SP Morgan Marundo akijibu swali la Mwandishi wa Mtandao huu
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limedai ukosefu wa Silaha na Askari wa kutosha unapelekea vituo vidogo vya Polisi kutofanya kazi nyakati za usiku.
Hayo yalibainishwa kwenye kikao kazi kilichowakutanisha Waandishi wa habari na Vigogo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Bwalo la Umwema.
Kwenye kikao hicho kilichoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro,kilichokuwa na agenda kuu moja ya ‘Juu ya Usalama wa Mwandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro.
’Vigogo hao wa Polisi waliruhusu Waandishi wa habari kuliza Maswali,na moja kwa moja Mwandishi wa Mtandao huu alitumia fursa hiyo kuliza swali hili.
“Mimi naishi Mji Mpya miezi kadhaa iliyopita majira ya saa 6 usiku nikiwa kwenye pilika pilika zangu za kusaka habari nilikutana na mtu akiwa amebeba lundo la Viti nikamsimamisha na kuanza kumhoji juu ya kuwa lundo hilo la Viti usiku huo Mnene,maswali yalimpalia kajichanganya kujibu huku akitetemeke kama ‘Mayele’ akihisi Mimi ni Polisi.
Nilimbeba na viti vyake mpaka kituo cha Polisi, Kata ya Mji Mpya tulipofika kituo kimefungwa, nikamwachia nikaendelea na majukumu yangu eneo hili ambapo kuna habari nilikuwa naipeleleza eneo hilo hivyo haikuwa rahisi kuondoka eneo hilo kwenda kituo kikuu na Polisi na mtuhumiwa huyo..
“Swali la Msingi Uzoefu unaonyesha matukio mengi ya kihalifu hufanyika nyakati za usiku kwa nini vituo vidogo vya Polisi vinafungwa nyakati hizo za usiku ili hali mchana vinafanya kazi.?
Akijibu swali hilo Mwakilishi wa RPC.SP Morgan Marundo alijibu.
”Toka niaenze kazi ya Polisi sijaona lango kuu la Kituo Kikuu cha Polisi umefungwa,ni kweli saa 12 jioni vituo vidogo vya Polisi vinafungwa, hii ni sheria ndio maana vile vituo tumeandika ‘Polisi Post’sababu nyingine vituo vile havina Silaha pia havina Askari wa kutosha”alisema kigogo huyo wa Polisi na kuongeza.
”Nyakati hizo za Usiku maeneo yote ya Manispaa Polisi wako doria,Shekidele nyie Waandishi mna namba zetu za simu ungempigia Afisa yoyote wa Polisi fasta angewasiliana na polisi wa doria eneo hilo wangefika haraka,
au huyo mhalifu aliyeiba Viti ungemleta Kituo kikuu cha Polisi”alisema Afande Morgan.
Swali la nyongeza sisi Waandishi kweli tunazo namba za Vigogo wengi wa Polisi je kwa wananchi wa kawaida wote watakuwa na namba za Polisi?.
Kama hiyo haitoshi Majibu hayo ya Mwakilishi huyo wa RPC hayakumtoshereza Mwandishi nguli wa gazeti la Mwananchi Hamida Shariff ambaye aliuliza swali la nyonge.
“ Mimi naishi Lukobe eneo la Kwa Wagogo pale pana uhalifu sana nyakati za usiku hivi karibuni alikamatwa mwizi nyakati za usiku akiwa na vitu mbali mbali ikiwemo Tv na Radio wananchi walimbeba kwenye boda boda mpaka kituo kidogo cha Polisi Mazimbu Road.
Walipofika kituo kimefungwa wakaanza safari ya kuja kituo kikuu huku Mjini wakiwa njiani boda boda ikazimawakahangaika kupiga kiki kumbe mafuta yalikata kufuatia umbali mrefu, wakati dereva akihangaika kuwasha boda boda Mwizi kawaponyoka kakimbia”alisema Hamida.
lfahamike kutoka Lukobe Mpaka kituo Kikuu cha Polisi ni umbali wa takribani kilometa 8.
Mtandao huu unamuomba Amiri Jeshi Mkuu Mama yetu Samia Suluhu Hassan’SSH’na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Wambura kuviongezea vitendea kazi vituo hivyo vya Polisi kisha kuruhusu kufanya kazi nchini nzima kwa Masaa 24 kuondoka kadhia hiyo ya wananachi.
BADO SIKU 13 SENSA TUJIANDAE KUHESABIWA
No comments:
Post a Comment