Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, June 13, 2023

MORO VETERAN YAIBANIA T.R.A DAR.

Kikosi ncha TRA Dar kikipigwa picha na kocha wao Hiza ambaye ndiye aliyempa tenda Mpiga Picha wa Mtandao huu kupiga Picha matukio yote ya timu hiyo.

                          Kikosi kabambe cha Moro Veterani



Mshambuliaji hatari wa TRA Dar akiwatoka kwa kasi ya ajabu mabeki wawili wa Moro Vieterani,


Winga huyo kafanikiwa kuwaacha mbali mabiki hao akiendelea na safari zake
             Beki wa Moro Veterani akimthibiti winga wa TRA

              ....Beki huyo akizidi kumbana winga huyo
Huyu hachezi Sebene   ni mshambuliaji hatari wa Moro Veterani Shabibu Mohamed' Chinga Boy'akisaka mbinu za komtoka beki wa TRA,
Chinga ambaye ni Askali Polisi wa Kikosi cha Usalama barabarani akizidi  kupiga hesabu za kumtoka kigogo huyo wa TRA
Mshambuliaji Chinga akijianadaa kupiga mkwaju wa Pelnati ambapo alikosa baada ya shuti lake kali kugonga Mwamba wa chini  na kuokolewa na mabeki wa TRA
,Mwamuzi akimpa maelekezo wa Kipa kabla ya mkwaju huo wa Pelnati kupigwa

 Chinga aking'ata kidole kwa uchungu baada ya kukosa pelnat. huku kipa wa TRA Dar akifurahia


             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU Kabambe ya Moro Veterani Wiki end iliyopita imewabania timu ya watoza kodi ‘TRA’kutoka Dar baada ya kutoka sale kwenye miche 2 iliyopigwa Jumamosi jioni na ya pili ikipigwa jumapili asubuhi.

Michezo hiyo ya kirafiki iliyojaa upinzani mkali, kufuatia ubora wa viwango vya wachezaji wa timu zote mbili imepigwa  viwanja 2 tofauti.

Gemu ya kwanza iliyotamatika kwa sale ya bao 1-1 imepigwa Uwanja wa Jamhuri, huku gemu ya pili iliyopigwa  Uwanja wa Shujaa ikitamatika pia kwa sale ya 0-0.

 Kwenye gemu ya Jumamosi Watoza kodi hao waliofunga safari kutoka Jiji la Maraha[Dar-es –salaam]walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza huku Moro Veterani wakisawazisha bao hilo dakika 75 kwa bao safi lililofungwa na Mshambuliaji hatari Shahibu Mohamed[Chinga Boy].

Lengo la Michezo hiyo ni kukuza Ujirani Mwema, kupeana Michongo ya kimaisha lakini kubwa zaidi  kuimalisha afya za wachezaji wa timu hizo akiwemo Mwandishi wa Mtandao huu anayekipiga Moro Veterani.

Kufuatia ukali wa mshambuliaji Shekidele Vigogo wa TRA waliamua kutumia zile mbinu zao za ukusanyaji kodi ambapo waliamua kumvuta pembeni na kumpa tenda ya kupiga Picha matukiyo yote ya Uwanjani.

Baada ya kushikishwa Posho nzuri ya kazi hiyo Shekidele alivua jezi za Moro Veterani akavaa kamera  akaingia mzigoni,kufuatia hali hiyo baadhi ya wachezaji wenzie walimtupia lawama za usaliti

Shekidele aliwajibu kwa kuwapa mfano huu kwamba  Mke na kazi bora nini?.Wachezaji wa veteran waliangua vicheko huku wakigawanyika kujibu wangine walidai bora kazi na wengine wakadai bora mke.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...