Tuliketi kikao cha dharura kama tunavyoonekana Pichani Mwenyekiti Hamis Suff [kuli]mwenye kanzu, Katibu Maharagande anayezungumza kwa ishala ya kunyoosha mkono,Seif Kijiji mwenye kanzu nyeupe na mwisho kushoto ni Mwenyekiti wa Mtaa lssa Chaballa, Mwandishi wa Mtandao huu hayupo pichani,yuko nyuma ya kamera.Viongozi hao Mwenyekiti suffi kulia na Maharagande wakiokea dua wakati majina hayo yakisomwaShehe mkuu wa Wilaya ya Morogoro akisoma majira ya marehemu hao wakati ibada hiyo iliyofanyika ljumaa iliyopita uwanja wa Shujaa Mji Mpya ikiendelea.
Na Dustan Shekidele Morogoro.
VIONGOZI wa zamani wa chama Cha Soka Wilaya ya Morogoro’MMDFA’ Mwenyekiti Hamis Suffi na Katibu wake Kafale Maharagande kwa pamoja wametoa maoni yao yalioambatana na ukosoaji wa lbada ya kuwaombea wanasoka walifariki dunia.
Viongozi hao ambao walialikwa Kwenye lbada hiyo iliyoandaliwa na timu ya Black People na kuongozwa na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Shehe Thiney Jaffar, hawakupewa nafasi ya kuzungumza kwenye lbada hiyo jambo lililoonekana kuwakwaza.
Kimsingi walijiataa kuzungumza neon kufuatia mwaliko huo
walioupokea, chaajabu hadi shehe Mkuu wa Wilaya anafunga ibada hiyo viongozi hao wakupewa fursa ya kuzungumza, hivyo kwa kinyongo Mwenyekiti Siffu alijitutumua na kumfuata Mwandishi wa Mtandao huu na kutema nyongo akisema” Shekidele wewe ni Mwandishi wa habari pekee ulioalikwa kwenye lbada hii, kimsingi mimi na mwenzangu Kafale tunawapongeza sana Viongozi wa Black People kwa kuwarehemu wachezaji wa zamani na wadau wa soka.
Lakini masigitiko yetu sisi viongozi wa Soka hatukupewa nafasi ya kuzungumza kwenye lbada hii licha ya kupewa mwaliko rasmi wa kuja hapa.
Mfano majina yaliyosoma wadau wengi wa soka hawakutajwa sisi tunawajua Mfano Mzee Ahmed Mumba mkufunzi Maarufu wa Makocha nchini, Mzee Aman Komanya mwenyekiti Mstaafu wa chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro, hao wamefariki hivi karibuni lakini majina yao hatukuyasikia kwenye ile orodha kama tungepewa nafasi ya kuzungumza tungewataja wengi kwenye habari yako utakayoiandika liweke sawa na jambo hili”alisema Mwenyekiti huyo kwa unyonge.
Mwandishi wa Mtandao huu alimjibu hivi
”Uko sahihi sana Mwenyekiti lakini kumbuka kwenye shunguli yoyote lazima mapungufu yawepo sasa niombe hilo libebeni kama ni pungufu”.
Ngoja nikamuite Mratibu mkuu wa shughuri hii Seif Kijiji ili muweze kumueleza dukuduku hilo mtokea hapa mkiwana amani ya Moyo”
Mwenyekiti huyo alikubari wazo hilo kwa sharti la kutozungumza yeye akimpa madaraka ya kuzungumza msaidi wake Maharagande. Mwandishi wa Mtandao alimfuta Rais wa Black People Seif Kijiji pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa ‘ A’ lssa Kitukwa Maarufu lssa Chaballa.
Baada ya kuelezwa Seif Kijiji na lssa Chaballa kwa pamoja walikubali kosa na kuwaomba Msamaha Viongozi hao wambao walipokea msamahama huyo na kuondoka makwao wakiwa na furaha ya amani ya moyo.
Alioulizwa juu la jambo hilo shehe mkuu wa wialya alisema" Kwanza ni cheki Shekidele mbona hilo ni jambo dogo kama hao viongozi wangesema tungewapa nafsi wazungumze hakuna shida yoyote"alisema shehe huyo na kuangua kicheko.
No comments:
Post a Comment