Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 14, 2022

UDAKUZ SPESHO . MWENYENYUMBA ADAIWA KUMCHOMA KISU MPANGAJI WAKE.


 Mwenyekiti Bito akihojiwa na Mdakuzi wa Mtandao huu  kuhusiana na tukio hilo.

 

Na Mdakuzi Dunstan Shekidele, aliyezushiwa kifo

.

Kama kawaida tunakutana tena kwenye kipengele Pendwa cha Udakuzi Spesho ndani ya Mtandao Pendwa wa Shekidele unaosomwa na watu wengi Pande zote za dunia.

 

Leo Jumanne Mdakuzi anakurambisha Ubuyu wa baba Mwenye nyumba kudaiwa kumchoma kisu Mtangaji wake wa kike.

 

Katika hali ya kulinda uhusiano wake na baba mwenyenyumba inadaiwa Mpangaji huyo hakwenda kuripoti tukio hilo Polisi akihofia kufukuzwa kwenye nyumbani hiyo.

 

Tukio hilo la shambulizi la hatari limetokea Mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya nyumba  hiyo iliyopo Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa.

 

Baada ya kutokea kwa tukio hilo la kikatili baadhi ya wambeya walioshuhudia tukio hilo walimtwangia simu  Mdakuzi na kumpenyezea umbeya huo, fasta Mdakuzi alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi na ndani ya dakika 0 katinga eneo la tukio.

 

Kama ilivyo kanuni za Uandishi wa habari ukifika kwenye tukio kabla ya kuzungumza na wahusika awari unapaswa kuzungumza na Mashuhuda Mahakamani watu hao wanajulikana  kama Mashahidi.

 

Walipotakiwa kuzungumzia tukio hilo Mashuhuda hao walisema.

 

” Huyu Kijana[anamtaja Jina]yuko na ndugu yake wamerithi nyumbani hii ya marehemu wazazi wao, na kazi hafanya kila akipata kodi ana kwenda kunywa Pombe.

 

Leo alivyotoka kulewa  Mpangaji wake kamuliza kama amechukua sufulia yake ya kupigia, chaajabu baba mwenye nyumba huyo aliyekuwa na kisu mkononi akila Muhogo alichukizwa na swali hilo hivyo kwa hasira kamua kumchoma kisu mkononi dada huyo Mrembo.

 

Tukamwambia aende Polisi na baadae hospital, Cha kushangaza dada huyo kagoma kwenda Polisi akihofia kufukuzwa kwenye nyumbani  kwa kumshitaki baba mwenyenyumba wake.

 

Kaenda hospital tu huko sijui kadanganya vipi mpaka kapata matibabu tumemshuhudia kaludi akiwa amefungwa bendeji kwenye jeraha”walisema mashuhuda hao ambao ni wakulima wa Mboga mboga  kando kando ya Mto Morogoro uliopo jirani na nyumba hiyo.

 

Baada ya kupata maelezo hayo yaliyotukuka kutoka kwa Mashuhuda hao Mdakuzi kapata picha kamili ya tukio hilo na engo nyingi za kuwauliza maswali wahusika wa tukio hilo.

 

Mdakuzi aliwa kamili gado na vifaa vyake vya kazi katinga ndani ya nyumbani hiyo kwa lengo la kufanya mahojiano na wahusika wa tukio hilo,chaajabu wahusika wote kwa maana ya baba mwenyenyumba na Mpangaji wake wamegoma kumpa ushirikiano Mdakuzi wakidai kwamba hakuna tukio kama hilo  kwenye nyumba yao.

 

Kufuatia Majibu hayo  Mdakuzi kafunga safari hadi Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa River Side na kufanikiwa kuzungumza na Mwenyekiti wa Mtaa huo Bw Hashimu Bito ambapo alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo lililodaiw akutokea mtaani wake alisema taarifa hizo hazijafika kwenye ofisi yake.

 

” Shekidele sina taarifa za tukio hilo ila kama ni kweli huyo mpangaji ni mjinga huwezi ukafanyiwa ukatili huo ukaacha kuripoti ofisi ya kata au polisi kisa ukihofia kufukuzwa kwenye nyumbani kwani mtaa mzima nyumba ni hiyo moja kabla kama anakaa bure, any way umenitajia nyumba ngoja nifuatilie nitakupa mrejesho baada ya kuzungumza na wahusika wote wawili”alisema Mwenyekiti huyo.                       


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...