ANZIA.
Taifa la watanzania leo limegubikwa na simani kwa kifo cha Mwamba huyu Mwanasiasa maarufu nchi mwenye misimamo Mh Bernard Membe.
Nakumbuka moja ya misimamo yake kwenye utawara wa awamu ya 5 aliingia matatani yeye na wakwengwe wenzie wawili wa siasa nchini.
Baadae watatu hao walipewa masharti ya kuomba radhi ili wasamehewe.
Wenzie wawili waliomba radhi na kusamahewe laki yeye alishikilia msimamo wake huku akisema
”Bora nife nimesimama kuliko kufa huku nimechutama nampigia mtu magoti”
Binafsi nilikuwa shabiki wako mkubwa kwenye maswala ya Siasa huku ukiniachia somo la Misamamo yako.
Wenzie walioomba radhi walirejeswah kwenye chama chao cha CCM huku Membe aliyegoma kuomba radhi akitimuliwa kwenye chama hicho tawara nchini.
Baada ya kufukuzwa Mh Membe alijiunga na chama cha ACT Wazalendo cha Zito Kambwe na kuteuliwa kugombea Urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ambapo kura hazikutosha, huku mgombea urais kupitia CCM kipenzi cha wengi hayati John Pombe Magufuli akiibuka kidedea kwa kura nyingi akiwapiga kumbo wapinzani wake.
Tangulia kamanda tutaonana baadae, sisi tulikupenda lakini Mungu amekupenda Zaidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe sote tuseme ameni.
No comments:
Post a Comment