Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, February 25, 2024

TAJIRI ABOOD ASHUHUDIA MASTAA WA LIGI KUU WAKIONYESHANA UNDAVA FAINALI YA NDONDO CUP.

 Papatu  Papatu ya Winga wa Black People Salum Kihimbwa ‘Chuji’[kulia] na beki wa Damu Chafu Jobiso John.




Licha ya Jobiso Kumvuta jezi na kumkata mtama, bado faulo hizo mbili ambazo refa alizimezea filimbi hazikumzuia Kihimbwa kuendelea na safari zake.

Beki kisiki wa Damu Chafu Sady Mapuya akimthibiti mshambuliaji wa Black People Richard Maarufu ‘Richi’



Nahodha wa Balack People lbra Mkaa akiwatambulisha wachezaji wenzake kwa mhe Abood
Wachezaji nyota wa Black Pleople anaokipiga ligi ligi kuu lsmail Mhessakulia anakipiga Mashujaa ya Kigoma na Salum Mkihimbwa'Chuji' anayekipiga lhefu wakiteta jambo labla mchezo huo kuanza. lkumbukwe wawili hao kabla ya kutimkia timu hizo wote walikuwa Mtibwa Sugar
Mh Abood akijianda kumkabidhi kombe la ubingwa Nahodha wa Black People lbrahim Mkaa
              Shabiki lia lia wa Black People Mtu mweusi

waliimba hivi 'Tunapotaka sisi ni hapo tunapotaka sisi ni hapo tu'

 


         Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MBUNGE wa Jimbo la Moropgoro Mjini Mh Aziz Abood wiki iliyopita alishuhudia wachezaji nyota wanaokipiga timu za Ligi Kuu Tanzania Bara na Zanzibar  wakionyeshana umahiri wao kwenye fainali ya Michuano ya Ndondo Cup.

Mastaa hao wa ligi kuu walisheheni kwenye mchezo huo wa fainali uliozikutanisha timu za Black People ‘Taifa la Watu weusi kutoka Jijiga Kata ya Mji Mpya na timu ya Damu Chafu’Vijana wa Kelvin John’ Kutoka Pande za Mafisa Kata ya Mwembesongo.

Timu hizo zinazoogozwa na Marais  Ayubu Aziz  wa Damu Chafu na Seif Kijiji wa Black People zilisheheni wachezaji hao wa ligi kuu kutoka timu za  Mashujaa ya Kigoma ‘Wazee wa Mapigo na Mwendo’ Ihefu ya Mbarali Mbeya, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Tanzania Prinsons,Mbeya City na Mlandege ya Zanzibar. Baadhi ya wachezaji hao ni Salum Kihimbwa ‘Chuji’ anayekipiga lhefu Fc Wababe wa Yanga. lsmail Aidan Mhessa[Maafande wa Mashujaa] Mohamed Kapeta Mbeya City, Sady Mapuya Mlandege ya Zenji na Kipa wa Hassan Dior wa Prinsons.

Wengine ni Omar Manga’Adebayo’ Mkopi na Richi wote kutoka Mtibwa Sugar ya Manungu  Kata ya Mtibwa Tafara ya Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa. 

Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa February 16 uwanja wa Saba saba,Black People waliinyuka Damu Chafu Pelnaty 7-6 baada ya dakika 90 za awari miamba hiyo kutoka sare. Gemu hiyo ilivyotamatika mgeni Rasmi Mh Abood alimkabidhi nahodha wa Black People lbra Mkaa kombe na pesa taslimu Milion 2.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hizo mashabiki wa Black People wake kwa waume watoto kwa wakubwa waliingia katikati ya uwanja  na kuanza kucheza Muziki wa mavumbini Maarufu Kigodoro.

Kama hiyo haitoshi huku akiwa na kombe lao mashabiki hao waliliamsha shangwe kwa maandamano mpaka Mji Mpya eneo la Kaloleni’Maarufu Jijiga’ huko balaa lilikuwa kubwa.

Baada ya kupokea pesa hizo Juzi ljumaa Black People wakitumia sehemu ya pesa hizo kufanya ibada ya kuwarehemu Marehemu iliyoongozwa na shehe Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

Matukio ya lbada hiyo sambamba na Majina ya marehemu yote waliotajwa yataruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtanmdao huu muda wote uweze kuyaona majina ya ndugu zetu waliyetajwa na kufanyiwa maombi Maalumu kwenye lbada hiyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...