Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 31, 2023

KUMBUKIZI YA UCHAGUZI MKUU TANZANIA


Hii ni uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa mwaka 2015 Wastara wa Sajuki alijitosa kugombea Ubunge viti Maalumu kwa leseni ya Chama Cha Mpinduzi'CCM' Mkoa wa Morogoro.

Pichani Wastara  akiomba kura kwa wajumbe kwa unyenyekevu mkubwa.

Hata hivyo licha ya Unyenyekevu huo hakufanikiwa kutinga mjengoni Dodoma baada ya kura zake za ndio kuwa chacha huku za hapana zikiwa nyingi kwenye masanduku yake.

 Je Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Mkali huyo wa Bongo Movi atatinga tena kwa wajumbe kuomba kura za kuingia Ujengoni?.

 .


 Mwandishi wa habari hizi akimhoji Wastara

Saturday, July 29, 2023

WAANDISHI WA HABARI MORO WAMFARIJI MH ABOOD.

Mkilanya akimpa mkono wa pole Mh Abood kwa niaba ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro.
Viongozi wa Moro Press Club walipiga Picha ya Pamoja na Mh Abood, kutoka kulia ni Ashton Balaigwa Makamo Mwenyekiti. Thadei Hafigwa. Hilda Singano[Mjumbe kamati ya Utendaji] Ratifa Ganzel Mama wa shughuri za kijamii ambaye ndiye aliyeongoza zoezi la mkeka kwenye Group hilo.

lfahamike Ratifa pia ni Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM, anayefuatia ni Mh Abood wa Mwisho ni Mkilanya.

Mohamed lssa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Tendaji Moro Press Club,akimpa pole bossi wake ukumbukwe lssa ni kaimu meneja wa Abood Media
Mamaa wa Shughuli anayejua kujistili Mh Ratifa Ganzel akimpa pole Mh Abood
                  Hilda Singano naye akimpa Pole Mh Abood
Mratibu Moro Press Club Thadei Hafigwa 'Baba Paroko' akimpa Pole Mh Abood
 


          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Waandishi wa habari mkoani Morogoro leo Julai 29 wamempa mkono wa pole Mlezi wa chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’Morogoro Press Club’ Mh Aziz Abood aliyefiwa na Mama yake mazazi wiki iliyopita.

Mara baada ya kutokea kwa Msiba huo mzito kwa wanafamilia  wa mkoa wa Morogoro,  wanachama wa Moro Press Club walitandika mkeka wa kumchangia mlezi wao huyo kupitia Group la Whatsap.

Hivyo leo  Viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti Nickson Mkilanya walitinga Ofisini kwa Mh Abood na kumpa mkono wa Pole ulioambatana na bahasha ya Rambi rambi za waandishi hao.

 Mh Abooda maybe pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro na Mfanyabiashara Maarufu nchini anayemiliki Viwanda, Mabasi, Malori, Vituo vya Mafuta[Shell] na Vyombo vya bahari, aliwashukuru waandishi hao kwa kumkimnbia kwenye mziba huo mzito wa Mpendwa mama yake.

” Kipekee nawashukuru sana Waandishi wote wa habarikwa moyo wetu wa Upendo na Mshikamono mliouonysha kwenye msiba wa Mpendwa mama yangu.

Nathamini mchango mlioutoa  toka toka na muuguza mama yangu tulikuwa pamoja mpaka kifo chake, nitafikisha salama hizi kwa familia yangu pia nitaendelea kushirikiana na Waandishi wote wa habari wa Mkoa wa Morogoro”alisema Mh Abood  

                              

  

Thursday, July 27, 2023

KUMBUKIZI.,MH ABOOD KUKUTANA NA VIONGOZI WA CHADEMA

 

Upinzania sio Uadui,Mbunge wa Jimbo la Morogoro kwa leseni ya Chama Cha Mapinduzi[CCM]Jimbo la Morogoro kwa Zaidi ya miaka 15 mfurulizo Mh Aziz Abood[kulia aliyeweka mkono mfukoni] akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo[[CHADEMA] Mkoa wa Morogoro.

Viongozi hao vya Vyama Vikuu vya Upinzania nchini walinaswa na kamera za Mtandao huu Miaka 9 iliyopita wakiteta jambo baada ya kukutana kwenye  Msiba wa  Mtu Maarufu Mkoa wa Morogoro.

Pichani nawakumbuka viongozi wawili wa Chadema waliovaa  flana za mistaristari, Mh Juma Tembo aliyekuwa Diwani wa Kata ya Tungi kwa leseni ya Chadema[Wakati anayezungumza na Mh Abood] na anayemfuatia kushoto ni Omar Mvambo Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema[BAZECHA] Mkoa wa Morogoro.

Picha na Dustan Shekidele Morogoro.

Tuesday, July 25, 2023

KUMBUKIZI

Watoto hao wakiwa hospitarini hapo  siku chache baada ya kuzaliwa.

 Mwandishi wa Mtandao huu [kulia] akizungumza na mmoja wawananchi wa kijiji cha Berega nje ya hospital ya kijiji hicho.


 Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Tukio hili la watoto mapacha wote  jinsi ya kike kuzaliwa huku wakiungana miili yao limetokea Julai 21-2017 katika hospital ya Misheni ya Berega Wilaya ya  Gairo Mkoa wa Morogoro.

 

 

 

Baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa  wawananchi wa Kijiji  hicho kilichopo takribani kilometa 15 kutoka Makao makuu ya Wilaya ya Gairo, Mwandishi wa habari hizi alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi kutoka Morogoro Mjini hadi kijijini hapo na kufanikiwa kuwaona watoto hao sambamba na kuzungumza na baba yao Lucas Chomolo.

 

Akizungumza na Mtandao huu Chamola alisema mkewe Bi. Rebecca Mwendi[42] alijifungua kwa njia ya upasuaji mapacha hao  wakiwa wameungana kifua na tumbo huku akiiomba Serikali kumsaidi gharama za kuwatenganisha.

Serikali ya Tanzania ni sikivu llisikia ombi la Mzazi huyo na kubeba jukumu la kumsaidia kwa kuwahamishia watoto hao kwenye hospital kubwa na kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.

Hadi leo Julai 25-2023 ni miaka 6 imepita toka watoto hao watenganishwe,hivyo kwa kuwa nilikuwa Mwandishi wa habari wa kwanza kuripoti tukio hilo kwenye Magazeti ya Global Publishers.

 Siku mbili hizi najitafuta nikifanikiwa kupata Pesa ya mafuta ya Pikipiki nitaelekea kijijini hapo kujua maendeleo yao.

Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kwa mwendelezo wa habari hii ya kijamii zaidi.

                     


 

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...