Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 29, 2023

WAANDISHI WA HABARI MORO WAMFARIJI MH ABOOD.

Mkilanya akimpa mkono wa pole Mh Abood kwa niaba ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro.
Viongozi wa Moro Press Club walipiga Picha ya Pamoja na Mh Abood, kutoka kulia ni Ashton Balaigwa Makamo Mwenyekiti. Thadei Hafigwa. Hilda Singano[Mjumbe kamati ya Utendaji] Ratifa Ganzel Mama wa shughuri za kijamii ambaye ndiye aliyeongoza zoezi la mkeka kwenye Group hilo.

lfahamike Ratifa pia ni Diwani wa Viti Maalumu kwa leseni ya CCM, anayefuatia ni Mh Abood wa Mwisho ni Mkilanya.

Mohamed lssa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Tendaji Moro Press Club,akimpa pole bossi wake ukumbukwe lssa ni kaimu meneja wa Abood Media
Mamaa wa Shughuli anayejua kujistili Mh Ratifa Ganzel akimpa pole Mh Abood
                  Hilda Singano naye akimpa Pole Mh Abood
Mratibu Moro Press Club Thadei Hafigwa 'Baba Paroko' akimpa Pole Mh Abood
 


          Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Waandishi wa habari mkoani Morogoro leo Julai 29 wamempa mkono wa pole Mlezi wa chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro’Morogoro Press Club’ Mh Aziz Abood aliyefiwa na Mama yake mazazi wiki iliyopita.

Mara baada ya kutokea kwa Msiba huo mzito kwa wanafamilia  wa mkoa wa Morogoro,  wanachama wa Moro Press Club walitandika mkeka wa kumchangia mlezi wao huyo kupitia Group la Whatsap.

Hivyo leo  Viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti Nickson Mkilanya walitinga Ofisini kwa Mh Abood na kumpa mkono wa Pole ulioambatana na bahasha ya Rambi rambi za waandishi hao.

 Mh Abooda maybe pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro na Mfanyabiashara Maarufu nchini anayemiliki Viwanda, Mabasi, Malori, Vituo vya Mafuta[Shell] na Vyombo vya bahari, aliwashukuru waandishi hao kwa kumkimnbia kwenye mziba huo mzito wa Mpendwa mama yake.

” Kipekee nawashukuru sana Waandishi wote wa habarikwa moyo wetu wa Upendo na Mshikamono mliouonysha kwenye msiba wa Mpendwa mama yangu.

Nathamini mchango mlioutoa  toka toka na muuguza mama yangu tulikuwa pamoja mpaka kifo chake, nitafikisha salama hizi kwa familia yangu pia nitaendelea kushirikiana na Waandishi wote wa habari wa Mkoa wa Morogoro”alisema Mh Abood  

                              

  

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...