Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, October 11, 2023

TANZIA. AFANDE ANGUKA GHAFLA UWANJANI NA KUFARIKI DUNIA.

                        Marehemu Tumaini enzi za Uhai wake
Marehemu Tumaini wapili kutoka Kushoto enzi za uhai wake akiwa na wachezaji wenzie wa Reli Family kutoka Kushoto ni Mohamed Mtono, hayati Tumaini, Peter Mjata na kulia ni Ally Jangalu. lkumbukwe baada ya timu ya Reli ya Morogoro; Maaruru Reli Kiboko ya Vigogo’ kufa’ wachezaji wa timu hiyo waliamua kuanzisha timu yao waliyopita jina la Reli Family ikiundwa na wachezaji na mashabiki wa Reli kiboko ya Vigogo’

 Academy mbali mbali zikituma salamu za rambi rambi kwenye mitandao ya Kijamii.


Na Dustan Shekidel,Morogoro.

MCHEZAJI wa timu ya Reli Veterani Maarufu Reli Family] Afande Tumaini anadaiwa kuanguka ghafla wakati akifanya mazoezi na timu yake Reli Family juzi kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mwere.

Taarifa zinadai baada ya kuanguka  Polisi huyo Mstaafu alikimbizwa hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro iliyojirani kabisa na shule hiyo ya Mwere.

 lmeelezwa baada ya kufikishwa hospital Mpendwa wetu Kamanda Tumaini alifariki dunia.

Enzi za uhai wake Afande Tumaini aliwahi kuichezea timu ya Polisi Morogoro baadae akawa kiongozi wa timu hiyo kabla ya kustaafu miaka ya hivi karibu na kusomea ukocha wa Mpira wa Miguu.

Hadi umauti unamfikia Afande Tumaini alikuwa  Mwanachama wa Chama Cha Makocha Mkoa wa Morogoro’TAFCA’ akiwa miongoni mwa makocha wa timu za Vijana za  Taasisi Mpya ya kukuza na kuibua vipaji ya Uluguru Mountain Centre akiwa kocha Mkuu wa timu ya Vijana chini ya miaka 13 ‘Under 13’ huku timu ya Vijana Under 20 ikifundishwa na Kocha Mkuu Ally Jangalu akisaidiwa na Mohamed Mtono, na Kocha wa Makipa Bure Mtagwa.

lfahamike Viongozi wa ngazi za juu wa Uluguru Academy  inayoinukia kwa kasi mkoani Morogoro   ni John Simkoko na Hussein Ngurungu.

Mwandishi wa Mtandao huu aliishuhudia timu hiyo ya Uluguru Academy akitoa upinzani mkali kwenye michuano ya Azam Sports Federation Cup 2023 iliyotamatika majuzi Uwanja wa Saba saba kwa Tanzanite Academy kutwaa ubingwa baada ya kuinyuka timu ngumu ya Moro Kids 2-1.

Uluguru alitolewa kwenye nusu fainali na Tanzanite kwa kuchapwa bao 2-0.

Kwenye mchezo huo wa Nusu fainali Mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia Vigogo hao wa Uluguru, Hussein Ngurungu, Hamis Malifedha, Marehemu Tumain, Dr Adrew, Ally Jangalu na Bure Mtangwa waliokuwa benchi.

 Simkoko na Mtono hawakuwepo uwanjani japo siku ya mchezo huo.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

”Tangulia Kamanda Tumaini tutaonana baadae”

                           


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...