Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 7, 2023

PAPA FRANSISKO AMTEUA PADRE KIANGIO KUWA ASKOFU WA JIMBO LA TANGA AKICHUKUA NAFASI YA HAYATI ASKOFU BANZI.





 Baba Mtakatifu Fransisko amemteua Padre Thomas John Kiangio[Pichani] kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa Kwa Vyombo vya Habari na Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)Padre Charles Kitima ime eleza kuwa uteuzi huo umefanyika Leo June 7,2023.
Askofu mteule Thomas John Kiangio, alizaliwa Machi 17, 1965 huko Mazinde Ngua, Jimbo Katoliki la Tanga.

Alipata malezi na majiundo yake ya Kipadre kutoka Seminari kuu ya Mtakatifu Antony wa Padua Ntungamano iliyopo Jimbo Katoliki la Bukoba na Seminari Kuu ya Mt. Karoli Lwanga, Segerea Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.

Mnamo Julai 16, 1997 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki la Tanga.

Tangu wakati huo, alihudumu pamoja na kutekeleza utume wake kama Paroko-usu, Parokia ya Lushoto mwaka 1997-1998.

Baadaye akateuliwa kuwa mlezi, mwalimu na Gambera Msaidizi na hatimaye Gambera wa Seminari Ndogo ya Mtakatifu Yosefu Soni, Tanga kati ya mwaka 1998-1999 na kati ya mwaka 2004 hadi mwaka 2013.

Mwaka 1999 hadi mwaka 2003 alitumwa kuendelea na masomo ya juu Chuo kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichopo mjini Roma.
Mwaka 2013 aliteuliwa kuwa Katibu wa Jimbo hadi kuteuliwa kwake kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Tanga kufuatia kifo cha Askofu Anthony Mathias Banzi aliyefariki dunia Desemba 20-2020.

lfahamike hayati Askofu Banzi alikuwa Mluguru Mzaliwa Tawa Matombo Wilaya ya Morogoro.Vijijini

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...