Na Mtumishi Dunstan Shekidele,Morogoro.
AMANI ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yenu, ama baada ya salamu moja kwa moja tuingia kwenye ujumbe wetu wa neno la Mungu leo Jumapili ya Octobar 15.
Leo sitanukuu mstali wowote katika biblia bali nitatema nyongo iliyojaa ndani ya moyo wangu kwa dhambi zinazoendelea kufanywa hapa duniani.
Ama kwa hakika Mungu ni Mvumilivu sana hakika kama mimi Dustan Peter Shekidele’D.P.S’ ningekuwa Mungu nisingeweza kuvumilia haya ninayoyaona na kuyasikia hapa duniani.
Utasikia na kuona Mwanaume anajiuza’Shoga’ Mimi ningekuwa Mungu nisingelivumilia hili.
Utamuona Mwanaume baba mtu mzima amepima na kubainika kuwa na virusi vya HIV ‘UKIMWI’anameza dawa za kurefusha Maisha kila siku.
Baba huyo mwenye nyumba anayejijua anagonjwa hilo la hatari ‘Taa ya oil inawake kwenye Bashibord lake’ anamrubuni mfanyakazi wake huyo ’House Girl’ anatembea naye na kumuambukiza maradhi hayo yasio na tiba kwa makusudi akitumia ufukara wa bint huyo tegemo kwa wazazi wake waishio Kijijini.
Mimi ningekuwa Mungu mwanaume huyo ningemuangamiza kabla hajafanya dhambi hiyo.
Tunasikia na kuona Mwanadamu anashonwa tumbo lake kama gunia anasafirisha Madaya ya kule ili awe tajiri, Shekidele ningekuwa Mungu nisingevumilia hili.
Juzi nimesikia kwenye vyombo vya habari Mama kawapeleka mabinti zake Mapacha kwa Mganga wa kienyeji kuwakuza matiti yakue haraka ili waooze kwa wanaume apate mahali.
Masikini ya Mungu mabinti hao wadogo wasio na hatia baada ya kunywa dawa hiyo kwa amri ya Mama yao wote wawili wamefariki duania, mimi ningekuwa Mungu nisingekubali hili.
Pia unasikia kwenye vyombo vya habari mtumishi wa serikali anayelipwa mshahara mnono kwa kodi za walala hoi.
Huyo huyo mtumishi utasikia kala pesa za Ujenzi wa Zahanati ya kijiji zilizotolewa na serikali .
Baada ya mtumishi huyo kutafuna Pesa hizo za ujenzi wa Zahanati,siku chache mbele unasikia Mama Mjamzito Mlala hoi amejifungua njiani na kupoteza maisha baada ya kukosa huduma ya Zahanati kwenye kijiji hicho.
lnauma sana mimi ningekuwa Mungu nisingemvumilia mtumishi huyo wa Serikali aliyepewa dhamana na Rais kusimamia kimanilifu Miradi ya wananchi.
Baada ya kutafakari kwa kina mambo hayo machafu nimebaini Mungu anakusudi jema kwetu,anatupenda watu wake licha ya kumkosea ama kwa kujua ama kwa kutokujua anaendelea kutupa nafasi ya kujitasmina kwa lengo la kujirekebisha na kutubu makosa yetu kabla ya kuingia kaburini ambako huko hatutapata tena nafasi ya kuziungama dhambi zetu.
So Wenye masikio na wasikie wasio na masikio[……]
No comments:
Post a Comment