Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 14, 2022

LICHA YA CHANGAMOTO MUNGU ENDELEA KUIMALISHA IMANI ZET




 


 

 Na Mtumishi Dunstan Shekidele,

 

Nawasalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo,tukimshukuru Mungu kwa kuendelea kutupa zawadi ya uhai, kuna ndugu zetu waliitamani zawadi hii lakini siku zao za kuishi hapa duniani zimefika kikoma wameiaga dunia kwa njia ya kifo.

 

 

Baada ya salam hizo ambazo ni agizo la Mitume wetu wakisema, wanaosalimiana wana kheri kwa Mwenyezi Mungu, moja kwa moja ningie kwenye Mada yetu ya neno la Mungu linalokujia kila siku za Jumapili kupitia Mtandao wako Pendwa wa Shekidele.

 

Jumapili ya Leo Agost 14 nitakuwa tofauti kidogo hatutachambua neno la Mungu badala yake tutazungumzia baadhi ya watu wanaowavunja moyo watumishi wa Mungu wanaojitoa kufanya kazi ya Mungu.

Tumesoma kwenye maandiko kwamba Mtumishi Ayubu alikuwa mchana Mungu mzuri  aliyeyatoa maisha yake kumtumikia Mungu kwa hali na Mali.

 

Baadae Mungu alijaribu lmani ya Ayubu kwa kumpa maradhi ya Muda mrefu akiota majipu Mwili mzima, alijitibia bila mafanikio, watu wengi akiwemo mkewe walimwambia maneno ya kumkatisha tamaa.

 

”Huyo Mungu unayemuabudu ni Mungu gain?mbona hakuponyi unateseka miaka yote bora uachane naye” walisema watu hao akiwemo mkewe.

 

 Maneno hayo haya kumkatisha tamaa Ayubu hakuludi nyuma aliendelea  kumtazama Mungu akizidi kuimalisha kimani.

 

Kwa sasa hapa dunia kuna baadhi ya watu wakiwemo watumishi wa Mungu wanapitia mapito kama ya Ayubu,wanakatishwa tamaa na ndugu na jamaa zao kwa matendo mazuri wanayomfanyia muumba wao, miongoni mwa watu hao ni pamoja na Mwandishi wa habari hizi.

 

Takribani miaka 6 iliyopita wakati Mwandishi huyo anaendelea na ujenzi wa nyumba yake kwa kusua sua kufuatia udogo wa kipato chake, alikuja mchungaji wa kanisa la Tanzania Assemblies of  God’TAG’akamwambia.

 

”Tulikuwa tunaabudu kwenye boma[nyumba inayoendelea kujengwa]  hapo mtaa wa pili mmiliki wa boma hilo kamuzia mtu mwingine na aliyenunua katuondoa hivyo kwa kuwa unaeneo kubwa hapa kwako tunaomba tujenge kaniza la Muda wakati tunajipanga kununua eneo letu”. alisema Mchangaji huyo.

 

Mwandishi huyo alimjibu” Vyote ni Mali wa Bwana Kwa kuwa ujengi Baa wala Gest unajenga nyumba ya lbada ya kumtukuza Mungu karibu umjengee Mungu  kanisa lake”

 

Baada ya kanisa hilo kujenga na watumishi wa Mungu kuanzi lbada baadhi ya ndugu zangu wa damu na Majirani zangu walinifuata na kuniambia maneno ya kukatisha tamaa juu ya uamuzi wangu huo wa kuruhu Mungu kujengewe nyumba yake ya lbada kwenye eneo la ngu.

 

Baadhi ya ndugu waliniambia” Kanisa hilo la TAG linapesa baadae watakushawishi kwa pesa nyingi uwauzie eneo hilo”.

 

 Nikawajibu  “hakuna mtu yoyote aliyenipa hata senti tano kwenye ununuzi wa kiwanja na ujenzi wa nyumba hiyo hivyo,  naheshimu ushauri wenu kama ndugu zangu lakini kwangu mimi Mungu kwanza Mali badae, haya maboma tutakufa tunayaacha hivyo yasitutenganisha na lmani zetu na Muumba wetu”.

 

Baada ya kuwajibu hivyo hakuna ndugu yangu yoyote aliyekuwa na swali la nyongeza wote walikaa kinya. 

                MAJIRANI SASA.

Baada ya ndugu changamoto ikahamia kwa majirani, baadhi yao walinitia moyo wakinipongeza kwa kuruhusu kanisa kujengwa kwenye eneo langu hao wote walifanya hivyo Mungu awabariki sana, lakini wengine walinivunja moyo wakisema.

 

’Hao walokole uliowakaribisha watakupigia kelele nyumbani kwako kinachoniumiza zaidi wengine wanaosema hivyo ni wakristo wa madhehebu ya Sabato,. KKKT.na Roman Katoliki na wale wa dini nyingine.

 

 Nilichowajibu Majirani hao ni kwamba kelele hizo za maombi yanayofanywa nyumbani kwangu ni baraka  kubwa kwenye  nyumba yangu na Maisha yangu kwa ujumla.

 

Kwenye kanisa hilo lbada ni kila  Jumapili kuanzia saa 3 asabuhi mapaka saa 7 mchana hivi ninavyoandika habari hizi niko hapa nyumbani lbada lnaendelea, baada ya hapo lbada yao nyingine ni  ljumaa  mkesha unanza saa 1 usiku mpaka saa 12 alfajiri.

 

Cha kushangaza hapo jirani  kuna nyumba  2 zina baa.

 

 Mziki unapigwa kila siku kuanza asubuhi mpaka usiku pia kuna kelele za wanywaji wa Vilevi pia kuna kibanda umiza wanaonyesha Mipira kwenye Luninga, si zani kama wenye kuna mtu aligonga hodi kwa wamiliki wa nyumba hizo kuwashauri kuruhusu kelele za baa hizo, lakini wamekuwa na ujasili wa kuja kwangu kunihoji kelele za maombi ya Mungu. .

 

 Kanisa  hilo litakuwepo hapo nyumbani  mpaka wenyewe wakatapo pata eneo lao na kuamua kuondoka kwa hiyali yao wenyewe.

 

Namuomba Mungu azidi kunipa lmani hiyo nisikatishwe tamaa na maneno ‘Negative’ya walimwengu wanaoingalia leo yao na kuipa kisogo kesho yao.

 

Kwa leo naishia hapa Mungu akipenda tukutane jumapili ijayo kwa Jumbe wa Mungu.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...