Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 16, 2022

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI. BAND YA MAISHA MAPYA YA NYAKUA WANAMUZIKI KUTOKA TWANGA PEPETA NA WALUGURU OG



Mnenguaji Mpya wa band ya Maisha Mapya kutoka Twanga Pepeta akifanya yake wakati wa utambulisho juzi ljumaa
                                        Sabrina akinengua




Mwanamuziki Sabrina akiimba Wimbo Copy wa Jide

                    Wasanii hao wakihojiw ana Mlala Nnje
Wasanii wanamuziki hao wapya wakiwajibika jukwaani




               Husna Ramadhan akifanya yake kwa raha zake

.

 

Na Mlala Nnje Dunstan Shekidele,Morogoro. 

BAND Pendwa mkoni Morogoro inayokua kwa kasi ya ajabu Maisha Mapya Music Band’Wana Full Vipaji’ wiki iliyopita wamewatambulisha wanamuzi wapya kutoka band kubwa nchini za African Stars’Twanga Pepeta’ya jijini Dar na Waluguru Original ya Mkoani Morogoro.

 

Mlala Nnje akiwa kwenye pilika pilika zake za kusaka matukio kwenye kumbi mbali mbali za burudani Mkoani Morogoro, ijumaa iliyopita majira ya saa 5 usiku ilitinga kwenye onyesho la band hiyo inayoongozwa na Vijana wadogo waliokomaa Vichwa kwa Ugumu wa Maisha wakiwatambulisha wanamuziki hao wa kike.

 

 Zoezi la utambulisho huo limefanyika kama yale matamasha ya Simba Day na lile la Yanga  Day Maarufu Siku ya Mwananchi yaliyofanyika wiki iliyopita wakiwatambulisha wachezaji wao Wapya. Wakati Mlala Nnje anaingia kwenye ukumbi Mmoja jina kapuni uliopo maeneo ya Mazimbu, mmoja wa wamiliki wa band hiyo Abubakar Pugi alimfuata Mlala Nnje na kumtonya kwamba siku hiyo ya ljumaa walifanya tukio la Utambulisho wa wanamuzi wao wapya.

 

Kweli majira ya saa 6 usiku zoezi hilo lilifanyika ambapo wa kwanza kutambulishwa alikuwa Sabrina Danger Kutoka Band ya Waluguru Og ambaye yeye anapiga Miguu yote miwili kwa maana kwamba anaimba na kunengua ambapo alipotambulishwa alipanda jukwani alianza kuimba wimbo wa Copy uliopigwa wa Msanii Jide.

 

Lisong hilo linakwenda kwa jina la Siwema lenye mahudhui ya’Sibabaiki na sura, nahitaji tabia njema, nimezunguka bara na Visiwani’.

 

Baada ya kuimba wimbo huo Msanii huyo aligongewa Sebene kavu kavu akanza kuwasha Moto akionyesha udanger wake kweli kweli na kukong’a nyoyo za Mashabiki.

 

Msanii huyo aliposhuka Jukwaani, Mc wa utamburisho huo Rapa wa Band hiyo Yahya Masauti alimwita jukwaani Mcheza shoo Mourine V.A.R Kutoka Twanga Pepeta akiwa na lundo la Nywele kama Mkia ya Kondoo Mnenguaji aliuwasha moto Mkali kwa Style za Pinda mugongo.

 

 Siku hiyo ilikuwa ni balaa kubwa waliokosa shoo hiyo ya utamburisho wa wanengauji hao italudiwa keshokutwa Alhamis  kwenye ukumbi  namba 2 wa JKT Bwalo la Umwema uliopo ndani ya Stend Mpya ya daladala ya Mafiga eneo la Mnada wa Nyama Choma.

 

Baada ya utambulisho huo  Maingizo hayo mapya baadae walijumuika na wanenguaji wa zamani wa band hiyo Kavera  One Brother na Husna Mama Lao.

 

Picha za wanamuziki hao wapya ziko hapo chini ya stori hii zicheki.

BADO SIKU 7 SENSA TUJIENDAE KUHESABIWA

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...