Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 5, 2023

BALOZI WA MAZINGIRA ASHIRIKI KUPANDA MITI SHULE YA MSINGI MORO.

Balozi Chege[kati] akishiriki kupanda moja ya Miti hiyo kwa kusaidiana na  wasaidizi wake Sophi kushoto mwenye rasta na Caroryni kulia.

                           ...Wakishangilia
                Mmoja wawalimu wakipanda miti
                Mgeni Rasmi Balozi Chege akizungumza
                             Walimu wakipanda miti
                Mkuu wa shule Peter Mahongo akipanda mti


Michezo hiyo imeendelea mpaka kwenye safari ya kwenda kunywa chai, ambapo kuligawanywa mistari miwili ya mashabiki wa Simba waliofungwa  Kamba nyekundu na wa Yanga waliofungwa Kamba nyeupe.

Mashabiki wa Yanga waliongozwa na Mkuu wa shule waliibuka washindi  baada ya kuwaacha mbali mashabiki wa Simba waliongozwa na Balozi Chege.





 Heshima imechukua mkondo wake Mgeni rasm na ujumbe wake licha ya kushindwa kwenye mbip hizo lakini wamekuwa wa kwanza kuchukua chai


                              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

BALOZI wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamo wa Rais Chege Alex Chege, juzi ameshiriki kupanda miti eneo la shule ya Msingi ya ‘Morogoro Bapitist Academy’iliyopo Mtaa wa Area Six Nane Nane Mkoani hapa.

Balozi huyo aliyeambatana na Malkia wa Mazingira Sophia Kalinga na IRONIC, Carolyni Masuka kwa kushirikiana na Walimu wa shule hiyo kwa pamoja wamepanda Miti 30 kwenye eneo la shule hiyo inayomilikiwa na Wamarekani wawili Mume na mkewe.

 Akizungumza kabla ya kupanda Miti hiyo Balozi Chege amesema lengo ya serikali ya awamu wa 6 inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imejikita kupanda miti zaidi ya milioni 30 kote nchini.

“ Kwa niaba ya Waziri wa Mazingira Mh Seleman Javu nipongeze shule hii kwa kuendelea kupanda miti kwenye eneo lenu,nakumbuka hii ni mara ya pili na kuja hapa kupanda Miti.

 Mara ya kwanza tulipanda miti ile pale naiona  inaendelea kustawi vizuri nawapongeza kwa kuitunza kuna baadhi ya maeneo tunapanda miti haitunzwi siku ikitembelea eneo hilo inakuta yote imekufa”alisema Balozi huyo na kuongeza.

 

 “ Miti hii 30 na ile tuliyoipanda siku za nyuma yote tutaingiza kwenye ldadi ya Miti hiyo inayotakiwa kupandwa nchi nzima”alimalizia kusema Balozi Chege.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Peter Mahongo alisema baada ya shule kufungwa, Uongozi umeamua kuanda tamasha kwa Walimu wote  kwa lengo la kuweka miili yao sawa.

Mahongo aliitaja michezo hiyo kuwa ni pamoja na Soka, Netball, Riadha na Michezo ya kuruka Vijiti.

”Baada ya walimu wetu kufanya kazi kubwa ya kuwafundisha wanafunzi leo tumeamua kuwaandalia Event, hivyo kabla ya kuanza kwa michezo hiyo tumeamua kupanda miti kwenye eneo letu la shule tukiunga mkono juu za serikali za kupanda miti”alisema Mkuu huyo wa shule. 

Mpiga Picha Maarufu wa Mtandao huu anayemiliki kamera za kisasa ndiye aliyepewa tenda na Uongozi wa shule hiyo kupiga Picha matukio yote

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...