Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 7, 2023

SOMO LA MAHABARA LEO LINAANGUKIA KWENYE UGUMBA.

Mwandishi wa hadithi hii akizungumza na  Askofu wa KKKT Jacob Ole Mameo

  Akizungumza pia na Askofu wa kanisa Katoliki Telephfori Mkude.


           Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Mpendwa msomaji wa Blog Pendwa ya Shekidele nawasalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wasomaji wangu wote  duniani  hasa wale wa Marekani, Uingereza, Uarabuni,China Kenya, Uganda na nyumbani Tanzania.

Ama baada ya salamu ambazo Mitume wote wa Mwenyezi Mungu wanasema wanaosaliminana wana Kheri kwa Mwenuzi Mungu.

Some letu la leo linajikita kwenye ugumba.

Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa Mwaka mmoja [miezi 12] na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.

 Hii imezihilika kwa wanandoa wanapofunga ndoa baada ya mwaka mmoja wakijaliwa kupata mtoto ndugu na majirani husikika wakisema ndoa ya wawili hao imejibu.

 Katika hali hiyo hiyo ikifika mwaka wanandoa hao hawajajaliwa kupata mtoto Vikao vya ‘Wambeya’  vinaanza kwa Majirani na ndugu hasa mawifi na mashemeji.

 Uzoefu unaonyesha inapotokea hali hii kwa wanandoa  mara nyingi ndugu na Mwanaumu hasa mawifi  wakiongozwa na majirani kwa pamoja humtupia zigo la lawama Mwanamke  wakimwita Mgumba na kumshawisha ndugu yao kumpa talaka Mwanamke huyo kwa hoja kwamba anakula ugari wa bure hana faida kwenye familia ni sawa na mti usio zaa matunda unakazi ya majani yake kuchafua uwanja bila faida yoyote.

Huku wakimwacha kaka yao ambaye kiuhalisi huenda yeye ndiye Mgumba huku mtoto wawatu wanayemsimanga  si mgumba.

KIIMANI VIONGOZI WA DINI WANASEMAJE KUHUSU SWALA HILI.

Katika kazi yangu ya Upigaji Picha nimefanikiwa kupiga Picha kwenye harusi nyingi za kiislam, Kikristo na zile bomani[Kwa Mkuu wa Wilaya.]

 Kwenye harusi hizo zote hakuna mfungisha ndoa yoyote aliyewaambia Maharusi kwamba mmoja wao akiwa mgumba ndoa hiyo inavunjika.

Zaidi Viongozi hao Mashehe kwenye mawaidha yao baada ya kufungisha ndoa huwapa nasaha wanandoa hao kwamba ndoa ni lazima kwa maelekezo ya Mwenyezi Mungu lakini kupata watoto sio lazima  ni bahati hivyo isitokee kwa namna yoyote mkasimangana au kupeana talaka kwa sababu hamkupata mtoto kwenye ndoa.

Kwa upande wa wakristo ni hivyo hivyo Maaskofu, Wachungaji na Mapadri wanapofundisha ndoa, kwenye Mahubiri yao pia husema ndoa ni agizo la Mungu  na watoto ni Neema kutoka kwa Mungu.

”Ndoa hii imefungwa na Mungu, na anayeweza kuivunja ni Mungu mwenyewe kwa  mmoja wetu atakapofariki dunia, hivyo ndoa hii iheshimiwe na watu wote wakiwemo wazazi na wanandoa wenyewe hakuna mwenye haki ya kuivunja,alichokiunganisha Mungu Mwanadamu awaye yote asikitenganishe kwa sababu yoyote ile” hicho ndicho kiapo cha ndoa kwa wakristo.

Kwenye kiapo hicho na mimi naongezea toa hiyo inaweza kuvunjika kwa uzinzi uliothibishwa

Baadhi ya watu wengine waliokemea tatizo hilo la unyanyapaa wa Ugumba kwa njia ya Sanaa ya nyimbo ni Mwanamuziki Mkongwe nchini Muumini Mwijua ‘Kocha wa Dunia’

Kuna aina mbili za ugumba;

Ugumba wa asili (Primary Infertility) – Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutungisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary Infertility) – Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.

 

Asilimia 20-30 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.

 Kwa leo naishi hapa kwa ushauri, maoni au pongezi tuwasiliane kwa namba 0715 28 90 73.

 Mada ya wiki ijayo ni somo la njia sahihi za kudumisha mahusiano’Mapenzi  ya mbali’mfano kwa sababu za kazi au masomo  wapenzi au wanandoa wanaishi mbali mbali.                             

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...