Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 27, 2023

KAMA UNASHINDWA KUMDEKEZA MPENZI WAKO ATADEKEZWA NA WENZIO.


 


KARIBU mpenzi msomaji wa Ulimwengu wa Mahaba, nikushukuru kwa maoni na ushauri wako iwe kwa SMS au kunipigia simu.

 

Mpenzi msomaji kama una mpenzi wako na ukashindwa kumbembeleza basi tegemea kubembelezewa na wanaume au wanawake wenzio.

 

Angalia usije ukaishia ku¬lalamika kila siku kuwa kila mpenzi unayekuwa naye unaibiwa, unapokonywa au anakuacha bila kujua sababu ya kuachwa kwako.

Penzi ni kitu  laini sana ambacho wala huwezi kukielezea.

 Na hata utamu wake ni mtamu ila huwezi kumuelezea mtu akauelewa uhalisi wa utamu wa penzi unaoumaanisha.

 

Hata hivyo penzi hilo limekuwa likiwatesa watu wengi sana wakiwemo wapenzi wachumba na hata wanandoa.

Kwa mtu ambaye hafahamu, mapenzi yanahitaji mambo mengi ili kulifanya penzi lako liweze kuendelea kudumu na kuwa bora, moja ya kitu hicho ni kubembelezana iwe kwa mwanaume au mwanamke na inapotokea hutengi muda wa kumbembeleza mpenzi wako basi tegemea kukaribisha usaliti ndani yako.

 

Hivi jaribu kutafakari kuwa umetoka ka-zini umevurugwa, kichwa kimejaa msongo wa mawazo ya kazi, maisha na mambo mengine halafu unafika nyumbani kwa mwenza wako ambaye ulidhani atakuwa sehemu ya kukubembeleza iwe kwa maneno au vitendo ili kukupunguzia msongo ulionao lakini yeye anaonekana yuko bize na hamsini zake akiperuzi mitandao ya Kijamii, unadhani nini utakuwa unawaza kwenye akili yako.

 

Ulitegemea kupata faraja kwa mwanamke au mwanaume uliyempenda lakini anakuwa ni sehemu ya tatizo la kukuongezea mawazo.

Bila shaka utajisikia vibaya na utamuona ni mwanamke au mwanaume asiye wa Ubavu.

 

Kama huwezi kumbembeleza mwenza wako ikatokea akapata mtu ambaye anamjali, anambem

beleza basi uwezekano wa kusalitiwa ni mkubwa sana.

 Kwani Mbembeleza mpenzi wako shilingi ngapi?Kumbembeleza  kunamfanya mwenza wako auhisi uhalali wa kukumiliki, ajione yeye ni mwenye bahati kubwa sana ya kupendwa. 

Unapombembeleza hata kama kichwa chake kinakuwa kimevurugwa lakini uwepo wako humfanya abadilike na kuchangamka kama hakuna jambo lolote gumu au lililomkwaza.

 

Katika kubembelezwa huku wanawake ndiyo hasa wanapenda na wanajua kuwa wanastahili wao zaidi kubembelezwa kuliko wanaume.

 

Kama wewe ni mwanaume hili unapaswa ulifahamu kuwa mwenzi wako anategemea nafasi kubwa zaidi ya wewe kumbembeleza.

Inawezekana hukuwa unalijua hili au ulijisahau basi ni vyema ukaelewa somo hili na kuliweka akilini mwako ikiwezekana hata ukalifanya kwa vitendo ili kuboresha uhusiano wako.

Kama ulikuwa hujui kuna wakati

anambembeleza¬

 

mwenza wako anatamani hata ashinde nawe ndani, mkicheza, mkitaniana, mkikwaruzana na michezo mingine ya kimapenzi lakini muda huo haupati kutokana na majukumu au mazingira yako ya kazi lakini ni vyema ukatenga hata siku yako ya mapumziko kushinda na kufurahia na mwenza wako kuliko kujifanya uko bize.

Kama utaendelea na ubize wako ipo siku utakuja kujutia kwani mwenza wako anaweza kufika sehemu akahisi labda pengine huna mapenzi naye, au upendo wako umeanza kuchuja au umepata mchepuko basi na yeye atatafuta mtu wa kumfariji.

 

Niwe Muwazi kwa sababu hata mimi pia kama binadam napita kwenye njia hizo hizo za mahusiano.

Kweli la kupenda kuna tatizo la baadhi ya wanawake na baadhi ya sisi wanaume kwamba.

Mpenzi wako akikuonyesha upendo wa kweli wewe hiyo unaifanya kama fimbo ya kumchapita.

Akikokosea kidogo unamfokea kisha unamnunia siku nzima akikusemasha unamjibu mkato hilo tatizo.

Tambua chuki inapunguza upendo kwa kasi kubwa na mwisho wa siku naye akinuna basi hapo hakuna tena penzi. Hapa chini ya juna hakuna mwanamke au mwanaume aliyekamilika hivyo tunapswa kubebeana madhaifu yetu. 

Kila mwanamke au mwanaume ukigombana naye kidogo badala ya kutafuta suluu ya kulinda uhusiano wenu wewe unakimbilia kuachana utaachana na wangapi? Kwa leo naweka nukta hapa tukutane wakati mwingine.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...