Mwandishi wa Mtandao huu [kulia] akizungumza na mmoja wawananchi wa kijiji cha Berega nje ya hospital ya kijiji hicho.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
Tukio hili la watoto mapacha wote jinsi ya kike kuzaliwa huku wakiungana miili yao limetokea Julai 21-2017 katika hospital ya Misheni ya Berega Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro.
Baada ya kupokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa wawananchi wa Kijiji hicho kilichopo takribani kilometa 15 kutoka Makao makuu ya Wilaya ya Gairo, Mwandishi wa habari hizi alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi kutoka Morogoro Mjini hadi kijijini hapo na kufanikiwa kuwaona watoto hao sambamba na kuzungumza na baba yao Lucas Chomolo.
Akizungumza na Mtandao huu Chamola alisema mkewe Bi. Rebecca Mwendi[42] alijifungua kwa njia ya upasuaji mapacha hao wakiwa wameungana kifua na tumbo huku akiiomba Serikali kumsaidi gharama za kuwatenganisha.
Serikali ya Tanzania ni sikivu llisikia ombi la Mzazi huyo na kubeba jukumu la kumsaidia kwa kuwahamishia watoto hao kwenye hospital kubwa na kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa.
Hadi leo Julai 25-2023 ni miaka 6 imepita toka watoto hao watenganishwe,hivyo kwa kuwa nilikuwa Mwandishi wa habari wa kwanza kuripoti tukio hilo kwenye Magazeti ya Global Publishers.
Siku mbili hizi najitafuta nikifanikiwa kupata Pesa ya mafuta ya Pikipiki nitaelekea kijijini hapo kujua maendeleo yao.
Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kwa mwendelezo wa habari hii ya kijamii zaidi.
No comments:
Post a Comment