KUTOKA 35-6
“Katwaeni kati yenu Matokeo kwa Bwana.Mtu awaye yote aliye na Moyo wa kupenda ayalete matokeo, dhahabu na fedha na Shaba”Hilo ndilo neno letu la Leo Jumapili November 13.
UCHAMBUZI WA NENO HILO.
Neno hilo la Mungu linatukumbusha sisi wanadamu kumtolea Mungu Sadaka kwa njia mbali mbali ikiwemo ya kuwasaidia watu wenye uhitaji, Mfano Wagonjwa, Yatima, Walemavu na kadharika.
Binafsi naamini hapa chini ya Jua Maisha hayana dhamani kwa kuwa na Mali nyingi, Cheo kikubwa au umaarufu Mjini.
Bali maisha yangu ya hapa dunia yatakuwa na dhamani kwa kugusa moja kwa moja maisha ya watu wenye uhitaji.
Tukumbuke kwenye utoaji tunakutana na changamoto nyingi hasa za kukatishwa tamaa na watu wetu wa karibu wekiwemo ndugu zetu.
Mfano kwenye kipato chako unaweka kutenga bajeti ya kusaidi watu wenye uhitaji lakini Mke au Mume anakuambia achana na jambo hilo, kama huna msimamo ukafuata ushauri huo Hasi‘Negative’unaweza kuhatarisha uhusiano wako mzuri na Muumba wako. USHUHUDA MZITO.
Nimeamua kutafuta ujumbe huo kwenye Biblia baada ya juzi kukutana na tukio la kukatishwa tama na rafiki yangu baada ya kunishuhudia nikiwakabidhi fedha Wagonjwa wa akili wanaookota Makopo na Chakula Jalalani.
Takribani Miaka 2 sasa Mungu amenipa Neema ya kuwapa msaada wagonjwa 5 wa akili ambao baadhi ya watu hupendelea kuwaita majina ya wenda wazimu au Machizi’ binafsi sipendi kutumia jina hilo napewa kutumia jina la kiungwa la wagonjwa wa akili.
Wagonjwa hao wa akili ambao ni maarufu katikati ya Mji wa Morogoro ni pamoja na Hamad Mnywa kahawa Maga Sharobaro. Castor. Kanyong’ole na Kifeku Rhumba Kondo,
hivyo kwa miaka yote 2 kila siku nikitoka nyumbani natenga shilingi elfu 2500 kwa maana kila mmoja shilingi mia 5.
Kituo chetu cha kukutana na ndugu zangu hao wote wanakijua ni pale Lunna kwa wauza Madafu jirani na Soko Kuu la Morogoro, baadhi yao huwa wananisubiri pale na wafanyabiashara waeneo hilo kwa maana ya wauza madafu, wauza magazeti, Mafundi baiskeli wote ni mashuhuda wa tukio hilo.
Kufuatia hali hiyo baadhi ya wagonjwa hao wa akili wamelikalili jina langu wakifika eneo hilo wasiponiona wanawauliza wafabiashara hao shekidele yuko wapi.?
Sasa juzi nilichelewa kufika Lunna wakati natokea Nyumbani nilipofika Mjini mzunguko wa barabara eneo la Posta Jirani na Ofisi ya Manispaaya Morogoro nikiwa na usafiri wa baiskeli Castor kaniona katimua mbio ananifuata kwa nyuma mimi sijamuona naendelea na safari watu wanashangaa nafukuzwa na mngonjwa wa akili.
Nikasikia sauti ya kike ikisema”Kaka ongeza mwendo yule chizi anakufukuza toka kule Posta”,nilivyogeuka nyuma nikamuona Castor nikasimama pembesoni mwa barabara ya zamani ya Dar es salaam kwa lengo la kumpatia Castor ujira wake.
Baada ya kuona nimesimama Castor kavuka barabata fasta bila kuchukua tahadhari kwenye barabara hiyo yenye msongamamo wa magari alipojaribu kuvuka kakoswa koswa kugongwa na gari.
Tukio hilo lilizua taharuki kwa watu waliokuwa eneo hilo wakishikwa na kutwaa awari livlivyokufukuzwa na Mgonjwa huyo wa akli lakipi pili alivyonusurika kugongwa na gari. Miongoni mwa mashuhuda hao alikuwepo pia rafiki yangu mmoja kwa busara jina lake nalihifaddhi, akanifuta na kuniuliza
” Shekidele mbona huyu chizi amekufukuza umbali mrefu kiasi kwamba alitaka kugongwa na gari” Nikamjibu huyu ni mtu wangu ambaye kila siku nampatia msaada wa fedha hivyo alivyoniona kamua kunifuata kwa mbio.
Rafiki huyo kaniambia” We shekidele unapoteza pesa zako bure na upati baraka yoyote kwa Mungu huyu Castor anakwenda kununua sigara hiyo pesa”alisema.
Nikamjibu kwamba sitoi sadaka au msaada kwa kipaumbele cha kubarikiwa bali natoa Msaada kwa kipaumbele cha mahusiano yangu mazuri na Mungu wangu hivyo msaada niliyompa simpangia cha kununua nimetimiza agizo la Mungu.
Chaajabu Muda leo nikiwa kwenye lbada kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya Morogoro kwenye mahuburi yake mtumishi wa mungu akifundishi somo la utoaji akitumia mstari wa Kumbukumbu ya Torati 16-17
” Kila Mtu na atowe kama awezavyo kwa kadri ya Baraka ya Bwana Mungu wako alivyokupa”
No comments:
Post a Comment