Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, November 13, 2022

MWANDISHI WA HABARI AZUSHIWA KIFO.

Mwandishi wa Mtandao huumwenye flana nyeupe akiwa kanisani akimuungamia Mungu wake
Mwandishi wa Mtandao huu akiangalia Muda kwenye Viwanja wa Gym Khana 'Gofu 'Morogoro

                   Mwandishi wa Mtandao huu akitafakari jambo


 

Na Mwandishi Wetu Morogoro.

 

 Mwandishi wa habari wa Siku nyingi Mkoani Morogoro Dustan Shekidele’Mkude Simba’Maarufu Ez Come Ez Go’jana jumapili majira ya asubuhi amezushiwa kifo na taarifa hizo zi sizo sahihi zilisambaa kwa kasi ya ajabu kwenye kijiwe cha Wapiga Picha kilichopo Lunna eneo la Ahamadya katikati ya Mji wa Morogoro.

 

Baada ya kuibuka kwa uvumi huo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Shekidele kwa lengo la kuzungumzia tukio hilo ambapo alipopatikana alifunguka yafuatayo.

 

”Kama ilivyokawaida yangu Jana jumapili nikiwa na afya njema niliamka majira ya saa 12 asubuhi nikajiandaa kuelekea Kanisani, majira ya saa 1na robo nilielekea kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya kuhudhuria lbada ya Pili inayoanza saa 1 na nusu.

Kwa kuheshimu lbada nilitoa mlio kwenye simu yangu majira ya saa 2 na nusu zimeanza kuingia simu mfurulizo nyingi zikiw ani za wapiga Picha na wamiliki wa stukio za kusafisha Picha Mkoani wa Morogoro.

 

Baada ya kuona simu hizo zinaingia kwa wingi na kusababisha na kunisababishia usumbufu niliamua kuzikata wahusika wakaendelea kupiga mtetemo huo wa simu hizo za muda mrefu zilipelekea paja langu kuuma kwani simu hiyo ilikuwa mfukoni nikaamua kuizima ili nipate utulivu kwenye lbada yangu.

 

lbada ilivyotamatika majira ya saa 3 na nusu nivyowasha simu tu ikaingia simu ya Msafirisha Picha wa Stukio ya Wahindi ya Seif Bw Hassan ambapo nilipopokea simu hiyo akiwa na sauti ya unyonge kaniambia kwamba kumekuja taarifa kwenye stuodi yao kwamba mimi nimefariki dunia.

 

Nikamueleza taarifa hizo zimeletwa na nani akaniambia mPiga Picha aitwaye Mbogo Mkazi wa Kasanga, nilipokata simu hiyo zikaanza kuingia simu nyingi zaidi ya 15 zote zikiwa ni za wapiga Picha wakitaka kujua kama kweli nimefariki au la niliwambia ni mzima wa afya na sina tatizo lolote.

 

Nilipomaliza kuongea na simu hizo niliwasha Pikipiki yangu nikaelekea kwenye Kijiwe hicho cha Wapiga Picha Ahmadya walipofika wapiga Picha wote wakaanza kunishangaa huku wengine wakinikumbatia kwa furaha wakiniambia maneno ya utani kwamba tumeambiwa muda huu huko kwenye majokovu pale Mochwari”alisema Shekidele

 

Baadhi ya wapiga Picha hao ni pamoja na Manyama, Hamis Gho’s na Tamba ambapo Tamba alisema.

 

 “Awari nilimpigia Shekidele simu imeita bila kupokelewa nikapiga tena simu imezimwa nikamua kumpiga Juma Mtanda Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi kumuliza akasema hana taarifa hizo lakini akaniambia ngoja aingie kwenye Group la Whatsapp la Waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro angalie kama kuna taarifa hiyo, kaingia hakuona taarifa hizo”alisema Tamba ambaye anamiliki studi ya kusafisha Picha za Passpot Size eneo la Ahmadya.

 

 Alivyoulizwa hatua atakazochukua kwa watu walioeneza uzishi huo wa uongozi juu yake na kusababisha taharuki na usumbufu mkubwa  Shekidele alisema.

 

” Binafsi sijajua walioeneza taarifa hizo walikuwanalengo gani, kama Mkristo safi tumeambiwa tusamehe 7x70 hivyo nimewasamehe huku nikiamini pia  baadhi yao waliosambaza habari hizo walikuwa na upendo  kwangu waliamini kweli nimefariki hivyo walisambaza habari hizo kwa nia vyema ya kuratibu Mazishi yangu.

 

Nilimtafuta Mpiga Picha Mboga kumuliza taarifa hizo za kifo changu alizipata wapi alisema aliambiwa na Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu anakitaja jina kwamba dent huyo alimueleza  aliingia kwenye Group la Whatsapp la chuo hicho na kukuta taarifa zilizodai Mwandishi wa habari na Mpiga Picha Maarufu Mkoani Morogoro Dustan Shekidele amefariki dunia.

 

Ndipo yeye Mbogo alipofunga safari mpaka Kijiwe cha Wapiga Picha Ahmadya na kusambaza taarifa hizo kwamba Mpiga Picha mwenzao Dustan Shekidele amefariki dunia hivyo wajipange kwa Mazishi.

 

Ndugu Mwandishi Mboga ametaja Chuo Kikuu hicho  kwangu mimi kwa kuwa sijaona habari hiyo kwenye Goup hilo  siwezi kutaja jina la Chuo hicho”alisema Shekidele.Alipotakiwa kusema jambo lolote juu ya tukio hilo Shekidele alisema

 

”Ninakauli matatu kama sio nne kwenye tukio hilo.

 

 Mosi- Nasisitiza tena kwamba nimewasamehe wote waliosambaza taarifa hizo pia nawapa pole watu wote waliopata usumbufu juu ya taarifa hizo.

 

Pili- Nahisi taarifa hizo zimeniongezea umri mrefu wa kuishi kwa mujibu wa Wahenga wetu. 

 

Tatu-.Niwaombe watu tukisikia taarifa tusifanyie utafiki wa kina kabla ya kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuondoa taharuki kama hizi.

 

Namini wakati wangu ukifika nitakufa na wapendwa wangu  mtanililia na kumisi vingi kutoka kwangu hasa habari moto moto za Mitaani.

 

Pia nafarijika nimezushiwa kifo nikiwa kanisani namuabudu Mungu wangu anayeendelea kunipa zawadi ya uhai.

 

Nne- Nashukuru taarifa hizi hazikufika kwenye familia ya Hayari Mzee Peter Shekidele yenye jumla ya watoto 7 nikiwa 5 kuzaliwa juu yangu kuna wakubwa zangu 4 na chini yangu kuna wadogo zangu 2.

 

Kati ya watoto hao 7 familia hiyo inajua fika kwamba Mtoto kipenzi cha  Bi Tumain Samwel Juma ‘Mrs Shekidele’ ni Dustan  kama mnavyojua Bi Mkubwa huyu ni Mgonjwa akiendelea na matibabu jijini Dar na juzikati nilifunga safari kwenda Dar kumjulia hali, sasa  kama angekumbana na taarifa hizo za  kifo ‘feki’ cha Mwanaye Kipenzi nahisi ingemletea shida zaidi kwenye afya yake.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...