Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
TIMU ya Efm Fc inayomilikiwa na Taasisi ya Efm Media yenye maskani yake Mbezi Beach jijini Dar es salaam, Mwishoni mwa wiki imeifunga kwa hira timu ngumu ya Moro Veterani kwa bao 3-0.
Timu hiyo ya Efm imekiuka makubaliano ya mchezo huo wa kirafiki uliopigwa juzi jumamosi uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.
Makubaliano yalikuwa ni wachezaji wa kiveterani[Watu wazima wanaocheza kwa kujifurahisha kwa lengo la kuweka sawa afya zao ] na sio kuleta wachezaji chimbukizi [Watoto] wanaotafuta mafanikio kwenye mchezo huo wa soka.
Chaajabu kikosi hicho cha Efm kilipowasili kwenye uwanja huo watulishangazwa kushuhudia timu hiyo ikiwa na maluki wachezaji wengi Vijana wengi wao wakiwa na umri chini ya miaka 25[Under 25] kama wanavyoonekana pichani.
Kwenye kikiso hicho cha Efm mtu mzima alikuwa mmoja tu mkuu wa vipindi vya Efm Radio na Efm Tv Senior Sembo[wa mwisho kulia waliosimama.
Jambo hilo lilizua manung’uniko kutoka kwa wachezaji, Viongozi na Mashabiki wa Moro Veterani akiwemo kaimu Afisa habari wa Moro Veterani Dustan Shekidele’Mkude Simba.’
Manung’uniko hayo yalivuma na kuwafikia Viongozi wa Efm Wakiongozwa na Big Bos Madizo waliofunga mziki Mneno uwanjani hapo na kurusha live matangazo ya Mpira huo kwa muda wote wa dakika 90.
Katika hali ya kijitetea wakijibu manung’uniko hayo Mtangazaji wa Mpira huo Rashid a.k.a Mgunduzi wa Off Side alisema.
” Taasisi ya Efm inavitengo vingi vinavyoongozwa na Vijana hivyo wachezaji wote hao wanatoka kwenye taasisi yetu”alisikika mtangazaji huo akiitetea taasisi yake.
Chaajabu licha ya utavauti huo wa wachezaji bado Moro Veterani waliwapigia mpira mwingi Efm akiasi cha Nahodha wa timu ya Efm Ssembo kumvamia refa na kumkalipia akililia pelnati kama anavyoonekana pichani.
Sababu nyingine iliyopelekea Moro Veterani kufungwa na timu hiyo dhaifu ya Efm, siku 1 kabla ya mchezo huo Moro Veterani walipata msiba wa kufiwa na mchezaji wao Salum Kondo ambaye pia alikuwa mchezaji wa timu ya Ligi kuu ya Polisi Tanzania kabla ya kutemwa na timu hiyo na kujiunga na Moro Veterani.
Hayati Kondo ambaye pia alikuwa Askari Polisi tumlizika kijini kwao Kauzeni Nnje kidogo ya Mji wa Morogoro na mazishi hayo yaliongozwa na rais wa TFF Taifa Wales Karia.
Baada ya kutoka kwenye mzishi hayo majira ya saa 10 jioni moja kwa moja tuliingia uwanja wa Saba saba na kuwashuhudia wapinzani wetu wakiwa uwanjani hapo toka majira ya saa 9 Alasiri akifanya hom-Up.
Hivyo kwa sababau hizo mbili nikiwa kama Afisa habari wa Moro Veterani nawaambia Efm wasijitape kuwafunga Morogoro Veterani bali wajitathmini kwa kukiuka makubariano.
Kwa leo nimeamua kuwachana Live Efm Picha zaidi za Matukio ya uwanjani zitaruka hewani hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment