Mh Tundu Lissu kushoto[Makamu mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Moza Ally[kati] na Devotha Minja wakipokea maombi kutoka kwa Askofu Mdee juzi
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Askofu Mdee ameshusha maombi mazito kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo[CHADEMA’uliofanyika juzi kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoani hapa.
Mkutano huo ulioanza majira ya saa 8 mchana na kutamatika saa 12 jioni umehudhuriwa na Viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Makamu mwenye kiti wa Chadema Taifa Mh Tundu Lissu ‘Mzee wa Ubelgiji’ Makamu Mwenyekiti wa ‘BAWACHA’ Taifa Bi. Moza Ally, na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Taifa Mh Peter Msigwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa kanda ya Nyasa.
Wengine walioshuhudiwa na Mwandishi wa habari hizi ni Viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho Mkoani Morogoro, wakiongozwa na Devotha Minja aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu akiwakilisha Mkoa wa Morogoro.
Kwenye mkutano huo Mh Tundu Lissu aliendelea kuhamasisha wananchi kudai katiba Mpya kabla ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Taarifa zilizopatika kwenye Mkuatno huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wawatu zilidai Chadema wataendelea na mikutano ya hadhara kwenye maeneo mbali mbali ndani ya jimbo la Morogoro.
ljumaa watafanya mkutano Kihonda Manyuki, Jumamosi watafanya mkutano Kata ya Lukobe na Jumapili watafanya mkutano Tubuyu Kata ya Tungi.
Baada ya Tundu Lissu kuhitimisha kwa kuwamwagia madini ya maana umati huo wawatu, mjira ya saa 12 jioni Askofu Mdee aliyewahi kuwa Askofu wa kanisa la Kabobe lililopo Mafika makoani hapa, kabla ya kutimka kwenye kanisa hilo na kuanzishi kanisa lake Tubuyu Kata ya Tungi alifunga mkutano huo kwa maombi mazito yaliyopokelekwa mikono miwili na Mh Tundu Lissu.
Baada ya Mh Tundu Lisu kushuka jukwaani huku akisaidiwa na mabausa kufuatia hali ya mguu wake uliojeruhiwa kwa risasi wakati akitoka kwenye kikao cha bunge mwaka 2017 kutotengemaa vizuri,kundi la wananchi walimvamia kwa upendo wakitaka kumshika mkono.
Hata hivyo maaskari waliokuwa wakilinda usalama kwenye mkutano huo walifanikiwa kuwadhibiti wananchi wasimsongelea mwanasiasa huyo mashuhuri Duniani ambaye kitaaluma ni Mwansheria.
Picha za matukio hayo zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment