Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, August 13, 2022

ALICHOFANYA MSANII TUNDA MAN KWENYE TAMASHA LA SIMBA DAY SIO SAWA.

 

Mwandishi wa Mtandao huu kushoto akitenda Jambo na Tunda Man siku alipofunga ndoa na Mtoto wa Kiarabu Sabra Hussein Balhaboou. Msomi wa Chuo Kukuu Mzumbe
 
                Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
 
Agost 8 timu ya Simba ilifanya Tamasha lao la 14 la ‘Simba Day’kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar huku Msanii Tunda Man akiingia kwenye Tamasha hiyo na Jeneza lenye Msalama.
kwenye Matamasha hayo Simba huandaa burudani mbali mbali kwa lengo la kunogesha siku yao hiyo muhimu wanayoifanya kwa Mwaka mara Moja.
 
Tamasha la Mwaka huu limetiwa doa na Msanii Khalid Ramadhan’Tunda Man’ aliyedhiaki dini ya Kristo kwa kuingia na Jeneza huku wasaidizi wake wakivalia mavazi yanatumiwa na Viongozi wa dini hiyo.
 
lkumbukwe Kazi ya Mwandishi wa habari ni Kuhabarisha,kuelimisha, Kuburudisha na Kukosoa.
Licha ya kwamba Tunda Man ni rafiki yangu na kwenye harusi yake iliyofanyika Kata ya Mazimbu Morogoro takribani miaka 5 iliyopita shekidele alikuwa Mpiga Picha wa harusi hiyo iliyofana.
 
Lakini kwenye hilo ulilofanya la kudhihaki dini ya Mwenyezi Mungu, rafiki yangu Tunda umepotoka pakubwa sana, najua kwenye matamasha hayo ya Simba na Yanga kila Msanii anataka kuonyesha utofauti kwenye tukio hilo.
 
Si sawa hata kidogo kufanya utofauti wa kudhihaki dini au lmani za watu wengine, kama ulitaka utofauti basi ungevaa gauni la mkeo hakuna mtu ambaye angekulalamikio. 
 
Tumeona wasanii kama Lucas Mkenda’Joti’anakuwa wa tofauti kwa kuvaa nguo za kike, hakuna mtu anayemlalamikia kazi yake inaendelea.
 
Naamini Joti angeigiza kwa kuingia kwenye jeneza lenye Msalama, kama ulivyofanya wewe wenyedini yao wasingekubali wangetoka hadharani na kutoa lalamiko lao kwa Mamlaka zinazohusika.
Nakumbuka siku za nyuma kiongozi mmoja wa dini aliwaeleza waumini wake kwamba ni kosa kubwa kudhihaki dini au imani ya mtu mwingine.
 
”Ni bora ukachezea ugari lakini sio dini au maneno Matakatifu ya Mwenyezi Mungu”.
 
Baada ya Msanii huyo wa Muziki wa kizazi kipya kufanya dhiaki hiyo kwenye Tamasha hilo la Simba Day. 
 
Siku iliyofuata Maaskofu walijitokeza hadhani na kuonyesha masigitiko yao wakilalamikia dini yao kudhihakiwa na Msanii huyo.
Baadae Uongozi wa Simba walioandaa Tamasha hilo na kumwalika Msanii huyo walijitokeza hadharani kuwaomba Radhi Maskofu hao na waumini wote wa dini ya Kikristo kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...