Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 12, 2023

KIPA ALIYEFUTA MAGORI YA WAZI AMWAGA MACHOZI UWANJANI.

Kipa Mustapher Mrisho akimwaga machozi baada ya mpira kutamatika
Kipa huyo akiendeleakumwaga machozi huku akibembelezwa na viongozi wake.

....Wakati kipa huyo akilia wenzake walishangalia ubingwa
  Mustapher Mrisho bila woga akinyama mpira katikati ya Miguu ya Mshambuliaji wa Moro Kids Bernadct Matora anayeruka juu kumkwepa Kipa huyo.

Mrisho akiruka juu kupangusa mpira wa kona uliokuw aunajaa wavuni
Mrisho akichupa bila mafanikio akiruhusu Moro Kids kupata bao hilo la kufutia machozi.

 



          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Awari ya yote naomba radhi kwa wadau wa Mtandao Pendwa wa Shekidele,juzi niliahidi kurusha hewani matukio ya fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup 2023-24 ngazi ya Wilaya ya Morogoro  iliyotamatika juzi Uwanja wa Saba saba kwa Tanzanite Academy kuibuka mabingwa.

Sisi tunapanga yetu lakini Mungu naye anapanga yake, hivyo juzi tasnia ya Mpira wa Miguu mkoa wa Morogoro tulipatwa na msiba mzito wa kufiwa na mdau mkubwa wa soka Mkoa wa Morogoro kocha Tumaina, hivyo kwa umuhimu wa tukio hilo, jana Mtandao huuu uliweka kando matukio ya fainali hiyo na matukio ya Picha za beki wa Yanga Kibwana Shomari aliyekuwepo kwenye fainali hiyo.

Mtandao huu ukaamua kuwapasha habari wadau juu ya kifo cha Mpendwa wetu huyo aliyeanguka ghafla wakati akifanya mazoezi na timu yake ya Rely Family.

Hebu Piga picha marehemu Tumaini akiwa na afya nyema majira ya jioni anamwambia mkewe amuandalie nguo zake za mazoezini amuwekee kwenye gari.

Baadae Kocha Tumaini anawasha gari lake anatoka nyumbani kwake Kingurunyembe Kata ya Kilakala anaelekea Mazoezini Uwanja wa Shule ya Msingi Mwere, anafika huko katikati ya Mazoezi ananguka ghafla wenzake wanamkimbiza hospital na alipofika alifariki dunia.

Baada ya masaa 2 hivi toka Mpendwa Muwe wake atoke nyumbani Mke anapokea taarifa za kifo cha Mpendwa baba wa watoto wake aliyezimika kama mshumaa, inauma sana aisee.

Marehemu Tumaini amesafirisha jana mchana kuelekea nyumbani kwao Musoka Mkoa wa Mara ambapo leo jioani atapumzisha kwenye nyumba yake ya Milele.

TUREJEE KWENYE MATUKIO  YA FAINALI YA F.A.

Kipa wa mabingwa wapya wa mshindano ya taifa ya Azam Sports Federation Cup timu ya Tanzanite Academy Mustapher Mrisho ambaye kanatajwa kuwa  nyota wa mchezo huo wa fainali kati ya timu yake dhidi ya mahasimu wao wakubwa Moro Kids, akiokoa mabao mengi ya wazi na timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

 Chaajabu baada ya kutamatika kwa mchezo huo Kipa huyo wakati wenzie wakishangilia ubingwa yeye aliangua kilio hali iliyopelekea viongozi wa timu hiyo kubeba jukumu la kumbembeleza.

Mwandishi wa habari hizi  alimfuta na kumuliza kulikoni anamwaga machozi ili hali  amefanya kazi kubwa kuipa ubingwa timu yake, alisema machozi hayo ni yafuraha.

” Gemu ilikuwa tafu sana tunamshukuru Mungu tumeibuka mabingwa kwenye michuano hii mikubwa ambayo huko mbele kuna Neema ya kupata Pesa za Azama na kuonekana kwenye Luninga”alisema Kipa huyo huku jezi yake akirowa machozi hayo ya furaha.

                

 .

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...