Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, December 21, 2023

MTUMISHI WA MUNGU ATOA UFAFANUZI PETE YA UCHUMBA ALIYOFISHWA HAYATI NOERA.

Mwinjilisti Nyange akiongoza moja ya lbada kwenye usharika huo.
Hayati Noela enzi za Uhai wake na Picha hii ndio inasoma kwenye Profaili la Mtumishi Nyange.

                                   Mwinjilisti Nyange


   Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MARA baada ya Mwana kwaya ‘Soro Rist’wa kwaya ya Sifuni, hayati Rehema Chao’ Maarufu Noela’ kufariki dunia kwa ajari akiwa njiani kuelekea Jijini Arusha Kufunga ndoa na Mchumba’ke Aman Moleni, maswali mengi yaliibua,Kwamba Pete hiyo ya Uchumba‘Engagement’amezikwa nayo au amevuliwa na kurejeshewa kwa Mchumba’ke huyo aliyemfisha siku chache kabla ya kufunga ndoa Jumamosi ya Desemba 2.

Kufuatia Maswali hayo Mwandishi wa Mtandao huu alitinga kanisa la Kiinjiri la Kiluteheri Tanzania’KKKT’ Usharika wa Mji Mpya na kuzungumza na Mtumishi wa Mungu Mwinjilisti Godfrey Nyange ambaye alikuwa  mtu wa karibu sana na hayati Noera.

Kwa kulitambua hilo Mara baada ya kutinga kanisani hapo  Juzi mchana,nje ya Mlango mkuu wa kuingia kanisani Mwandishi  aliwashuhudia Mchungaji Dunia anayechunga Kondoo wa Usharika wa Mji Mpya akipiga Story na Mchungaji Tengeneza anayeongoza waumini wa KKKT Usharika wa Kolla.

Mara baada ya kumuona Mwandishi huyo Mchungaji Tengeneza alimtania akisema” Shekidele Jumapili sijakuona  Kanisani ulisari wapi”?

Mwandishi alimjibu “ Siunajua huu ni Mwezi wa Maokoto nilisari KKKT Usharika wa Mji Mwema kwa mchungaji Simba  kulikuwa na Kipa lmara;”

Baada ya maongezi hayo  Mtandao huu aliwaacha Wachungaji hao na kuingia Ofisi ya Mwinjilisti Nyange na kuzungumza naye juu ya kifo cha Noela.

lfahamike Mwandishi huyo anaye sari kanisani hapo aliamua kumruka Mchumbani Dunia na kwenda kuzungumza naMsaidizi wake,hii ni kwa sababu ya ukaribu wa Mwinjilisti huyo na hayati Noela.

Kwa kudokeze tu siku ya harusi ya Mwinjilisiti Nyange iliyofungwa takribani miaka 2 iliyopita hayati Noela alikuwa mstati wa mbele kwenye harusi hiyo iliyofanyika ukumbi wa Tanzanate Msamvu.

Mara baada ya Noera kufariki dunia Novembar 28 na kuzikwa Desemba 2, Mwandishi wa habari hizi alichungulia  Profari la Mtandao wa WhatSap  na kushuhudia  Mwinjilisti Nyange aliweka Picha ya Noela.

Hadi juzi wakati Mwandishi wa habari hizi anachati na Mwinjilisiti huyo kupitia Mtandao huu wa Whatsap alishuhudia Picha ya Noera ikiendelea kusalia eneo hilo.

Alipowasili ndani ya Ofisi ya Mwinjilisti Mahojiano yalikuwa hivi.

Mwandishi. Habari Mtumishi wa Mungu na Poleni kwa msiba Mzito.

Mwinjilisti. Asante Msiba ni wetu sote hata wewe pia pole kwa kuondokewa na Mwana kwaya mwenzenu.

Mwandishi.Asante najua fika wewe ni mtu wakaribu sana na hayati Noela ndio maana nimemruka Mchungaji hapo Nje nimekuja kuongea na wewe nikiamini nitapata madini mengi juu ya kifo hicho cha Mpendwa wetu  aliyezimika kama Mshumaa.

Mwinjilisti. Ni kweli Shekidele Noela alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana na siku anaanza safari nilichati naye akinifahamisha kwamba ameniombea Lifti kwenye gari la Mke wa Mchungaji wa KKKT Usharika wa Bungo nielekea kwenye harusi yake.

Baada ya kuchati naye hiyo asubuhi nilikuja hapa ofisini nilipoingia tu nilipata homa la ghafra nikaomba ruhusa nikaenda kulala nyumbani, unajua mtu wako wa karibu akipata tatizo nawe kuna ishara unaziona.

Majira ya jioni napigiwa simu nikielezwa  Noela amefariki dunia homa lilipona muda huo huo nikampigia mchungaji kuthibitisha akaniambia ni kweli hayo uliyosikia Noela natunaye tena amepata ajali .

Mwandishi. Je ulifanikwa kwenda kumzika na amezikwa lini na wapi?

Mwinjilisti. Mungu alinipa kibari cha kwenda kumzika Noela, tumemzika Desemba 2 Kijijini Kwao Moshi, siku tuliomzika ndio ilikuwa siku ya harusi yake.

Mwandishi. Tunajua Kabla ya harusi alivishwa pete ya Uchumba na Mchumba’ke je amezikwa na Pete hiyo au amevuliwa na kurejeshwa kwa mchumba’ke?  kiimani jambo hilo likoje?

Mwinjilisiti. Lile lilikuwa agano la Noela na Mchumba’ke Aman Molen sasa kwa kuwa Noela amefariki agano hilo limevunjika, Kavuliwa Pete imerejeshwa kwa aliyemvisha.

 Kiimani angezikwa nayo ingekuwa na maana kwamba agano hilo halijavunjika na huyu Mchumba’ke asingepata nafasi ya kuchumbia tena kwa kuwa agano lake la awari hajalivunja.

Ifahamike Pete inamaana kubwa sana kwenye maagano ndio maana kabla ya Maharusi au wachumba kuvishana pete  ni lazima zibarikiwe na Mtumishi wa Mungu.

Mwandishi Asante Mtumishi kwa ushirikiano wako.

Mwinjilisti  Asante na wewe kwa kuja   

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...