Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, March 28, 2023

TANZIA. KIGOGO WA SHINDANO LA MISS MOROGORO AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO.


Marehemu Cool Guy enzi za Uhai wake
Pyana [kati] waliosimama akiwa na Mwanaye kwenye mapokezi ya Simba mwaka 2017 walipofanikiwa kutwaa Ubingwa wa Tanzania;  

 

Picha hii ilipigwa na Mwandishi wa Mtandao huu kwenye moja ya hotel iliyopo Masika Manispaa ya Morogoro, ambapo Simba walifikia kwenye hotel hiyo walipotoka Dodoma kureja Dar es salaam.


 

TANZIA

Kigogo wa Mashindano ya Miss Morogoro na Miss Kanda ya Mashariki Masoud Mohamed Mulenga Almaarufu Cool Guy amefariki dunia jioni ya leo kwenye hospital ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

 

 Taarifa za kifo hicho zilizoumiza Mioyo ya wana Morogoro zimetolewa na Mdau Mkuwa wa burudani Mkoa wa Morogoro Pyana Mwandembwa ambaye pia alikuwa  mmoja wa Vigogo wa ngzi za juu wa timu ya ligi kuu ya Moro United. ‘Chelsea Bongo’

 

 lfahamike pia Hayati Mulenga alikuwa  Mdau Mkubwa wa Mtandao Pendwa wa Shekidele.

 

 “Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”

 

Tangulia kamanda Tutaonana Badaye.                         

 

Monday, March 27, 2023

KAMA UNASHINDWA KUMDEKEZA MPENZI WAKO ATADEKEZWA NA WENZIO.


 


KARIBU mpenzi msomaji wa Ulimwengu wa Mahaba, nikushukuru kwa maoni na ushauri wako iwe kwa SMS au kunipigia simu.

 

Mpenzi msomaji kama una mpenzi wako na ukashindwa kumbembeleza basi tegemea kubembelezewa na wanaume au wanawake wenzio.

 

Angalia usije ukaishia ku¬lalamika kila siku kuwa kila mpenzi unayekuwa naye unaibiwa, unapokonywa au anakuacha bila kujua sababu ya kuachwa kwako.

Penzi ni kitu  laini sana ambacho wala huwezi kukielezea.

 Na hata utamu wake ni mtamu ila huwezi kumuelezea mtu akauelewa uhalisi wa utamu wa penzi unaoumaanisha.

 

Hata hivyo penzi hilo limekuwa likiwatesa watu wengi sana wakiwemo wapenzi wachumba na hata wanandoa.

Kwa mtu ambaye hafahamu, mapenzi yanahitaji mambo mengi ili kulifanya penzi lako liweze kuendelea kudumu na kuwa bora, moja ya kitu hicho ni kubembelezana iwe kwa mwanaume au mwanamke na inapotokea hutengi muda wa kumbembeleza mpenzi wako basi tegemea kukaribisha usaliti ndani yako.

 

Hivi jaribu kutafakari kuwa umetoka ka-zini umevurugwa, kichwa kimejaa msongo wa mawazo ya kazi, maisha na mambo mengine halafu unafika nyumbani kwa mwenza wako ambaye ulidhani atakuwa sehemu ya kukubembeleza iwe kwa maneno au vitendo ili kukupunguzia msongo ulionao lakini yeye anaonekana yuko bize na hamsini zake akiperuzi mitandao ya Kijamii, unadhani nini utakuwa unawaza kwenye akili yako.

 

Ulitegemea kupata faraja kwa mwanamke au mwanaume uliyempenda lakini anakuwa ni sehemu ya tatizo la kukuongezea mawazo.

Bila shaka utajisikia vibaya na utamuona ni mwanamke au mwanaume asiye wa Ubavu.

 

Kama huwezi kumbembeleza mwenza wako ikatokea akapata mtu ambaye anamjali, anambem

beleza basi uwezekano wa kusalitiwa ni mkubwa sana.

 Kwani Mbembeleza mpenzi wako shilingi ngapi?Kumbembeleza  kunamfanya mwenza wako auhisi uhalali wa kukumiliki, ajione yeye ni mwenye bahati kubwa sana ya kupendwa. 

Unapombembeleza hata kama kichwa chake kinakuwa kimevurugwa lakini uwepo wako humfanya abadilike na kuchangamka kama hakuna jambo lolote gumu au lililomkwaza.

 

Katika kubembelezwa huku wanawake ndiyo hasa wanapenda na wanajua kuwa wanastahili wao zaidi kubembelezwa kuliko wanaume.

 

Kama wewe ni mwanaume hili unapaswa ulifahamu kuwa mwenzi wako anategemea nafasi kubwa zaidi ya wewe kumbembeleza.

Inawezekana hukuwa unalijua hili au ulijisahau basi ni vyema ukaelewa somo hili na kuliweka akilini mwako ikiwezekana hata ukalifanya kwa vitendo ili kuboresha uhusiano wako.

Kama ulikuwa hujui kuna wakati

anambembeleza¬

 

mwenza wako anatamani hata ashinde nawe ndani, mkicheza, mkitaniana, mkikwaruzana na michezo mingine ya kimapenzi lakini muda huo haupati kutokana na majukumu au mazingira yako ya kazi lakini ni vyema ukatenga hata siku yako ya mapumziko kushinda na kufurahia na mwenza wako kuliko kujifanya uko bize.

Kama utaendelea na ubize wako ipo siku utakuja kujutia kwani mwenza wako anaweza kufika sehemu akahisi labda pengine huna mapenzi naye, au upendo wako umeanza kuchuja au umepata mchepuko basi na yeye atatafuta mtu wa kumfariji.

 

Niwe Muwazi kwa sababu hata mimi pia kama binadam napita kwenye njia hizo hizo za mahusiano.

Kweli la kupenda kuna tatizo la baadhi ya wanawake na baadhi ya sisi wanaume kwamba.

Mpenzi wako akikuonyesha upendo wa kweli wewe hiyo unaifanya kama fimbo ya kumchapita.

Akikokosea kidogo unamfokea kisha unamnunia siku nzima akikusemasha unamjibu mkato hilo tatizo.

Tambua chuki inapunguza upendo kwa kasi kubwa na mwisho wa siku naye akinuna basi hapo hakuna tena penzi. Hapa chini ya juna hakuna mwanamke au mwanaume aliyekamilika hivyo tunapswa kubebeana madhaifu yetu. 

Kila mwanamke au mwanaume ukigombana naye kidogo badala ya kutafuta suluu ya kulinda uhusiano wenu wewe unakimbilia kuachana utaachana na wangapi? Kwa leo naweka nukta hapa tukutane wakati mwingine.

 

Sunday, March 26, 2023

ASKARI NA WAANDISHI WATAJWA KWENYE MANENO LA MUNGU.


Mwandishi wa habari Dustan Shekidele[kushoto] akiwa na Askari R.P.C Fortunatus Muslim wakiteta jambo.
Waandishi na Askari wametajwa kwenye neno hilo la Mungu hapo

 


 
LUKA.23 8-12
 
”Na Herode alipomwona Yesu,akafurahi sana kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona toka siku nyingi,maana amesikia habari zake,akataraji kuona ishara iliyofanywa nay eye. 
 
Akamuliza maneno mengi,yeye asimjibu lolote. Wakuu wa makuhani na Waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana. 
 
Basi Herode akamfanya duni,pamoja na askari wake akamdhihaki na kumvika mavazi mazuri kisha wakamrudisha kwa Pilato.
 
Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.”
 
Hilo ndilo neno letu la leo jumapili ya March 26
 
 
 

Saturday, March 25, 2023

KIJIWE NONGWA.









 
 
UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA
 
Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.
 
Kama kawaida mtumishi wako kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijamii kukusanya jumbe mbali mbali.
 
Miongoni mwa jumbe jizo ni za Kuelimisha, Kukosoa na Maneno ya hekima yanayotukumbusha kuwa jirani na Mwenyezi MUNGU. 
 
Tukutane Wiki Ijayo kwa mabango Mengine yenye Jumbe Moto Moto.
Shekidele Mkude Simba hana hatia.

Thursday, March 23, 2023

WAKALI WA NYWELE MORO



 

 KUMBUKIZI.

Mwanaume Nywele Bhana uweke Upara umefiwa?

 

Wakali wa Nywele Mkoani Morogoro Ras Richie ambaye ni Mpiga debe maarufu Stend ya Mabasi Msamvu akiwa na rasta zake zenye umri wa takribani miaka 10.

Kulia ni Msanii chipukizi wa sinema za kibongo kutoka Pande za Mji Mpya Manispaa ya Morogoro akiwa na style yake ya Nywele.

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...