Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, May 10, 2023

POLISI MORO WAFANIKIWA KUWAZUIA WANANCHI WALIOKUWA NA SHAUKU YA KUMSHIKA MKONO TUNDU LISSU.







 


               Dunstan Shekidele,Morogoro.

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuthibiti kundi la wananchi waliokuwa na shauku ya kumshika mkono Mwanasiasi Maarufu duniani Tundu Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa.

 

 Tukio hilo lililonaswa Live bila chenga na Mwandishi wa Mtandao huu limetokea jumapili kwenye Viwanja vya shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoani hapa ambapo chama hicho kilifanya mkutano wa hadhara.

 

Baada ya mkutano huo uliojaza umati mkubwa wawatu kutamatika majira ya saa 12 jioni,  Mh Lissu  alisaidiwa  kushuka jukwaani na Mabaunsa kufuatia matatizo yake ya Mguu,.

Alipotua chini na kuachiwa na mabausan hao Lissu alisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee’BAZECHA’Mkoa wa Morogoro, Omari Mvambo.

Wakati akisalimiana na Mzee Mvambo  kundi la wananchi lilivamia eneo hilo wakigombea kusalimiana na Lissu.

 

Baada ya kuona hivyo Polisi waliokuwa wakilinda Mkutano huo walivamia eneo hilo na kuwazuia wananchi hao kumsogelea Mwanasiasa huyo.

 

 Kwa upendo wathati kwa mashabiki wake Lissu baada ya kuingai kwenye gari lake la kifahari Toyota ‘Shangingi’ V8 alichomoza juu ya gari hilo na kuwasalimia wananchi hao kwa ishara ya kuwapungia mkono.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Lissu alifanikiwa kushinda Ubunge kwenye moja ya majimbo ya Mkoa wa Singida na mwaka 2017 wakati akitoka kwenye Vikao vya Bunge jijini Dodoma akirejea nyumbani  alivamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa Risasi nyingi sehemu mbali mbali za mwili wake.

 

Akiwa kwenye matibabu nchini Ubelgiji alivuliwa Ubunge kwa madai ya Utoro Bungeni.

 Siku chache baada ya shambulio hilo kiongozi pekee wa awamu ya 5 aliyekwenda hospital nchini Kenya kumjulia hali Tundu Lissu alikuwa Makamu wa Rais Mh Samia Suluhu Hassan. Kama hiyo haitoshi Rais wa awamu 6 Mh Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine tena alifunga safari mpaka nchini Ubelgiji kumjilia hali Tundu Lissu.

 

Pia Mh Rais Maarufu Mama Samia aliamua Lissu kulipwa haki zake zote za Ubunge.

Kwenye eneo hilo  Mwandishi wa Mtandao huu kutoka ndani kabisa ya sakafu ya moyo wake  anatamka kwamba kwenye hilo Mama Samia kaupiga mwingi duniani mpaka mbinguni.

Licha ya madaktari kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha yake lakini bado hali ya miguu  haijatengemaa vizuri hivyo kwenye maeneo kama hayo ya minuko anahitaji msaada.

 Tunasema ni Mwanasiasa maarufu dunia kwa vigezo kwamba baada ya kukumbwana tukio hilo Vyombo mbali mbali vya habari duniani vilimtafuta Lissu na kufanya naye mahojiano ikiwemo vituo vikubwa vya redio Dunia  kutoka nchini kubwa dunia za Uingereza, Ujerumani na Marekani.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...