Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, May 16, 2023

ADAM MALIMA MKUU WA MKOA MPYA WA MOROGORO


 


 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Rais Dk Samia Suluhu Hassam.’SSH’Jana amefanya mabadiliko ya wakuu wa Mikoa ambapo aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Adam Malima[Pichani] amehamishiwa Mkoa wa Morogoro, huku aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Fatma Mwassa akihamishiwa Mkoa wa Kagera.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkowa wa Kagera Mh Alberth Chalamila yeye amehamishiwa Mkoa wa Dar es salaam akichukua nafasi ya Amos Makalla aliyehamishiwa Mwanza akichukua nafasi ya Malim.

Mtandao huu unamkaribisha kwa mikono miwili Jembe Adam Malima ambaye pia rekodi zinaonyesha ni mtu wa michezo hivyo ujio wake hapa Morogoro tunaamini atafufua mchezo pendwa wa soka uliodidimia kwa miaka ya hivi karibu na kuendelea mchezo wa ngumi unazidi kuchanua mkoani hapa.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...