MWANA
BIRTHDAY Dustan Shekidele alivyosheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto
wenye ulemavu wa viungo na Vijana yatima. Angalia Clips Video hiyo kwenye kurasa za Facebook za Shekidele mkude simba na ile ya Dustan Shekidele
MWANA
BIRTHDAY Dustan Shekidele alivyosheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto
wenye ulemavu wa viungo na Vijana yatima. Angalia Clips Video hiyo kwenye kurasa za Facebook za Shekidele mkude simba na ile ya Dustan Shekidele
Na Mwandishi Wetu, Morogoro.
MWANANCHI wa kawaida ‘Mtoto wa Mkulima’Dustan Shekidele Mkazi wa Mji Mpya Mkoani Morogoro juzi alisheherekea siku yake ya kuzaliwa’Happy Birthday’ na Watoto wenye ulemavu wa Viungo na Vijana Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Mehayo kilichopo Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro.
Shekidele ambaye kitaaruma ni Mwandishi wa habari alizaliwa Desemba 25 miaka kadhaa iliyopita siku ambapo pia Mwana wa Mungu Mesia Yesu Kristo’Nabii lssa’ alizaliwa tarehe hiyo hiyo takribani miaka elf 2 iliyopita huku kumbikizi yake hiyo kupewa jina la ‘Merry Christmas’.
Katika kusheherekea siku hiyo ndugu, jamaa na Marafiki walipanga kumuandalia sherehe kabambe ya kumpongeza Shekidele kwa kuongeza mwaka, huku wengine wakimtumia zawadi mbali mbali zikiwemo keki.
Shekidele alikataa ofa hiyo ya kwenda ukumbini kusheherekea siku yake hiyo kwa kuwanywesha watu Pombe na Vyakula vya kifahari ili hali kuna watoto na vijana yatina wanaohitaji Msaada wetu.
Kwa kuzingatia hilo kapiga chini ofa hizo za kwenda ukumbini na badala yake kaenda kituo cha Mehayo kusheherekea siku yake hiyo na Watoto hao.
Mwana Birthday huyo alipofika kwenye kituo hicho alipokelewa kwa upendo mkubwa na watoto hao na moja kwa moja akapelekwa kwenye ukumbi wa kituo hicho na kusheherekea Birthday kwa utukufu wa MUNGU walikata keki na kula kwa pamoja.
Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo Shekidele alisema.
”Siku zote siangalii maisha yangu binafsi nangalia maisha ya watu wengine hasa wale wenye uhitaji, kweli ninandugu na Marafiki wengi wenye uwezo ambao tungefanya sherehe kapambe.
Binafsi nimeona hilo halina utukufu mbele za Mungu ningewafurahisha wanadamu kwa kuwapa Pombe na chakula huku nikimchukiza Mungu aliyenipa zawadi ya kuongeza mwaka.
Hivyo nimeamua kuja hapa Mehayo Centre kusheherekea Birthday yangu na ndugu zangu hao ambao pia wanahitaji faraja na misaada yetu”alisema Shekidele.
Kwa upande wake Matron wa kituo hicho Esther alisema” Watoto hao wanahitaji faraja ya mara kwa mara kutokana na changamoto wanazopitia hivyo kitendo chako cha kuwakumbuka kwa kusheherekea nao siku yako ya kuzaliwa nifaraja kubwa sana kwao na Mungu atakubariki.
Kwa muda mrefu hatujaona mtu akija hapa kufanya shehere yotote na watoto hao wewe ndio wa kwanza ubarikiwe sana”alisema.
Baada ya sherehe hiyo kutamatika Shekidele aliwashuhudia baadhi ya watoto hao wakivaa nguo zilizochanika jambo ambalo lilimgusa sana.
Hivyo siku iliyofuata yaani jana Desemba 28 alikusanya nguo nyingi nyumbani kwake na kwenda kuwakabidhi.
Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Shekidele aliingia kazini na kuzungumza na Matroni huyo ambapo amefunguka mazito wanayokutana nayo kwenye kituo hicho moja ya changamoto alizotaja ni baadhi ya watu kuelekeza mitaro ya maji Machafu kwenye kituo hicho jambo ambalo linaweza kuibua magonjwa ya mlipuko kwa watoto hao.
Clip Video za matukio hayo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MARA baada ya Mwana kwaya ‘Soro Rist’wa kwaya ya Sifuni, hayati Rehema Chao’ Maarufu Noela’ kufariki dunia kwa ajari akiwa njiani kuelekea Jijini Arusha Kufunga ndoa na Mchumba’ke Aman Moleni, maswali mengi yaliibua,Kwamba Pete hiyo ya Uchumba‘Engagement’amezikwa nayo au amevuliwa na kurejeshewa kwa Mchumba’ke huyo aliyemfisha siku chache kabla ya kufunga ndoa Jumamosi ya Desemba 2.
Kufuatia Maswali hayo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga kanisa la Kiinjiri la Kiluteheri Tanzania’KKKT’ Usharika wa Mji Mpya na kuzungumza na Mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Godfrey Nyange ambaye alikuwa mtu wa karibu sana na hayati Noera.
Kwa kulitambua hilo Mara baada ya kutinga kanisani hapo Juzi mchana,nje ya Mlango mkuu wa kuingia kanisani Mwandishi aliwashuhudia Mchungaji Dunia anayechunga Kondoo wa Usharika wa Mji Mpya akipiga Story na Mchungaji Tengeneza anayeongoza waumini wa KKKT Usharika wa Kolla.
Mara baada ya kumuona Mwandishi huyo Mchungaji Tengeneza alimtania akisema” Shekidele Jumapili sijakuona Kanisani ulisari wapi”?
Mwandishi alimjibu “ Siunajua huu ni Mwezi wa Maokoto nilisari KKKT Usharika wa Mji Mwema kwa mchungaji Simba kulikuwa na Kipa lmara;”
Baada ya maongezi hayo Mtandao huu aliwaacha Wachungaji hao na kuingia Ofisi ya Mwinjilisti Nyange na kuzungumza naye juu ya kifo cha Noela.
lfahamike Mwandishi huyo anaye sari kanisani hapo aliamua kumruka Mchumbani Dunia na kwenda kuzungumza naMsaidizi wake,hii ni kwa sababu ya ukaribu wa Mwinjilisti huyo na hayati Noela.
Kwa kudokeze tu siku ya harusi ya Mwinjilisiti Nyange iliyofungwa takribani miaka 2 iliyopita hayati Noela alikuwa mstati wa mbele kwenye harusi hiyo iliyofanyika ukumbi wa Tanzanate Msamvu.
Mara baada ya Noera kufariki dunia Novembar 28 na kuzikwa Desemba 2, Mwandishi wa habari hizi alichungulia Profari la Mtandao wa WhatSap na kushuhudia Mwinjilisti Nyange aliweka Picha ya Noela.
Hadi juzi wakati Mwandishi wa habari hizi anachati na Mwinjilisiti huyo kupitia Mtandao huu wa Whatsap alishuhudia Picha ya Noera ikiendelea kusalia eneo hilo.
Alipowasili ndani ya Ofisi ya Mwinjilisti Mahojiano yalikuwa hivi.
Mwandishi. Habari Mtumishi wa Mungu na Poleni kwa msiba Mzito.
Mwinjilisti. Asante Msiba ni wetu sote hata wewe pia pole kwa kuondokewa na Mwana kwaya mwenzenu.
Mwandishi.Asante najua fika wewe ni mtu wakaribu sana na hayati Noela ndio maana nimemruka Mchungaji hapo Nje nimekuja kuongea na wewe nikiamini nitapata madini mengi juu ya kifo hicho cha Mpendwa wetu aliyezimika kama Mshumaa.
Mwinjilisti. Ni kweli Shekidele Noela alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana na siku anaanza safari nilichati naye akinifahamisha kwamba ameniombea Lifti kwenye gari la Mke wa Mchungaji wa KKKT Usharika wa Bungo nielekea kwenye harusi yake.
Baada ya kuchati naye hiyo asubuhi nilikuja hapa ofisini nilipoingia tu nilipata homa la ghafra nikaomba ruhusa nikaenda kulala nyumbani, unajua mtu wako wa karibu akipata tatizo nawe kuna ishara unaziona.
Majira ya jioni napigiwa simu nikielezwa Noela amefariki dunia homa lilipona muda huo huo nikampigia mchungaji kuthibitisha akaniambia ni kweli hayo uliyosikia Noela natunaye tena amepata ajali .
Mwandishi. Je ulifanikwa kwenda kumzika na amezikwa lini na wapi?
Mwinjilisti. Mungu alinipa kibari cha kwenda kumzika Noela, tumemzika Desemba 2 Kijijini Kwao Moshi, siku tuliomzika ndio ilikuwa siku ya harusi yake.
Mwandishi. Tunajua Kabla ya harusi alivishwa pete ya Uchumba na Mchumba’ke je amezikwa na Pete hiyo au amevuliwa na kurejeshwa kwa mchumba’ke? kiimani jambo hilo likoje?
Mwinjilisiti. Lile lilikuwa agano la Noela na Mchumba’ke Aman Molen sasa kwa kuwa Noela amefariki agano hilo limevunjika, Kavuliwa Pete imerejeshwa kwa aliyemvisha.
Kiimani angezikwa nayo ingekuwa na maana kwamba agano hilo halijavunjika na huyu Mchumba’ke asingepata nafasi ya kuchumbia tena kwa kuwa agano lake la awari hajalivunja.
Ifahamike Pete inamaana kubwa sana kwenye maagano ndio maana kabla ya Maharusi au wachumba kuvishana pete ni lazima zibarikiwe na Mtumishi wa Mungu.
Mwandishi Asante Mtumishi kwa ushirikiano wako.
Mwinjilisti Asante na wewe kwa kuja
Afande Ally Chinga Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...