanafunguliwa  majira ya saa 8 mchana  Mzee mmoja hakufahamika mara moja ni wa timu gani aliweka mayai viza 2 getini.

ile anaweka tu mayai hayo Kunguru wawili ya Zanzibar wameyapitia na kuondoka nayo,babu katoa macho kama fundi saa kangusha nati,kabaki mdomo wazi akiamini mipango yake ya ushindi imeshavurugwa na Kunguru hao ‘Zoa zoa’

  Gemu ilipoanza sasa mipango hiyo ya kamati za  ufundi  ziliendelea,Mwandishi wa Mtandao huu aliyeketi nyuma ya gori la Black People akipiga Picha matukio mbali mbali, alimuona Rais wa Damu Chafu Ayub Aziz akitinga eneo hilo huku akiwa na kitu mkononi.

 Kunaona hivyo Shabini mmoja wa Black People alimfuta na kumkunja akimuamulu kuondoka nyuma ya gori lao, Rais Ayub aligoma hali iliyopelekea kuibuka kwa majibishano ya maneno makali huku wakisukumana sambamba na kukunjani wakitaka kuzichapa kavu kavu.

Hali hiyo ilimsukuma Baunsa Maarufu Mkoani Morogoro lsmain Juma Almaarufu ‘Big Suma’aliyetinga eneo la tukio na muamulu Rais huyo kuondoka nyuma ya gori na mazaga zaga yake.

“ Kukaa nyuma ya gori la wapinzani wako  ni uchokozi kwa nini usiende kukaa nyuma ya gori la timu yako tunahitaji amani kwenye mchezo huu hivyo naomba uondoka hapa gorini” Alsema baunsa huyo na rais Ayub kutii na kuondoka.

 Mchezo wa Kiungwana ‘Fair Play’Mara baada ya Black People kunyakua ubingwa huo wa Ndondo Cup na kukabidhi Kombe na Pesa Cash Milioni 2.

Uongozi wa timu hiyo uliamua kutumia sehemu ya pesa hizo kuandaa lbada ya kuwarehemu wachezaji na wadau wa soka waliofarikim dunia. Rais huyo wa Damu Chafu alialikwa kwenye lbada hiyo.

 RAIS AYUB NA SHABIKI WAKUTANA TENE KWENYE SUFURIA LA PILAU.

Kwenye lbada hiyo Mwandishi wa Mtandao huu aliwashuhudia tena Rais Ayub na Shakini wa Black People wakikutana kwenye sufuri la Pilau. Mwandishi aliacha shughuri zote na kusogea eneo hilo kusaka udaku nini kitatokea tena kati ya wawili hao waliokunyanja Uwajani?

                 KILICHOTOKEA HIKI HIKI.

Shabiki huyo wa  Black People[pichani mwenye Nguo ya Njano mbele ya  sufuria la Pilau ambaye uwanjani  alivaa nguo nyeusi tu akiwakirisha kwa vitendo’Taifa la Watu Weusi’, alipewa jukumu la Uandazi na ugawaji wa Chakula.

Mara paa Rais wa damu Chafu katinga jikoni akihitaji sahani ya Pilau, Shabiki huyo kamtazama kisha kamkumbatia na kumjazia Pilau na Mavyama kibao.

Usimuone hivyo lfamiake Rais huyo wa Damu Chafu  Ayub Aziz ndio mwenye sauti ya Mwisho kwenye timu hiyo na mchezo Kelvin John akiwa huko Ulaya hata awe bize vipi akiiona simu ya  Rais Ayub lazima aipokee.

 lkumbukwe Kelvin John ni Mzaliwa wa Mkoa wa Morogoro na nyumba yao iko jirani kabisa na Maskani ya timu hiyo ya Damu Chafu hivyo anaisaidi timu yake hiyo ya kitaa  kwa kiwango kikubwa. 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...