Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, June 11, 2023

UJUMBE WA NENO LA MUNGU. POMBE IMETAJWA MARA NYINGI KWENYE SOMO HILI.

Mama mwenye mtoto mgongoni alinaswa na Mpiga Picha wa Mtandao huu kwenye msitu mnene akijaza upepo baada ya baiskeri aliyosafiria kutoka Kilosa kuelekea Kimamba kupata Pancha kwenye Msitu huo,

Wenye uhitaji hapa kwenye Tanzania Wako wengi hivyo tuwasaidie.

 Pichani Mwandishi wa Mtandao huu alimnasa Mama huyo aliyekuwa na mwanae akichota maji machafu ya Mvua yaliyotuhama kando kando ya barabara kuu ya Morogoro -Dodoma eneo la Wami Dakawa Wilaya ya Mvomeo akienda kuyatumia nyumbani wake. 

Kushoto ni Pikipiki ya mwendokasi ya Mpiga Picha wa Mtandao huu.

 


SOMO.

MAFUNDISHO YA MAMA WA MFALME LAMUELI.

  MITHALI 31. 2-9.

 Mstari huu wa Pili mama anamuliza mwanae akisema.

[2]”Ni nini Mwanangu?.Tena ni nini Mwana wa tumbo langu? Tena ni nini Mwana wa Nadhiri zangu?. Mstari wa tatu anampa maagizo

[3]“Usiwape wanawake nguvu zako,wala Moyo wako usiwape wale wawaharibu wafalme”.

[4]“Ee Lamueli kunywa mvinyo hakuwafai  wafalme hakuwafai wafalme,Wala haifai wakuu waseme kiwapi kileo?

’lt is not for Kings O Lamueli,lt is  not  Kings  to  drink  wine, not for  Princes  strong drink’

kwenye mstsri huu wa 4 MUNGU ameweke msisitizo mara mbili mbili na mimi nimeweke msisitizo kwa lugha zote mbili za kiswahiri na kingereza.  

Mstari wa 5 anatoa angaliza

[5]“Wasije wakanywa na kuisahau sheria na kuipotosha hukumu ya Mtu aliye taabuni.

 Kweli maneno ya Mungu yanahitaji utulivu mkubwa kwenye kuyasoma na kuyatafsiri sikilia Mstari wa 6 unavyosema.

“Mpe kileo yeye aliye karibu na Uchungu.  kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini”. Mstari wa 7 unakadhia hilo ukisema hivi.

” Anywe  akausahau umasikini wake Asikumbuke tena taabu zake.  

Mstari wa 8 unamaneno ya faraja

”Fumbua Kinywa  chako kwa ajili yake aliye bubu, Uwatete watu wote walioachwa peke yao”.

Tunahitimisha somo letu na mstari wa 9 ukitoa maelekezo kwa wenye mamlaka ya kuhukumu na utoaji.

”Fumbua Kinywa chako hukumu kwa haki.

Uwapatie Masikini na wahitaji haki yao.” Hilo ndilo neno letu ya leo Jumapili ya June 6.

Takribani miezi 2 sikuwa hewani kwenye somo hili la Jumapili hii ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu lakini kwa Neema ya Mungu amezitatua na kazi yake inaendelea sasa.

             

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...