Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, December 25, 2023

KUMBUKIZI YA BIRTHDAY.





TAIFA la watu wa Mungu, familia ya Mungu, duniani kote leo Desemba 25 wanashehereke kusiku ya kuzaliwa Mtoto wao Mesia Yesu Kristo[Nabii lssa] aliyetajwa kwenye vitabu vyote vya dini. 
 
Sherehe hiyoHappy Birthday hiyo imepewa jina la Mery Chrismas ambapo leo dunia yote inasimama kupisha siku hiyo Muhimu. 
 
Katika hali ya kushangaza Mama Mzazi wa Yesu Bikira Maria mara baada ya kuhisia anaujauzito wa Yesu alipasa sauti akisema toka nizaliwe simjui Mwanaume hii Mimba nimeipataje? Malaika wa bwana akamtokea akamwambia usihofu huyo ni Mwana wa Mungu na utazaa hivi karibu. 
 
Baada ya siku kadhaa mbele Desemba 25 Bikira Maria alijifungua Mtoto wa Kiume ndani ya zizi la Ng’ombe na akapewa jina la Yesi Kristo Mokozi wa Ulimwengu. 
 
Mara baada ya Yesu kufanya maajabu makubwa ya kimungu Wapinzania wake walimteka na kumfunga majeredi na mataji ya Miba wakamuua kisha wakampigilia misumari Msalabani.
 
Baadae walimshusha Msalabani na kwenda kumzika kwa mshangazo wawengi baada ya siku tatu yesu alifufuka, kaburi lake lilifunikwa na mawe makubwa lilifunuka kwa miujiza ya Mungu mwana huyo wa Mungu akapaa Mbinguni kwa baba yake. 
 
                        FAMILIA YA SHEKIDELE
 
Familia ya Shekidele kupitia kwa Bi. Tumain Samwel Juma Mshimbula’Mrs Shekidele’Desemba 25 miakaa kadhaa iliyopita Mama huyo alipata ujauzito na kukimbizwa hospital ya Bombo jijini Tanga siku hiyo hiyo ya Desemba 25 alijifungua Mtoto wa kiume aliyepewa jina la Ubatizo Dustan Shekidele.
 
Hivyo familia hiyo ya Shekidele leo Desemba 25 inaungana wa watu wote waliozaliwa siku ya leo akiwemo Mesi wetu Yesi Kristo. Naendelea 
 
Keki yangu leo nakwenda kuikata na kuila na watoto yatima kwenye moja ya vituo vya kulelea watoto hao huku pia nikiwabebea zawadi kadhaa. 
 
Nakushukuru MUNGU kwa kendelea kunipa zawadi ya Uahi sina chakukulipa Zaidi ya kuendeleakutenda mambo mema yanayokupendeza wewe na malaika wako 
 
                      “Happy Birthday to Me” 
 
                                   SHUKRANI. 
 
Nawashukuru wazazi wangu, kaka na dada zangu pamoja na wadogo zangu. 
 
Wangu Tumain na Neema, Waandishi na wapiga Picha wenzangu .Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia ngazi ya Mtaa mpata taifa, Viongozi wa dini zote mbili,
majirani zangu pamoja na marafiki zangu kwenye mitandao ya Kijamii hakika leo mmenionyesha upendo wa thati lilichelewa kuwasha data ile naingia Facebook nakutana na jumbe zenu za kunitakia afya njema kwenye siku yangu hii muhimu, nasema kutoka chini  ya sakafu ya Moyo 
 
wangu Mungu awabariki wote walionipongeza sms zenu  sitazifuta kwenye eneo hilo zitabaki kama kumbukumbu kwenye maisha yangu.



 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...