Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, October 14, 2023

BEKI YANGA AWAKUMBUKA WALIOMPA MAFANIKIO.

Ticha Majuto kati akiwa na Vijana wake Nikson Kibabage kulia nan a Kibwana Shomari wakati huo wakiwa na umri wa miaka 10.
Ticha majuto akiwa na Kibwana Shomari[kulia] na Kibabage wakati huo wakiwa na umri wa Miaka 17.Picha kwa hizi kwa hisani ya Ticha Majuto.
Kibwana akizungumza na Kocha Majuto juu ya Jukwaa la Uwanja wa Saba saba.
             ....Wakipozi mbele ya kamera za Mtandao huu
Kibwana akizungumza na Viongozi wa Moro Kids Mratibu Mzee Kindagulekati mwenye kanzu’ kulia ni Meneja wa Moro Kids Mussa Miraji

Kinbwa akiwa nyuma ya benchi la Moro Kids akifuatia Afainali hiyo


 


       Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Beki nyota wa timu ya Yanga Kibwana Shomari, baada ya Ligi kusimama kupisha michezo ya kirafiki ya timu ya taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ametumia mwaya huo kurejea nyumbani kwao Morogoro na kuwatembelea watu mbali mbali waliofanikisha mafaniko yake ya Soka.

 Kibwana Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Morogoro aliyejenga Mjengo wake Kihonda, Mwanzo mwa wiki hii alitinga Uwanja wa Saba saba kuisapoti timu yake ya Moro Kids iliyotinga fainali Michuano ya Azam Sports Federation Cup 2023-24.

Mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo Kibwana aliyeketi nyuma ya benchi la Moro Kids kwa muda wote wa dakika 90 alizungumza na Viongozi wa timu ya Moro Kids Mratibu Mkuu  Rajab Kindagule, na Meneja Mussa Miraji.

Kama hiyo haitoshi baada ya kuzungumza na Viongozi hao Kibwana alipanda jukwaani na kuzungumza kwa muda mrefu na kocha wa Moro kids anayefunisha watoto chini ya miaka 10  Ticha Majuto  ambayendiye aliyeibua kipaji cha Kibwana toka akiwa na umri wa miaka 10.

 Kibwana baada ya kuonyesha kipaji kwenye Taasisi hiyo ya Moro Kids inayoongoza nchini kwa kuzalisha wachezaji wengi wanaong’ara kwa sasa Ligi Kuu ya Tanzania Bara alijiungana na Mtibwa B.

Kama hiyo haitoshi beki huyo wa kulia  baada ya kuonyeha kiwango kizuri Uongozi wa Mtibwa ulimpandisha timu ya wakubwa inayoshiriki Ligi kuu.

 Huko nako aliendelea kuonyesha kiwango bora kilichowavutia Viongozi wa Yanga walioamua kumsajiri akiitumikia timu hiyo yenye maskani yake Kariakoo Makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wachezaji nyota wanaotamba kwa sasa ligi kuu walioibuliwa na kituo hicho cha Moro Kids ni pamoja na Kibwana Shomari, Nikson Kibabage, Diksoni Job na Kipa Abuutwalibu Msheri wote wanakipiga Yanga.

Wengine ni Mzamiru Yassin’Simba’ Shiza Kichuya’Namungu’ Hamad Waziri’Kuku’ Singida Fouantain Gate.

                  

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...