Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, June 10, 2023

FUNDI WA MPIRA PETER TINNO AIBUKIA MORO KIDS.

Peter Tinno mpachiba bao wa zamani wa soka la Tanzania
...Tinno akitambulishwa na Prof Mdundo Mtambo

 


Na Dustan Shekidele,Morogoro. 

Mshambuliaji hatari aliyewahi kutamba  akiwa na timu ya Pan Afrika na timu ya Taifa ya Tanzania’Taifa Stars’ Peter Tinno hivi karibuni ameibukia kwenye Taasisi ya kukuza na kuibua Vipaji ya Moro Kids ya Mkoa hapa.

Mkongwe huyo Mkazi ya Kigurunyembe Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro alitikisa soka la Tanzania Miaka ya 80 kuelelea 90  akifunga mabao atakavyo kama ilivyo sasa kwa Mkongo Man Fiston  Mayele’ Mzee wa Mitetemo.’

 Hivi karibuni Tinno aliibuka kwenye kumbukizi ya Miaka 25 ya taasisi ya Moro Kids na kutambulishwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Profesa Madundo Mtambo ambaye pia ni mshambuliaji hatari wa zamani wa timu ya Reli ya Morogoro aliyezofunga apendavyo timu za Simba na Yanga.


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...