Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, December 29, 2023

MATENDO YA HURUMA. MWANA BIRTHDAY ASHEHEREKEA KUMBUKIZI YAKE NA WATOTO YATIMA.


Shekidele akiwarisha keki baadhi ya watoto hao juzi.
Matron Esther akimrisha Keki Shekidele kwa niaba ya Uongozi wa kituo hicho.

Shekidele akiwakabidhi zawadi ya nguo wapendwa wetu hao Jana jioni.


 


             Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

MWANANCHI wa kawaida  ‘Mtoto wa Mkulima’Dustan Shekidele Mkazi wa Mji Mpya Mkoani Morogoro juzi alisheherekea siku yake  ya kuzaliwa’Happy Birthday’ na  Watoto wenye ulemavu wa Viungo na Vijana Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Mehayo kilichopo Kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro.

Shekidele ambaye kitaaruma ni Mwandishi wa habari alizaliwa Desemba 25 miaka kadhaa iliyopita siku ambapo pia Mwana wa Mungu Mesia Yesu Kristo’Nabii lssa’  alizaliwa tarehe  hiyo hiyo takribani miaka elf 2 iliyopita huku kumbikizi yake hiyo kupewa jina la  ‘Merry Christmas’.

Katika kusheherekea siku hiyo ndugu, jamaa  na Marafiki walipanga kumuandalia sherehe kabambe ya kumpongeza Shekidele kwa kuongeza mwaka, huku wengine wakimtumia zawadi mbali mbali zikiwemo keki.

Shekidele alikataa ofa hiyo ya kwenda ukumbini kusheherekea siku yake hiyo kwa kuwanywesha watu Pombe na Vyakula vya kifahari ili hali  kuna watoto na vijana yatina wanaohitaji Msaada wetu.

 Kwa kuzingatia hilo kapiga chini ofa hizo za kwenda ukumbini na badala yake kaenda  kituo cha Mehayo kusheherekea siku yake hiyo na Watoto hao.

Mwana Birthday huyo alipofika kwenye kituo hicho alipokelewa kwa upendo mkubwa na watoto hao na moja kwa moja akapelekwa kwenye ukumbi wa kituo hicho na kusheherekea Birthday kwa utukufu wa MUNGU walikata keki na kula kwa pamoja.

Akizungumza na Mtandao huu mara baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo Shekidele alisema.

 ”Siku zote siangalii maisha yangu binafsi nangalia maisha ya watu wengine hasa wale wenye uhitaji, kweli ninandugu na Marafiki wengi wenye uwezo ambao tungefanya sherehe kapambe.

Binafsi nimeona hilo halina utukufu mbele za Mungu ningewafurahisha wanadamu kwa kuwapa Pombe na chakula huku nikimchukiza Mungu aliyenipa zawadi ya kuongeza mwaka.

 Hivyo nimeamua kuja hapa Mehayo Centre kusheherekea Birthday yangu na ndugu zangu hao ambao pia wanahitaji faraja na misaada yetu”alisema Shekidele.

Kwa upande wake  Matron wa kituo hicho Esther alisema” Watoto hao wanahitaji faraja ya mara kwa mara kutokana na changamoto wanazopitia hivyo kitendo chako cha kuwakumbuka kwa kusheherekea nao siku yako ya kuzaliwa nifaraja kubwa sana kwao na Mungu atakubariki.

 Kwa muda mrefu hatujaona mtu akija hapa kufanya shehere yotote na watoto hao wewe ndio wa kwanza ubarikiwe sana”alisema.

Baada ya sherehe hiyo kutamatika Shekidele aliwashuhudia baadhi ya watoto hao wakivaa nguo zilizochanika jambo ambalo lilimgusa sana.

Hivyo siku iliyofuata yaani jana Desemba 28 alikusanya nguo nyingi nyumbani kwake na  kwenda  kuwakabidhi. 

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Shekidele aliingia kazini na kuzungumza na Matroni huyo ambapo amefunguka mazito wanayokutana nayo  kwenye kituo hicho moja ya changamoto alizotaja ni baadhi ya watu kuelekeza mitaro ya maji Machafu kwenye kituo hicho jambo ambalo linaweza kuibua magonjwa ya mlipuko kwa watoto hao.

Clip Video za matukio hayo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

                         


 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...